Mimi UKIMWI bado nipo

Mimi UKIMWI bado nipo

Mohamed Ismail

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
228
Reaction score
249
Msiache mbachao kwa msaala upitao. Naona mmenizoea sana mpaka na kuamua kunitelekeza. Mliniogopa sana kipindi cha mwanzo hadi mkapelekea kuniita majina mabaya ambayo hata mimi yalikuwa yananikera. Nimeitwa umeme, miwaya, ngoma, mdudu na kila aina ya jina baya.

Sikuja hapa ulimwenguni wa nia mbaya bali na mimi ni kiumbe kama viumbe wengine nastahili kuishi. Tamaa zenu za mwili na ujinga wenu ndio umekuwa ukiwaponza miaka yote. Kweli hata vitabu vinasema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mlivyozidi kuteketea nyinyi wanadamu msiyokuwa na haya mkaanza na kuniogopa wengine ni ndugu kabisa wa damu wakapelekea kunyanyapaana kisa mimi.

Leo hii najiuliza sasahivi mmekuwa na ujasiri wa kutoniogopa kiasi hicho. Ila nikakumbuka kuwa kwa shujaa kuna kilio. Ujasiri wenu kwangu unawaponza sasahivi mnateketea sana wengine bado vijana wadogo. Ninacheka sana eti mnapeana elimu ya kutumia mipira wakati mnasahau kupambana na chanzo asili.

Naona sasahivi hizi dawa zinawadanganya na kuwapa ujeuri kumbuka hizi kazi yake haziwezi kuniua. Zinanilewesha nikiamka na hang over napata supu ya moto na soda baridi nazidi kuwatekeketeza nyinyi kwa sababu mmenibip wenyewe sasa mimi nawapigia.

Acheni kiburi cha huo ubinadamu wenu. Ebu tafakari umekuja kufanya nini ulimwenguni. Nchi yako inakutegemea na wewe ni nguvu kazi. Familia yako inakutegemea kama umeoa au kuolewa au bado hujaingia kwenye majukumu ya ndoa. Kumbuka unahitaji kutengeneza kuwa na familia bora na ambayo itakutegemea uwepo wako. Kiburi na jeuri lako vimekuponza sasa hivi umekufa. Umeacha vilio na simanzi katika familia yako na jamii yako kwa ujumla. Kuna watu walikutegemea sasahivi wanabaki angekuwepo angefanya hiki kisa tu kiburi chako na tamaa zako za kipumbavu.

Naona kuna wajasiriamali wenye akili walikaa wakaona kuwa huu ujinga wa baadhi ya wanadamu ni fursa kwetu. Wameibatiza siku ya leo eti mnaniadhimisha ila nashukuru sana kwa kunipa heshima hii. Nakushauri tu wewe unayesoma ujumbe hu mimi bado nipo sana na nina nguvu kama zamani ukijichanganya umekwisha. Cha muhimu pendananeni na mshirikiane ukiona mwenzio hajui chochote mnongoneze sikioni kuwa mimi bado nipo na ninaua kama zamani. Atakayeziba sikio lake huyo muache tutapambana maana asiyesikia la mkuu muache guu lake livunjike na achechemee na akishachechemea na maisha yake yatachechemea.

Mnachopaswa kujua mimi sina huruma na nyinyi mkijichanganya kwenye kumi na nane zangu. Nimemtumia ndugu yenu Mlimwengu awafikishie ujumbe huu. Aaya sherehe njema ila mimi bado nipo.
Wako
VVU (Virusi Vya Ukimwi)

Imeandikwa na Mohamed Ismail(Mlimwengumimi)
Email: mohammedismail613@gmail.com
Phone no: 0762070361
 
Mabaharia kwenye kikao chetu tumefikia azimio hatupimi mpaka dawa ipatikane
78867479_176431733547897_3882762572885131264_n.jpeg
 
Hongera ummy mwalimu na timu yako na wahusika wote mmefikisha ujumbe vizuri kupitia ili jukwaa wiki hii yote kama ni atention mmeitengeneza bila shaka mwenye masikio na anayejua kusoma amepata ujumbe.
 
Sitaweza kuiacha nyeto, kwanza haina ukimwi, hutumii gharama, muda wowote unakupa starehe bila ya usumbufu, na haina maumivu ata ukiiwacha
 
Mabaharia na ile Team yetu ya Uvinza FC, tuwe makini sana.

Games zote za ligi kuu na zile mechi za UEFA tumekaniwa sana aisee! Tuwe makini mno.

Kikao kijacho tunaongeza mbinu za kibaharia uwanjani. Tumieni hizi zilizopo kwanza
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom