Mimi si mpenzi wa vyama vya siasa, ila kwa sera hizi CUF hamna upinzani Zanzibar zaidi ya vyombo vya dola

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Ukombozi wa Pili kote Zanzibar na Bara, baada ya kusalitiwa kwa Mapinduzi ya 1964 na Uhuru wa Tanganyika wa 1961 ndio malengo ya mapambano yetu.

1. Kurejesha Zanzibar iliyotawaliwa kijanja na Tanganyika kupitia Muungano kandamizi. Sambamba na kuwang'oa vibaraka wa Tanganyika waliopo Zanzibar wanaoendesha Nchi kwa misingi ya kibaguzi na kibabe kwa nguvu za Tanganyika huku kukikosekana tumaini la maisha bora yenye heshima kwa wazanzibari.

2. Halkadhalika kuhakikisha Uhuru wa Tanganyika wa 1961 unatamalaki kwa watanganyika wote na sio kwa misingi ya ubaguzi wa kikabila, kikanda, kidini na kitabaka. Sambamba na kuhakikisha raslimali za Nchi zinawanufaisha wananchi wote na sio tabaka tawala pekee.

3. Kuhakikisha utawala bora wenye misingi ya sheria, haki, usawa, demokrasia, uwazi na heshima kwa raia unakuwa ndio Dira ya Taifa letu.
CUF tumeanza kupigania haya tokea 1992 bila Ruzuku kutoka Serikalini. Pia CUF imeandamwa kwa majaribio mengi yaliyosukwa na Dola ya kutaka kuisambaratisha. Tumewahi kuendesha Chama chetu kwa mafanikio makubwa bila Ruzuku. Pia tumefanikiwa kukiokoa Chama chetu kutokana na majaribio mengi ya Dola kutaka kukisambaratisha.

Hivi sasa tunakiendesha Chama na tutaendelea kikiendesha kwa mafanikio makubwa bila ya Ruzuku. Wanachama wanaongeza hamasa na ari ya kubeba gharama za kukiendesha Chama chao. Kila wakibana Ruzuku wanachama wanazidi kuhamasika. Binafsi hata sina chembe ya kilio endapo Msajili kwa kushirikiana na Dola watamgaia Ruzuku yote kibaraka wao Lipumba na genge lake watie mifukoni.

Pamoja na taasisi 5 za Dola hadi sasa, Polisi, Msajili wa vyama vya siasa, RITA, NEC na Bunge kuungana kujaribu kuisambaratisha CUF bado Chama kipo Madhubuti kinaendelea kupigania malengo yake.

CCM na Dola rejeeni nyuma kidogo katika kauli ya Mzee Mwinyi "vyama vyote vitakufa ila ni vigumu kuuwa CUF kwa sababu CUF ina MALENGO thabit".
 
Ni Kweli mkuu CUF hawana upinzani zanzibar ila wana upinzani na vyombo vya dola
 
Cuf imekufa kifo cha mende, kama wewe ni mwana Cuf hamia ACT kwetu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom