barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,820
Mimi ni kama nimemuelewa Mwalimu wangu Prof Ndalichako,Mhadhiri wangu wa "Measurement and Evaluation",gwiji wa elimu na mawanda yake anayetekeleza kazi kwa uweledi mkubwa katikati ya miluzi mingi ya kisiasa.Dhamira yake ni kuturudisha katika mstari mkuu,lakini kwa sababu kwa miaka zaidi ya 20 walioko katika "mfumo" na walio katika madaraka ni sehemu ya "elimu ya kuungaunga" basi lazima atazubaishwa na kelele hizo.
Tatizo ni kuwa hata katika baraza la mawaziri ambalo yeye ni sehemu yake,wapo wanaoguswa na maamuzi haya,wanaweza wasipige kelele hadharani,lakini wakatumia watu kupiga kelele ili kumpoteza nahodha katika muelekeo sahihi.Tumeishi kiujanja ujanja kwa miaka mingi,kuanzia kwenye elimu mpaka kwenye maisha ya kawaida.Ukichanganyia na hizi siasa za "Post-Truth Politics",basi kweli watu wanarusha mawe kwa Prof Ndalichako bila kuwa na taarifa kamili.
Mchanganyo ulianza kwa hii NACTE na TCU,hawa ndio walianza kuchanganya "madesa".Unakuta chuo kipo K'koo mtaa wa Narung'ombe,kimesajiliwa na NACTE na hakijulikani na TCU,kimechukua vyumba viwili vya kupanga gholofa ya pili,kinatoa "certificate" ya "Front Office and Secretarial studies","Hotel and Tourism","Clearing and Fowarding" nk.
Anatoka mtu na Division IV.28,amerudia mtuhani mara nne akiwa na booklet ya vyeti vya form four,anakatiza njia ya mkato na kuchukua Certificate mtaa wa Narung'ombe na baadae anaunga Diploma kwenye vyuo hivi vya "kibiashara" pale "Aviation University of Tanzania" pale TABATA MAGENGENI juu ya jengo la bank ya CRDB.Mtu huyu anaunganisha certificate yake ya "Hotel and Tourism",diploma ya "Flight Dispatcher and Air Ticketing" anaamua kuomba degree ya Information Technology pale chuo Kikuu kilichopo Mbezi kwa Yusuf ambacho chenyewe huchukua tu kila mtu ili mradi uwe na ada.
Mfumo huo juu ulizalisha watu "wabovu" kitaaluma,na hii ni kutokana na utaratibu wa hovyo wa mawasiliano butu kati ya NACTE na TCU.Ukimsikiliza Prof hajasema juu ya Diploma zenye mtiririko sahihi,bali zile za kuungaunga kama kamba ya kokoro.Wapo walioanza kuhoji wale wenye PhD wakitokea Diploma,wanasahau hawa walitoka kidato cha sita,wakaenda ualimu enzi za Kasulu TTC,Tabora TTC,Mkwawa TTC ambapo diploma ilisomwa kwa miaka mitatu.
Enzi za FTC ya uhakika ya Mbeya Tech,Dar Tech na Arusha Tech.Huku kote Mama Ndalichako hajakugusia na kukataa.Ndalichako hajawananga wale walimu walioanza na Certificate,diploma ya ualimu na hatimaye degree.
Ugomvi wa Ndalichako ni kwa wale wa "Foundation",maana kila chuo kilichukua usajili NECTA na kutoa "bridging course".Ilikuwa ni pesa yako tu.Matangazo yakaongezeka kwenye "Education Centres" na vyuo vya mtaani..."Soma hadi kidato cha 4 na 6 kwa miaka 3",..."Pata elimu ya degree bila kupitia form six kwa mwaka mmoja".Hata kama elimu ni biashara lakini si kwa njia hizi za mkato.
Kama tunataka elimu bora,tuweke mjadala wa kitaifa,tutazame sera na tuitungie sheria na kuirudisha elimu yetu katika mstari.Ndio maana sasa "Tafiti" za elimu ya Masters zinauzwa kama inavyouzwa vocha ya simu.Tumeuwa "Tertiary institutions" na kuondoa mafundi mchundo,tumeondoa vyuo vya ufundi na kada ya kati na kuzalisha "mameneja" wanaokosa wa kuwaongoza.Dhana ni kuwa ni "lazima" kila mtu anatakiwa kuwa na degree hata kama hakuwa na sifa hizo.
Mimi nimemuelewa Mwalimu wangu Ndalichako,labda tusaidiane kueleweshana pale tusipomuelewa vizuri.Mwisho wa siku ni imani yangu kuwa Profesa Ndalichako ana nia nzuri ya kurudisha elimu yetu katika njia kuu