Mimi nimemuelewa vizuri Prof. Ndalichako na ninamuunga mkono 100%

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg

Mimi ni kama nimemuelewa Mwalimu wangu Prof Ndalichako,Mhadhiri wangu wa "Measurement and Evaluation",gwiji wa elimu na mawanda yake anayetekeleza kazi kwa uweledi mkubwa katikati ya miluzi mingi ya kisiasa.Dhamira yake ni kuturudisha katika mstari mkuu,lakini kwa sababu kwa miaka zaidi ya 20 walioko katika "mfumo" na walio katika madaraka ni sehemu ya "elimu ya kuungaunga" basi lazima atazubaishwa na kelele hizo.

Tatizo ni kuwa hata katika baraza la mawaziri ambalo yeye ni sehemu yake,wapo wanaoguswa na maamuzi haya,wanaweza wasipige kelele hadharani,lakini wakatumia watu kupiga kelele ili kumpoteza nahodha katika muelekeo sahihi.Tumeishi kiujanja ujanja kwa miaka mingi,kuanzia kwenye elimu mpaka kwenye maisha ya kawaida.Ukichanganyia na hizi siasa za "Post-Truth Politics",basi kweli watu wanarusha mawe kwa Prof Ndalichako bila kuwa na taarifa kamili.

Mchanganyo ulianza kwa hii NACTE na TCU,hawa ndio walianza kuchanganya "madesa".Unakuta chuo kipo K'koo mtaa wa Narung'ombe,kimesajiliwa na NACTE na hakijulikani na TCU,kimechukua vyumba viwili vya kupanga gholofa ya pili,kinatoa "certificate" ya "Front Office and Secretarial studies","Hotel and Tourism","Clearing and Fowarding" nk.

Anatoka mtu na Division IV.28,amerudia mtuhani mara nne akiwa na booklet ya vyeti vya form four,anakatiza njia ya mkato na kuchukua Certificate mtaa wa Narung'ombe na baadae anaunga Diploma kwenye vyuo hivi vya "kibiashara" pale "Aviation University of Tanzania" pale TABATA MAGENGENI juu ya jengo la bank ya CRDB.Mtu huyu anaunganisha certificate yake ya "Hotel and Tourism",diploma ya "Flight Dispatcher and Air Ticketing" anaamua kuomba degree ya Information Technology pale chuo Kikuu kilichopo Mbezi kwa Yusuf ambacho chenyewe huchukua tu kila mtu ili mradi uwe na ada.

Mfumo huo juu ulizalisha watu "wabovu" kitaaluma,na hii ni kutokana na utaratibu wa hovyo wa mawasiliano butu kati ya NACTE na TCU.Ukimsikiliza Prof hajasema juu ya Diploma zenye mtiririko sahihi,bali zile za kuungaunga kama kamba ya kokoro.Wapo walioanza kuhoji wale wenye PhD wakitokea Diploma,wanasahau hawa walitoka kidato cha sita,wakaenda ualimu enzi za Kasulu TTC,Tabora TTC,Mkwawa TTC ambapo diploma ilisomwa kwa miaka mitatu.

Enzi za FTC ya uhakika ya Mbeya Tech,Dar Tech na Arusha Tech.Huku kote Mama Ndalichako hajakugusia na kukataa.Ndalichako hajawananga wale walimu walioanza na Certificate,diploma ya ualimu na hatimaye degree.

Ugomvi wa Ndalichako ni kwa wale wa "Foundation",maana kila chuo kilichukua usajili NECTA na kutoa "bridging course".Ilikuwa ni pesa yako tu.Matangazo yakaongezeka kwenye "Education Centres" na vyuo vya mtaani..."Soma hadi kidato cha 4 na 6 kwa miaka 3",..."Pata elimu ya degree bila kupitia form six kwa mwaka mmoja".Hata kama elimu ni biashara lakini si kwa njia hizi za mkato.

Kama tunataka elimu bora,tuweke mjadala wa kitaifa,tutazame sera na tuitungie sheria na kuirudisha elimu yetu katika mstari.Ndio maana sasa "Tafiti" za elimu ya Masters zinauzwa kama inavyouzwa vocha ya simu.Tumeuwa "Tertiary institutions" na kuondoa mafundi mchundo,tumeondoa vyuo vya ufundi na kada ya kati na kuzalisha "mameneja" wanaokosa wa kuwaongoza.Dhana ni kuwa ni "lazima" kila mtu anatakiwa kuwa na degree hata kama hakuwa na sifa hizo.

Mimi nimemuelewa Mwalimu wangu Ndalichako,labda tusaidiane kueleweshana pale tusipomuelewa vizuri.Mwisho wa siku ni imani yangu kuwa Profesa Ndalichako ana nia nzuri ya kurudisha elimu yetu katika njia kuu
 
Iv hakuna watu wenye PhD waliyopitia foundation? Uhu uwamuzi asicheki degree tu acheki kote pia hiyo foundation haikuwa kisheria?
 
Kikubwa wengi wanaopinga haya mambo wana maslahi ya moja kwa moja au vinginevyo.Hivi kweli tukiangalia tu,mitihani ya madarasa ya nne,la saba,na kidato cha pili ipo kisiasa tu,sio kwa lengo la kupata wenye uwezo wanaotakiwa.
Sasa mpaka mfumo wa vyuo upo hovyo kama waziri alivyo baini.
Halafu mtu anakosoa bila kutoa suluhisho,bali kwa kutaka goli lipanuliwe tu mechi iwe rahisi.
 
tulioelewa tujitahid kusema ukweli mtaani maana cku hiz uongo unavumishwa Sanaa kwa mtaa
 
Mm nimemuelewa prof Ndalichako tangu kitambo.

Ninaomba tusimung'unye maneno kwa hili. LAZIMA UWE UMEFAULU KIDATO CHA 6 NDIPO UPATE isipokuwa wale waliopita shule za ufundi. SHAHADA. Kinyume na mtiririko huu ni kuungaunga elimu.

Walio ungaunga elimu hata wakiwa maprofesa bado uwezo wao ni mdogo mno. Ndiyo hao ambao wanampinga waziri.

Ktk nchi yetu tuna maprof wengi lkn hawana tija kabisa. Nje ya kazi ya kufundisha wanalia njaa. Mifano Iko Mingi Sana Sina Haja Ya Kuwataja.
 
Mkuu barafu ukiishiwa misumari ya kupigia majeneza nijulishe "supply" bado ipo.

Nisingeshangaa kama raisi Lungu na wa Chad wazee wa mikakati kama wasingekuja Tanzania kupeana ushauri na raisi JPM, wana maono sana watu hawa.
 
Nimemuelewa sana huyu Prof. Tunahitaji mawaziri km hawa kumi tu ..nchi itaenda hii
huyuhuyu aliewaambia walim kusimamia na kusahihisha mitihan ni kazi yao,unajua jinsi walimu wetu walivyonachuki na huyo bibi?umesahau kua aliwaambia serikali imelipa maden yao yote ilhali hata robo ya wanaodai hawakulipwa?fanya research,nikukumbushe na yale matamko yake ya hovyo kuhusu ada elekezi kwa shule binafsi?ina maana umesahau hata ukatili alioufanya kwa wadogo zetu udom kufukuzwa kama mbwa au wakimbizi tena usiku?tunasahau mapema sana
 
Mkuu wote tulimwelewa Waziri Ndalichako 100% zaidi yako kwamba ALIKOSEA 100% ndiyo maana within 24 hours Ndalichako akafanya U TURN -360 degrees. 100%!

Hapa hakuna Waziri ama ndugu ya Waziri anayetumia PROXY kuleta mada kuhusu Elimu. Bali ni raia wenyewe. Na kwamba she needs to think before she leaps!

Elimu ni sekta sensitive sana. Mtu ASIPOKUWA MAKINI anaweza kufikiri anajenga na kumbe anabomoa. Kuwahusisha WADAU wa Elimu si UDHAIFU bali ni kupata inputs zao zitakazo kusaidia kufanya maamuzi yasiokuwa na UTATA!

Umetoa maelezo kibao na unasema TAFITI za Masters zinauzwa kama VOCHA.
Na kama ni kweli Hiyo pia inaongeza FAILURE yake kama waziri.Naona hujamsadia ila UNAMSHITAKI!!!

Maana SIKU HIZI kuna SOFTWARE Maalumu inayogundua kama TAFITI ama THESIS ni PLAGIARISED/ Ya wizi.
Hivyo basi anahitaji kulifanyia kazi hilo ulilolitoa ili kuzuia UDANGANYIFU!
Nimempa RAI ya bure bila malipo!
 
Back
Top Bottom