Mimi nimemuelewa vizuri Prof. Ndalichako na ninamuunga mkono 100%

KIWANGO CHA ELIMU KIMESHUKA KULIKO TUNAVYODHANIA. WATU WANA VYETI ELIMU HAWANA. RAFIKI YANGU AMEMALIZA MASOMO YA DARASANI, MASTERS, LAKINI THESIS KAANDIKIWA NA MTU KWA GHARAMA YA MILIONI MBILI. ILIPOPELEKWA KWENYE SOFTWARE KUANGALIA WIZI IKAKUTWA KAIBA(PLAGIARISE) 90%. HUYU MWANAFUNZI NI KILAZA HANA MFANO NASHANGAA TESTS NA HOMEWORKS ALIKUWA ANAPITA VIPI. LAKINI VILE VILE WAPO WATU WANAISHI KWA KUJIBU HOMEWORKS ZA WANAFUNZI (HASA WA MASTERS) KWA MALIPO.
NDALICHAKO SONGA MBELE
Mkuu hali hii hata mimi nimeshuhudia kwa macho yangu,ukienda pale Ubungo Hostel eneo la kusomea ndio utajua ukweli wa hili jambo.Mama anapoanza kubana,watu wanaanza kupiga mayowe
 
AINA ZA WASUKUMA NA KISUKUMA

Lugha ya kisukuma ina lahaja kuu nne; ginantuzu, ginang'weli, ginangw'agala na gidakama. Vivyo hivyo, Wasukuma wamegawanyika katika misingi ya lahaja za lugha ya kisukuma.

1.Bhadakama. Hawa wanapatikana sehemu za mji wa Shinyanga, sehemu za Gahama na sehemu za Igunga na Nzega. Kwa idadi, hawa ndiyo Wasukuma wachache sana. Ni watu wenye aibu, wakimya mno... wana muingiliano na utamaduni wa Wanyamwezi. Pengine hawa ndiyo Wasukuma masikini kuliko aina yoyote ya Wasukuma!

2. Bhanang'weli.
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa mikoa ya Mwanza, Geita, na kusini - Magharibi mwa Mkoa wa SIMIYU. Kiidadi, hawa ndiyo Wasukuma wengi sana... katika ongea yao, wana matumizi mengi ya 'shi' kwa mfano, shikolo, shiliwa. Pia hawatumii 'ng'wadila' katika salamu za jioni. Wao hutumia 'gawiza' au 'dillo gawiza' Kwa sababu wanaishi katika strategic areas, wana muingiliano na watu wa makabila mbalimbali. Au tuseme wamemezwa na watu wa kuja. Ukienda Geita wenyeji hawaonekani, labda kukimbiza daladala za baiskeli. Mwanza ndiyo usiseme kabisa.

3. Bhanang'wagalla.
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa Wilaya za Meatu, Kishapu na Maswa na sehemu za Igunga. Ukikutana nao ni rahisi mno kuwasikia wakisema, 'yombaga bhahebhu', ong'wawiya, kaaa, aghayaa... ni nadra sana kuwasikia wakisalimia, 'ng'wadila' Wao hufupisha, 'dilla mayu' au dilla bhabha. Majina ya maeneo mengi huanza na Ng'wa. Kwa mfano, ng'wabagimu, ng'wajidalala, ng'wanhuzi... Utajiri wao uko kwenye mifugo.
Vijana wa huko hulizika mapema. Kwa mfano, kama mavuno ya matobholwa, karanga, alizeti na pamba ni mazuri, vijana wa maeneo haya hushinda kwenye ngoma za jadi. Hawajui kusaka ridhiki nje ya maeneo yao, utafikiri wako kisiwani. Wanaotoka nje ya maeneo yao ni wafugaji tu. Wanawake wa huko hupenda kuvaa shanga kiunoni na shingoni ingawa sio wajuzi wa mambo ya Tanga. Wavulana nao huvaa miguuni. Soko la wasichana liko juu sana. Pengine huu ukanda, hasa Meatu, ndiyo unaongoza kwa kutoa mahari kubwa Tanzania nzima.

4.Bhanantuzu /Wanyantuzu
Hawa ni Wasukuma wenyeji wa Wilaya za Bariadi na Itilima. Hawa ndiyo Wasukuma waliotapakaa kila kona ya nchi hii. Na pengine bila ya hawa kabila la Wasukuma
lisingejulikana kwa namna hii. Kisukuma chao hakina 'shi' bali hutumia 'si' kwa mfano, sikolo, siliwa....Jamaa hawa wanajua kuchakalika kutafuta mali. Hawaogopi kitu, hawaogopi mtu. Jamaa hawa ndiyo Wasukuma pekee wanaothubutu kwenda kupora ng'ombe za Wamasaai. Ni Wasukuma wenye dharau na mikogo mingi. Kama unasikia watu wanaopenda utani na masihara, basi hawa ni kiboko. Si unamjua Danni Makanga? Mambo ya ujanja ujanja na upigaji dili, hapa ndipo penyewe. We mwangalie Chenge tu, au hata Cheyo au hata Mbunge Njaru. Utanipa jibu. Wanaume wa huko hupenda kuoa wake weupe. Kama sio mweupe basi awe na sifa za ziada. Michepuko kwa mwanaume ni kitu cha kawaida.

Swala la ni msukuma yupi anaongoza kwa ushamba na ukilaza, halikuwa lengo la utafiti huu. Mobheja sana.
Moderator nafikiri hii ya bwana Lupyeee imepotea njia
 
Tatizo humu ndani mnanunuliwa. Jambo la elimu ni pana sana. Nilishawahi kusema elimu ndio kila kitu. Kwahiyo ni jambo halihitaji mihemko wala uvyama. Tunatakiwa kujua tunatoka wapi na tunakwenda wapi. ELIMU ndio uti wa mgongo wa taifa lolote duniani. Tunatakiwa tutafakari kwa kina ELIMU sio mtu mmoja.
 
Jadilini ELIMU kwa mustakabali wa nchi na watu wake. ELIMU inagusa kila mtu. Bavicha na CCM nao wanawatoto. Msikubali kununuliwa na yyt katika kujadili ELIMU. Wala kutetea uozo. Mtu mmoja hawezi kuendesha ELIMU ya nchi hii. Tunahitaji mjadala mpana.
 
Mimi nilimuelewa toka mwanzo, ukiangalia ile video alifanunua vizuri ila nadhani watu wengi walisoma hii habari juu juu na kuanza kutokwa povu.
 
Mimi nilimuelewa toka mwanzo, ukiangalia ile video alifanunua vizuri ila nadhani watu wengi walisoma hii habari juu juu na kuanza kutokwa povu.
Na ukiiangalia ile video,basi unapata picha ya alichokiongea huyu Mama.Ila kuna watu wana maslahi yao kisiasa na wanataka kumtoa Mama njia kuu
 
View attachment 441134
Mimi ni kama nimemuelewa Mwalimu wangu Prof Ndalichako,Mhadhiri wangu wa "Measurement and Evaluation",gwiji wa elimu na mawanda yake anayetekeleza kazi kwa uweledi mkubwa katikati ya miluzi mingi ya kisiasa.Dhamira yake ni kuturudisha katika mstari mkuu,lakini kwa sababu kwa miaka zaidi ya 20 walioko katika "mfumo" na walio katika madaraka ni sehemu ya "elimu ya kuungaunga" basi lazima atazubaishwa na kelele hizo.

Tatizo ni kuwa hata katika baraza la mawaziri ambalo yeye ni sehemu yake,wapo wanaoguswa na maamuzi haya,wanaweza wasipige kelele hadharani,lakini wakatumia watu kupiga kelele ili kumpoteza nahodha katika muelekeo sahihi.Tumeishi kiujanja ujanja kwa miaka mingi,kuanzia kwenye elimu mpaka kwenye maisha ya kawaida.Ukichanganyia na hizi siasa za "Post-Truth Politics",basi kweli watu wanarusha mawe kwa Prof Ndalichako bila kuwa na taarifa kamili.

Mchanganyo ulianza kwa hii NACTE na TCU,hawa ndio walianza kuchanganya "madesa".Unakuta chuo kipo K'koo mtaa wa Narung'ombe,kimesajiliwa na NACTE na hakijulikani na TCU,kimechukua vyumba viwili vya kupanga gholofa ya pili,kinatoa "certificate" ya "Front Office and Secretarial studies","Hotel and Tourism","Clearing and Fowarding" nk.

Anatoka mtu na Division IV.28,amerudia mtuhani mara nne akiwa na booklet ya vyeti vya form four,anakatiza njia ya mkato na kuchukua Certificate mtaa wa Narung'ombe na baadae anaunga Diploma kwenye vyuo hivi vya "kibiashara" pale "Aviation University of Tanzania" pale TABATA MAGENGENI juu ya jengo la bank ya CRDB.Mtu huyu anaunganisha certificate yake ya "Hotel and Tourism",diploma ya "Flight Dispatcher and Air Ticketing" anaamua kuomba degree ya Information Technology pale chuo Kikuu kilichopo Mbezi kwa Yusuf ambacho chenyewe huchukua tu kila mtu ili mradi uwe na ada.

Mfumo huo juu ulizalisha watu "wabovu" kitaaluma,na hii ni kutokana na utaratibu wa hovyo wa mawasiliano butu kati ya NACTE na TCU.Ukimsikiliza Prof hajasema juu ya Diploma zenye mtiririko sahihi,bali zile za kuungaunga kama kamba ya kokoro.Wapo walioanza kuhoji wale wenye PhD wakitokea Diploma,wanasahau hawa walitoka kidato cha sita,wakaenda ualimu enzi za Kasulu TTC,Tabora TTC,Mkwawa TTC ambapo diploma ilisomwa kwa miaka mitatu.

Enzi za FTC ya uhakika ya Mbeya Tech,Dar Tech na Arusha Tech.Huku kote Mama Ndalichako hajakugusia na kukataa.Ndalichako hajawananga wale walimu walioanza na Certificate,diploma ya ualimu na hatimaye degree.

Ugomvi wa Ndalichako ni kwa wale wa "Foundation",maana kila chuo kilichukua usajili NECTA na kutoa "bridging course".Ilikuwa ni pesa yako tu.Matangazo yakaongezeka kwenye "Education Centres" na vyuo vya mtaani..."Soma hadi kidato cha 4 na 6 kwa miaka 3",..."Pata elimu ya degree bila kupitia form six kwa mwaka mmoja".Hata kama elimu ni biashara lakini si kwa njia hizi za mkato.

Kama tunataka elimu bora,tuweke mjadala wa kitaifa,tutazame sera na tuitungie sheria na kuirudisha elimu yetu katika mstari.Ndio maana sasa "Tafiti" za elimu ya Masters zinauzwa kama inavyouzwa vocha ya simu.Tumeuwa "Tertiary institutions" na kuondoa mafundi mchundo,tumeondoa vyuo vya ufundi na kada ya kati na kuzalisha "mameneja" wanaokosa wa kuwaongoza.Dhana ni kuwa ni "lazima" kila mtu anatakiwa kuwa na degree hata kama hakuwa na sifa hizo.

Mimi nimemuelewa Mwalimu wangu Ndalichako,labda tusaidiane kueleweshana pale tusipomuelewa vizuri.Mwisho wa siku ni imani yangu kuwa Profesa Ndalichako ana nia nzuri ya kurudisha elimu yetu katika njia kuu
Na hawa hawa wanaondaliwa kwa zima moto ndio hupelekwa kufundisha, hapa elimu isishuke?
 
Mm nimemuelewa prof Ndalichako tangu kitambo.

Ninaomba tusimung'unye maneno kwa hili. LAZIMA UWE UMEFAULU KIDATO CHA 6 NDIPO UPATE isipokuwa wale waliopita shule za ufundi. SHAHADA. Kinyume na mtiririko huu ni kuungaunga elimu.

Walio ungaunga elimu hata wakiwa maprofesa bado uwezo wao ni mdogo mno. Ndiyo hao ambao wanampinga waziri.

Ktk nchi yetu tuna maprof wengi lkn hawana tija kabisa. Nje ya kazi ya kufundisha wanalia njaa. Mifano Iko Mingi Sana Sina Haja Ya Kuwataja.

Ni kweli kabisa na ukitaka kuthibitisha ingia bookshop yoyote kama utaviona vitabu vilivyoandikwa na wasomi wetu.! Halafu nenda hapo Nairobi utakuta authors wazawa wamejaza mashelfu. Yaani hawa wakwetu hata fiction books za kuikosoa serikali kiaina na kivichekesho hawawezi? Hata madaktari na wanasayansi wetu hawawezi kuweka uzoefu na utafiti wao kwenye vitabu ili tujisomee na nyongeza maarifa?
 
Nisingekubaliana na wewe zaidi.Hongera kwa uchambuzi mwanana.
View attachment 441134
Mimi ni kama nimemuelewa Mwalimu wangu Prof Ndalichako,Mhadhiri wangu wa "Measurement and Evaluation",gwiji wa elimu na mawanda yake anayetekeleza kazi kwa uweledi mkubwa katikati ya miluzi mingi ya kisiasa.Dhamira yake ni kuturudisha katika mstari mkuu,lakini kwa sababu kwa miaka zaidi ya 20 walioko katika "mfumo" na walio katika madaraka ni sehemu ya "elimu ya kuungaunga" basi lazima atazubaishwa na kelele hizo.

Tatizo ni kuwa hata katika baraza la mawaziri ambalo yeye ni sehemu yake,wapo wanaoguswa na maamuzi haya,wanaweza wasipige kelele hadharani,lakini wakatumia watu kupiga kelele ili kumpoteza nahodha katika muelekeo sahihi.Tumeishi kiujanja ujanja kwa miaka mingi,kuanzia kwenye elimu mpaka kwenye maisha ya kawaida.Ukichanganyia na hizi siasa za "Post-Truth Politics",basi kweli watu wanarusha mawe kwa Prof Ndalichako bila kuwa na taarifa kamili.

Mchanganyo ulianza kwa hii NACTE na TCU,hawa ndio walianza kuchanganya "madesa".Unakuta chuo kipo K'koo mtaa wa Narung'ombe,kimesajiliwa na NACTE na hakijulikani na TCU,kimechukua vyumba viwili vya kupanga gholofa ya pili,kinatoa "certificate" ya "Front Office and Secretarial studies","Hotel and Tourism","Clearing and Fowarding" nk.

Anatoka mtu na Division IV.28,amerudia mtuhani mara nne akiwa na booklet ya vyeti vya form four,anakatiza njia ya mkato na kuchukua Certificate mtaa wa Narung'ombe na baadae anaunga Diploma kwenye vyuo hivi vya "kibiashara" pale "Aviation University of Tanzania" pale TABATA MAGENGENI juu ya jengo la bank ya CRDB.Mtu huyu anaunganisha certificate yake ya "Hotel and Tourism",diploma ya "Flight Dispatcher and Air Ticketing" anaamua kuomba degree ya Information Technology pale chuo Kikuu kilichopo Mbezi kwa Yusuf ambacho chenyewe huchukua tu kila mtu ili mradi uwe na ada.

Mfumo huo juu ulizalisha watu "wabovu" kitaaluma,na hii ni kutokana na utaratibu wa hovyo wa mawasiliano butu kati ya NACTE na TCU.Ukimsikiliza Prof hajasema juu ya Diploma zenye mtiririko sahihi,bali zile za kuungaunga kama kamba ya kokoro.Wapo walioanza kuhoji wale wenye PhD wakitokea Diploma,wanasahau hawa walitoka kidato cha sita,wakaenda ualimu enzi za Kasulu TTC,Tabora TTC,Mkwawa TTC ambapo diploma ilisomwa kwa miaka mitatu.

Enzi za FTC ya uhakika ya Mbeya Tech,Dar Tech na Arusha Tech.Huku kote Mama Ndalichako hajakugusia na kukataa.Ndalichako hajawananga wale walimu walioanza na Certificate,diploma ya ualimu na hatimaye degree.

Ugomvi wa Ndalichako ni kwa wale wa "Foundation",maana kila chuo kilichukua usajili NECTA na kutoa "bridging course".Ilikuwa ni pesa yako tu.Matangazo yakaongezeka kwenye "Education Centres" na vyuo vya mtaani..."Soma hadi kidato cha 4 na 6 kwa miaka 3",..."Pata elimu ya degree bila kupitia form six kwa mwaka mmoja".Hata kama elimu ni biashara lakini si kwa njia hizi za mkato.

Kama tunataka elimu bora,tuweke mjadala wa kitaifa,tutazame sera na tuitungie sheria na kuirudisha elimu yetu katika mstari.Ndio maana sasa "Tafiti" za elimu ya Masters zinauzwa kama inavyouzwa vocha ya simu.Tumeuwa "Tertiary institutions" na kuondoa mafundi mchundo,tumeondoa vyuo vya ufundi na kada ya kati na kuzalisha "mameneja" wanaokosa wa kuwaongoza.Dhana ni kuwa ni "lazima" kila mtu anatakiwa kuwa na degree hata kama hakuwa na sifa hizo.

Mimi nimemuelewa Mwalimu wangu Ndalichako,labda tusaidiane kueleweshana pale tusipomuelewa vizuri.Mwisho wa siku ni imani yangu kuwa Profesa Ndalichako ana nia nzuri ya kurudisha elimu yetu katika njia kuu
 
Kinachotawala kwenye maofisi ya umma na hata ukifuatilia hapa jf ni watu kutamba na MBA, bachelors, PhD na maprofesa wakati kinachotamba kwenye ofisi za binafsi is what someone delivers kulinganisha na elimu yako. Sote tunajua maofisi ya umma value for money and work sio muhimu sana kama ilivyo kwa sekta binafsi.
Anachofanya Prof. Ndalichako ni kureverse hii hali na kwa vyovyote vile walalamishi wa mwanzo ni victims!
 
Kama unaelewa maana ya elimu na kuthamini maana ya elimu, nina maana maarifa, afanyalo Prof Ndalichako utaliunga mkono na kuomba litokee tu. Elimu haiwezi kuwa biashara hata siku moja. Waanzisha vyuo wengine walianzisha kama biashara na wanagawa alama hovyo za GPA ili kuwavuta wateja, kwani wanaoenda huko nao wanahitaji alama sio maarifa. Kwa kuwa kuna mwanya TCU na NACTE waliacha, wakabaki kuangalia alama tu, wkaingia mkenge, wakajikuta wanaadmit watu wasiokuwa na sifa hata.

Awali system zilikuwa sahihi, hao walimu mnaosema wa certificate wanarudia hata mitihani ya form four anapata credit then anasoma diploma mwaka wa kwanza lazima afanye mtihani wa form 6 kumqualify asome diploma. Sasa nisichokielewa inakuwaje vyuo ambavyo hata walimu wake sifa za ufundishaji wanazijua wenyewe wapewa mamlaka ya kumpa mtu A ya kujiunga na Chuo Kikuu? Hiki ni chuu kikuu (higher learning institution) lazima uchujwe uchujuke kuingia hapo. Otherwise, tutatalalamika sana.
Ajabu kuna watu ni jambo la kawaida analipa mtu anaandikiwa masters' thesis yake. Jamani tuwe makini, tukiyafumbia macho haya yatatula wenyewe.

Aidha, Prof. Ndalichako nakupongeza, songa Mbele, hakuna anayejua maana ya elimu atakayepiga kelele unless ana agenda zake binafsi. Nani hafahamu kuwa hivyo vyuo ni dili.
Uwezi fananisha vyuo vya nje na quality za diploma zetu, wao wana good quality assurance mechanism ya kuangalia na kupima qualities za waalimu na mitaala, hivyo vyuo vyetu vinavyo?, inakuwaje basi chuo kianzishwe buguruni au kariakoo kinafundishwa na walimu wasiokuwa na sifa then watoe diploma na tuje tuipigie kelele eti itumike kupeleka mtu chuo kikuu? Tuache siasa elimu lazima ithaminiwe daima.
 
Kinachotawala kwenye maofisi ya umma na hata ukifuatilia hapa jf ni watu kutamba na MBA, bachelors, PhD na maprofesa wakati kinachotamba kwenye ofisi za binafsi is what someone delivers kulinganisha na elimu yako. Sote tunajua maofisi ya umma value for money and work sio muhimu sana kama ilivyo kwa sekta binafsi.
Anachofanya Prof. Ndalichako ni kureverse hii hali na kwa vyovyote vile walalamishi wa mwanzo ni victims!
Umemaliza kabisa shemeji yangu lukindo
Ni usanii mtupu na elimu za makaratasi bila utendaji,Sasa Prof anataka kuwarudisha watu njia kuu,then wanaanza siasa na kupiga kelele
 
Umemaliza kabisa shemeji yangu lukindo
Ni usanii mtupu na elimu za makaratasi bila utendaji,Sasa Prof anataka kuwarudisha watu njia kuu,then wanaanza siasa na kupiga kelele
Hebu jiulize eti mtu ni CEO wa shirika kubwa la umma na analipwa million 45 kwa mwezi, tukihoji "tunaambiwa ni majukumu na status ya shirika". Kaja JPM akakoroma kuwa hakuna bosi yeyote wa shirika la umma anapaswa kulipwa zaidi ya million 15 na asiyetaka aache kazi. All over a sudden bosi yule yule wa 45m anakubali kulipwa 10m na kuimba [HASHTAG]#hapakazitu[/HASHTAG], hivi kweli mtu kama huyu unaweza kumwamini anachosema na anachotenda!?
Tukiamua kuishi kwa uhalisia mengi yatafunuka na tusisahau kuwa hakuna dhambi ya kuwa darasa la saba kama isivyo dhambi kuwa na PhD, cha msingi tufuate taratibu na viwango.
 
Sasa kama mtu hiyo Masters au PhD ni ya kuungaunga unafikiri atahoji nini?
 
Mkuu upo sahihi,hivyo vyuo vya njia ya mkato,unakuta mtu anapita chuo cha huko anaibuka na certificate sijui ya accounts,anaibukia diploma mara huyooo kwenye degree.Sasa hizi njia ndio Mama Ndalichako hazitaki,lkn watu wanataka kupotosha
Yani hapa ndipo huwa nawashangaa watanzania kwa kutokujua tatizo liko wapi la kuzungumzia.
Hata kwa jinsi uanavyoeleza inaonyesha wazi kuwa tatizo si mwanafunzi wala mfumo, tatizo ni vyuo na elimu itolewayo, hivyo basi kama anataka mabadiliko angeanza kudeal na vyuo pamoja na elimu yake kwani huu mfumo uko popote duniani na ndio maana ukazusha msemo wa ELIMU HAINA MWISHO.
Tusilazimishane njia uliyopita wewe nami nipite hatujawa nyumbu sisi, sisi ni binadamu wenye mawazo tofauti.
 
Back
Top Bottom