Mimi nimejifunza kitu hapa. Wewe Je??

Mimi nimejifunza kitu hapa. Wewe Je??

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
564
Reaction score
1,567
UNAMALIZAJE MWAKA

Muhubiri 7:8 Heri mwisho wa neno kuliko mwanzo wake,Na mvumilivu rohoni kuliko mwenye roho ya kiburi.

Tunamshukuru Mungu ametupa Neema ya kuiingia mwezi December... Mwezi wa mwisho mwaka huu haikuwa rahisi yapo mengi yawezekana yalituumiza yalitujeruhi..lakin yapo yaliyotufurahisha yapo yaliyotubariki .....Yote tunapaswa kumshukuru Mungu kwa yote..Mungu wetu habadiliki kulingana na majira wala matukio yeye anabaki kuwa yule yule!!

Swali ninatamani tujiulize pamoja....unamalizaje mwaka huu?....nini umebeba kwenye moyo wako?je UMEBEBA HERI?...Haijalishi ulianzaje mwaka haijalishi wapi ulianguka haijalishi nani alikujeruhi haijalishi nani alikudharau..haijalishi ulifanikiwa au hukufanikiwa jiulize unamalizaje?

Wale wanaokimbia mbio za marathon kuna wanaanza kwa speed lakin wengine wanaanza taratibu usiangalie wanaanzaje Ila kinachotazamwa wamemalizaje? Wengine pumzi huishia njiani wengine huanguka ktkt ya mbio wengine huumia japo walianza vizuri lakin wanaishia njiani na wengine walianza taratibu lakin wakamaliza kwa ushindi wakavaa medali

Ni ombi langu kwa Mungu umalize mwaka kwa ushindi..usiangalie ulianzaje Bali tazama unamalizaje?....yes you can [emoji123][emoji123][emoji123][emoji123]

Usimalize mwaka kinyonge...kama kuna watu umewabeba moyoni hakikisha huvuki nao mwaka waachilie ...umewabeba vya kutosha umewapa lift sasa inatosha let them gooooo.......Kuwa Huru katika Jina la Yesu!

Nawatakia Baraka za Mungu tunapomalizia mwaka huu 2018...tumepitia mengi tumeona mengi na TUTAMALIZA KWA USHNDI
 
Back
Top Bottom