Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
.
Anaandika Wakili Msomi Emmanuel Kihaule
______________________________________________
Suala na urais wa TLS limefanya kila kalumekenge na kalumanzila kuwa mtaalam wa sheria huku wakijifanya wanaijua vyema katiba yake pamoja na sheria na kanuni zake za uchaguzi. Cha kuchekesha hakuna hata mmoja anayetaja kipengele au sheria iliyokiukwa na jinsi unavyofuatilia mijadala unaona ni jinsi gani wapo weupe kwenye uwanja huu!
Mimi ni wakili na pia ni mwana TLS na pia sipendi siasa ziingie kwenye mambo yetu, lakini upo wapi ushahidi kwamba siasa imetumika mpaka katika shughuli zake? Mpaka sasa ni maoni na hisia binafsi zinatumika kujenga hoja.
Sishabikii yeyote kati ya wagombea na bahati mbaya sitakuwepo Arusha kupiga kura lakini sioni sababu ya kampeni hii chafu! Ooh huyu au yule akichagulia anaweza kufanya hiki au kile kwa sababu tu yeye ni mwanasiasa!
Toka lini sheria ikahukumu leo kosa linalohisiwa litakuja kufanyika baadae? Kama mpaka sasa mtu amekidhi vigezo sasa tatizo ni nini? Labda kuna sababu zaidi ambazo zikiwekwa upenuni tunaweza kushawishika.