SoC02 Mimi ni nani

Stories of Change - 2022 Competition

asim

New Member
Sep 12, 2022
4
0
MIMI ni NANI

Ni asubuhi niliyokua naisubiria kwa hamu sana na mwili wangu hauwezi kuvumilia kuonyesha shauku niliyokuwa nayo. Nahisi kama moyo wangu unadunda kwa kasi sana huku viganja vya mikono yangu vikitetemeka kwa furaha. Nashindwa kujizuia “Baba tunaondoka saa ngapi” niliuliza kwa kukosa uvumilivu “aah! Abdul , unashindwa kusubiri hata dakika moja tu” baba alijibu akitokea chumbani kuja sebuleni nilipokua nimeketi kwenye sofa. “haya beba begi lako twende stendi”alisema baba huku akielekea kwenye mlango wa kutokea nje, nilichukua begi langu na kumfuata huku nikigeuka nyuma kuangalia mlango wa chumbani kwa baba kama mama atatokea au la “ mama yako atakuja tu , sisi tutangulie kwanza” baba aliniambia baada ya kuona namtafuta mama.Mimi na baba tulitoka nje na kuanza safari ya kuelekea stendi taratibu ili kumsubira mama ambaye kwa sasa alikuwa nyuma yetu akitukimbilia .

Punde tulifika stendi kwani hapakuwa mbali na nyumbani na lichukua dakika tatu tu kwa mwendo wa kawaida ,mama nae alikuwa kashatufikia tayari , na wote tulipanda gari lilioandikwa kwa kifupi B/moyo T/nyuki likimaanisha Bagamoyo Tegeta nyuki .

Safari ya kueleka Gongo la mboto kwa shangazi Mariamu ambayo niliisubiria kwa hamu kwa wiki mbili bila kuchoka sasa ilkuwa tayari imeanza .Mimi ,Baba na Mama tulikaa kwenye siti za nyuma kabisa , mimi nikiwa nimepakatwa na baba upande wa dirishani, sehemu spesheli kwa ajili yangu. Nilipenda sana kushangaa miti watu na magenge ambayo niliyaona kupitia dirishani na hicho ndo kilikuwa kitu kilichonifanya nikae karibu na dirisha wakati wote wa safari.

Baada ya takribani masaa mawili ya kushangaa dirishani, tulifika stendi ya tegeta nyuki, na bila ya kupoteza muda tuliteremka na kwenda kupanda gari la kuelekea Mawasiliano ili kupata magari ya kwenda gongo la mboto.Ulikuwa ni mwendo wa saa moja mpaka kufika kwenye stendi kuu ya mabasi ya Mawasiliano, na kama kawaida nilikuwa upande wa dirishani wakati wote huo.

Siku zote magari ya gongo la mboto huwa ni shida kuyapata wa jioni lakini muda tulio wasili ulikuwa ni mzuri na magari ya gongo la mboto yalikuwa yapo ya kumwaga. Hatukuwa na mengi ya kufanya hivyo moja kwa moja tulipanda kwenye gari la kuelekea kwa shangazi ambaye bila shaka alikuwa anatusubiria tupige simu ili kumjulisha kama tumefika.

Mara hii baada ya kupanda mama ndiye aliye nipakata upande wa dirishani huku baba akiwa amekaa pembeni yetu. Gari lilianza kuondoka mdogo mdogo huku konda akiitia “ haya Tabata buguruni sheli Gongo la mboto hiyo” alindelea kuitia watu ili wapande lakini hapakuwa na dalili ya mtu yoyote kuja , alipoona hakuna na mtu alifunga mlango , gari liliongeza kasi na safari yenye kuchosha kwa foleni ilianza.

Safari ilindelea bila kusimama mpaka tulipofika kwenye daraja la juu la Kijazi . Tulisimama kwenye mataa chini ya barabara zilizokatisha juu kwa juu zilizoitwa flai ova.Mpaka wakati huu konda aliyekuwa anadai nauli alifika kwenye siti amabayo tulikaa sisi “Kata wawili” Baba alisema alipompatia konda noti ya shilingi elfu kumi “hauna hela ndogo” aliuliza konda “Hapana sina” alijibu baba . Niligeuka na kumwaangalia konda ambaye alikuwa akihesabu pesa ili amrudishie

baba chenji , niliduwaa kidogo na kugeuka tena dirishani baada ya kuhisi gari letu limeanza kutembea ila sikuona chochote Zaidi ya lori lililokuwa kasi likija kwenye gari tulilopanda, Mama alipiga kelele kali ambayo ilinishtua mimi na kila mtu na sikuweza kutafakari hata kidogo kilichokuwa kina endelea ,hapo hapo lile lori liligonga gari letu kwa nguvu sana na kusababisha gari letu kupinduka na kuburuzika barabarani.

Ilikuwa ni ghafla na haraka sana , sikuweza kuuhisi hata mwili wangu na kwa mbaali nilikuwa nikisikia sauti za watu wakilia na kupiga kelele. Bila kujua na mimi nilianza kulia kutokana na mshtuko ambao ulinifanya nisiwze kufikiria chochote.

Ghafla nilihisi kama nimshikwa na mikono mikubwa na migumu iliyonivuta na kunitoa nje ya gari kupitia dirishani, sikuweza kumtambua aliyenibeba kwani nilikuwa nimeduwaa na kulia bila kujua sababu.

Yule mtu alinibeba na kuniweka chini pembeni kidogo ya barabara alafu haraka aliondoka bila shaka kwenda kuokoa wengine.Bila kujielewa niliinuka huku nikilia na kuanza kuondoka kuelekea chini ya moja ya barabara za juu ambayo kwa mbali mbele yake ninliona kama mto.

Sikujua ninaoenda ila niliendela kwenda tu, lakini ghafla nguvu ziliniishia na nilidondoka chini na kuangukia kisogo na kuzimia. Sikujua nilizimia kwa muda gani ila ni Dhahiri ulipita usiku mmoja nikiwa pale kwani palionekana papo kawaida huku magari na watu ya kipishana kama ilivyo siku zote.Sikuweza kukumbuka chochote kuhusu mimi wala kilichotokea Zaidi ya vilio vya watu na mikono iliyonitoa ndani ya lile gari.

Kichwa kiliniuma sana kwani nilijilazimisha kukumbuka vitu ambavyo havikuwepo tena kichwani kwangu.Tumbo lilipounguruma kwa njaa ndipo nilishtuka toka kwenye mawazo yasiyokuwa na muelekeo wowotw wa kupata ufumbuzi.Nilipoangaza pembeni nilimwona mtoto aliye rika sawa na mimi akiwa anakula mkate na juisi, hakuna wazo lolote lililokuja kichwani kwangu Zaidi ya kwenda na kumuomba yule mtoto. “Naomba kidogo nina njaa” nilisema kwa sauti ya chini na upole mkubwa “ Kaombe yako, we vipi” aliniambia kwa sauti yenye kiburi, “Nikaombe yangu, nimwombe nani” nilijiuliza mwenyewe kichwani huku nikiangaza huku na kule.

Nilipotazama barabarani niliwaona watoto wengine kadhaa wakiomba kwenye magari yaliyokuwa yamesimama kwenye mataa . Sikujiuliza Zaidi niliinuka na kwenda moja kwa moja kwenye dirisha la nyuma la gari moja aina ya noah na kuanza kuomba “Niasidie nina njaa” nilisema kwa upole “Neema funga kioo wezi hao, yani ni washenzi sana hao” alisema kwa ukali yul dereva wa lile gari na kile kioo kilifungwa na sikuweza kumwona yoyote wa kwenye lile gari. Nilitoka evpembeni ya barabara haraka kwani mataa yalisharuhusu magari kutembea .

Nilijikokota huku nikiburuza kiganja changu kwenye mlingoti mpana wa moja ya barabara za juu zilizoko pale. Ghafla wakati natokeza mwishoni mwa ule mlingoti mtoto mwenye rika sawa na mimi ambaye alikuwa anakimbia kwa kasi alinigonga na kuniangusha chini, Kabla hata sijainuka watu wengine wawili wakubwa walitokea huku wakiita “mwizi …..mwizi” na bila ya kuuliza mtu mmoja kati ya wale alinipiga na tofali kubwa usoni , sikuweza hata kufumba macho tofali jengine lilitua tumboni kwa nguvu sana .

Mwili wangu ulikuwa wa baridi, huku moyo wangu ukidunda taratibu . sikuwaza chochote zaidi ya kufa nikijiuliza kwa nini wananipiga ? Mimi ni nani?
 
Mwili wangu ulikuwa wa baridi, huku moyo wangu ukidunda taratibu . sikuwaza chochote zaidi ya kufa nikijiuliza kwa nini wananipiga ? Mimi ni nani?🥱
20221203_123810.jpg
 
Mbona sijaielewa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom