Mimi ni mvivu kweli, naombeni ushauri

Mimi ni mvivu kweli, naombeni ushauri

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
28,029
Reaction score
52,507
Wadau nina shida moja katika maisha yangu. Mimi ni mvivu halafu huwa natake easy kila kitu, kitu ambacho kinanisababishia hasara nyingi maishani.

Kuhusu darasani nina akili za kutosha toka primary top ten ilikuwa hainikosi hata chuo sikuwahi kupata supp, hata kuna wakati somo moja lililamba robo tatu ya darasa, tena nilikuwa nimelazwa, nikatoka hospitali asubuhi nikaingia saa tisa kwenye paper nikapata zangu B. Niliosoma nao humu wanaweza kunikumbuka.

Sasa tatizo linakuja kwenye maisha, mimi ni mvivu. Kuamka nitashtuka tu saa kumi na moja najiongeza kidogo kidogo hadi inafika saa moja najiandaa kivivuvivu hivo hivo. Mara nivae nguo hii mara nione sijapendeza nivue hadi saa mbili natoka nduki kwenda job maana sio mbali, kwahiyo hapo naacha chumba kikiwa rafu maana muda wa kupanga na kutandika kitanda unakuwa hamna hadi nirudi jioni.

Nikialikwa kwenye party najiandaa kivivu hadi wakati mwingine naacha tu maana muda unakuwa hamna tena sherehe imeisha.

Nikienda benk sihesabu hela, jana nimeibiwa elf 10 duka la kubadilishia fedha maana sikuhesabu, kwenye daladala nilipewa hela feki hivi hivi maana hata sikuangalia.

Naombeni ushauri nifanyeje maana mimi mtu mzima nahitaji kuwa na familia na kuwa mama bora. Ndio maana nilitamani kuadopt mtoto ili niwe busy nae, haya maisha ya kuishi peke yangu yananilemaza jamani nifanyeje?

Natamani kuwa active. Hapa nimeandika hivi nimechoka kweli yaani.
 
Miss Natafuta..
Kumbe ndio maana unaishi kutafuta na haupati...!
Kipe kila kitu unachokifanya uzito then do one thing at a time
 
Pole sana single lady wengi ni wa aina yako
uzuri umejitambua na ukishajua ugonjwa ni rahisi kuutibu......

Nilishawahi kuwa na rafiki yangu kiukweli wka malezi yangu na yeye nilikuwa namshangaa sana maana ule haukuwa uchagu was too much..... choo kinakuwa cheusi tandu za buibui mpka mlangoni vumbi ndio kabisaaa unaabakisha nyayo.

Menigne ni aibu kwa kweli. Na bado anakuambia nataka kuolewa apaa
 
Tungeoana nyumba ingekua majanga, Mara nyingi hata safari naweza kuachwa au naingia last minutes. I am struggling niwe punctual na proactive, kwa sasa full reactive.
 
Back
Top Bottom