Mimi ni muathirika wa UKIMWI

Yawezekana na yeye alikuwa hajui kama anao pole sana Mkuu nikajua huku mbagala peke yake ndiyo wanyonge wanapata ukimwi kumbe hata huko Holm

Daah kweli Dunia ni Familia na sio kijiji tena
Zabron alijijua na ndiyo maana hakutaka kupima
 
Duuh, pole sana!
 
Aisee pole sana. ....mojawapo ya matokea ya ku jiweka wazi ndio kama hizo rejections.

Usikate tamaa muda bad unao na utabarikiwa mtu muelewa na mtakuwa na familia yenu.

Jitahidi kumsamehe na ujisamehe wewe pia, kwa maana ni jukumu lako kujilinda afya yako kwanza.

Ni muda sasa tujifunze kuacha kuwa nyanyapa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi na kuwaona kama wamemkosea Mungu au walikuwa na maienendo michafu kufika maambukizi.

Kila la kheri Protein
 
[emoji23][emoji23][emoji23]uliruka ruka sana ujanani ee
 

Ila alifanya maamuzi mazuri kujiweka wazi. Ni vizuri kujilinda na kumlinda unayempenda.

Rejection kitu gani bwana. Protein ulifanya maamuzi ya busara.

Naamini siku tukiacha kuwanyanyapaa waathirika nao hawatashindwa kujisema wana HIV. Kikubwa wanachohofia ni athari watakazokutana nazo wakishajiweka wazi.

Nilishawahi kwenda kusini mwa Afrika...nadhani ni jamii nzuri kuiiga kwenye suala la Ukimwi. Ukimtongoza mtu haoni shida kukuambia mimi nina Ukimwi na aliyeambiwa hata hastuki.

Huhitaji kusononeka na kuona umepoteza. Weka mind yako free utapata mwenza.

Sikutaka ku-comment kwenye huu uzi umejaa comments za kitoto.
 

Mimi pia nimeshangaa Mkuu kusema kujiweka wazi ni jambo baya, kutuwekea utu uzima siyo mbaya Mkuu kama ulivyofanya
 
Hata hospitali tumeambiwa ukiwa undecteble huna haja ya kumwambia date kuwa una HIV, lakini ki sheria mwanaume anaekuoa lazima umueleze.

So unaweza kudate ikawa siri yako as long as humuambukizi date.
 
Pole sana mkuu..tumia dawa kama ulivyoelekezwa na doctor wako,jipende,relax,na jenga familia yako..usikate tamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…