Najuta kumkopesha huyu mwanamke, kweli anataka kunitapeli hela yangu

jjs2017

JF-Expert Member
May 25, 2019
2,023
4,213
Huyu mwanamke alikua na shida sana na hakukua na mtu wa kumsaidia kiwango cha hela alichokua anaomba, alijaribu kukopa kwa kila mtu ila hakuna aliye mpa na mwishowe nikaona acha ni mkopeshe maana kidogo uwezo ulikuwepo, nilimkopesha takribani shilingi laki tano taslimu (500k) na yote haya ni sababu tuu ya huruma zangu na vile alivyokuwa anaomba kwa huzuni kuu na unyeyekevu.

Niliweka nae makubaliano ya kurudisha hela yangu niliyo mkopesha kiroho safi ila tokea muda wa kurudisha umefika ananichekea chekea tuu na kunirembulia macho kwa namna ya kutaka kunipa kitu cha tofauti alicho nacho ila na puuzia nataka hela yangu mimi, kwa kweli nimejaribu sana kumuhimiza anipe hela yangu ila naona haelewi somo yeye ni kunichekea chekea hovyo.

Mpaka na kuja hapa nimeshaongea naye kimafumbo sana kwa kutoa mifano ya wengine ila hata ashituki yupo yupo tu na sasa ni miezi imepita ya kutosha tokea nimkopeshe hela yangu na sijui nitumie mbinu gani maana hata sikuandikishana nae popote, nilimwamini nikamkopesha tena bila hata riba.

Yalaiti ningekua nimeandikishana nae ningemburuza kotini ila ndiyo hivyo naona hapa ni kama silipwi kimasihara hivi hivi.

Nimekoma kweli kumkopesha mwanamke hela na kumuonea huruma. Kweli sirudii tena.

Moyo unauma sana hela yangu inapotea kimasihara sana.

Nifanyaje ndugu zangu nipate hii hela.
 
Back
Top Bottom