Mimi na Mgahawa wa Chef Pride

Mimi na Mgahawa wa Chef Pride

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
MIMI NA CHEF PRIDE

Historia yetu sasa nadhani ina kiasi cha miaka 30 na zaidi.
Mgahawa ulikuwa Mosque Street, Zahir Hotel.

Katika miaka ya 1980/90 ndipo kilipokuwa kijiwe chetu cha mazungumzo, kula na kunywa.
Mwendeshaji wa mgahawa kijana mwenzetu Salim Mahsen.

Vyama vingi vilipoanza 1992 mgahawa ukawa uwanja wa siasa wanachama na wapenzi wa vyama vyote huwapungui hapo.

Mijadala moto moto ikiunguruma.
Unachagua mwenyewe ukae meza ipi.

NCCR Mageuzi na Augustino Mrema ilikuwa imepamba moto, NRA kisha CUF ya Maalim Seif na Kaka Mkubwa CCM.

Salim anatununulia magazeti yote wa nyakati zile anatuwekea mezani - Shaba, Rai, Bahari, Uhuru na haya magazeti yalikuwa yana mkondo wake katika siasa changa za vyama vingi.

Ukifika Zahir asubuhi kunywa chai unapata taarifa zote katika ulimwengu wa siasa za Tanzania.
Salim akiijua saikolojia ya sisi wateja wake.

Wakati mwingine akitutania anasema, "Nimekuwekeeni hizi meza ziwe mbali ili msiibiane sera."
Siku alipotuambia kuwa anairudisha hoteli kwa mwenyewe ilikuwa msiba.

Wateja wote tulitawanyika.
Hatukuwa na mahali pa kukutana.

Mgahawa ulikuwapo lakini haikuwa kama alipokuwa Salim.
Uwanja hakika ulikuwapo lakini magoli yameng'olewa.

Salim akafungua Chef Pride, Chagga Street.
Haba jana.

Tukapata uhai mpya.
Kisha akafungua Chef Pride nyingine Lumumba Avenue karibu na CCM.

Chef Pride hakika leo ni sehemu ya historia ya Dar-es-Salaam.
Hapati mtu mgeni sharti atampeleka Chef.

Chai ya asubuhi haipiti ila inywewe Chef.
Halikadhalika chakula cha mchana na usiku ukiwa na mgeni.

Nimeweka hapo chini picha ya Salim na Dr. Harith Ghassany nilipomfikisha Chef miaka michache ya nyuma nikamjulisha kwa Salim.

Chef ni mahali utamuona kila mtu.
Ni suala la subra na muda.

1746021397365.jpeg

Kulia Dr. Harith Ghassany na Salim Mahsen
1746021507322.jpeg
 
Tuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.

Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.

Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
 
Asante sana kwa historia hii mzee wetu. Hakika wewe ni tunu kwa wanachama wa JF.

Anyway mzee wangu mimi na vijana wenzangu tusio na ajira tu kikundi chetu kinaitwa "The expert group" tunajishugjulisha na kazi za site survey, kubandika tiles na paving blocks pamoja na kupaka rangi.
 
Sh Mohamed
Leo tena umenikumbusha miaka mingi iliyopita, Zahir ninaikumbuka lakini haikuwa katika sehemu za matembezi yangu
Nategemea sana utaikumbuka Ala-kefak (sijui kama jina nimeliandika sawasawa) iliyokuwa Kariakoo, wakati wa jioni tukienda kula bokoboko
Ahsante sana
 
Nakumbuka wakati nasoma, ilikuwa nikidunduliza visenti, nilikuwa naenda Zahir hotel kununua Cheese roll au Meat roll
Mara ya mwisho nimekula Zahir ilikuwa 2004, Wali Samaki, sijui kama bado ilikuwa na huyohuyo mmiliki.

Na Miaka miwili iliyopita, nilipokuwa Dar, nilikuwa napita Chefs pride kila bada ya siku mbili tatu napita kupiga ama biriani au chai ya jioni kwa sambusa na kababu......
 
Tuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.

Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.

Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
Kiukweli hii bomoa bomoa imekuwa tatizo kubwa. Miaka kadhaa ijayo hakutakuwepo na kumbukumbu yoyote ya Dsm.
 
MIMI NA CHEF PRIDE

Historia yetu sasa nadhani ina kiasi cha miaka 30 na zaidi.
Mgahawa ulikuwa Mosque Street, Zahir Hotel.

Katika miaka ya 1980/90 ndipo kilipokuwa kijiwe chetu cha mazungumzo, kula na kunywa.
Mwendeshaji wa mgahawa kijana mwenzetu Salim Mahsen.

Vyama vingi vilipoanza 1992 mgahawa ukawa uwanja wa siasa wanachama na wapenzi wa vyama vyote huwapungui hapo.

Mijadala moto moto ikiunguruma.
Unachagua mwenyewe ukae meza ipi.

NCCR Mageuzi na Augustino Mrema ilikuwa imepamba moto, NRA kisha CUF ya Maalim Seif na Kaka Mkubwa CCM.

Salim anatununulia magazeti yote wa nyakati zile anatuwekea mezani - Shaba, Rai, Bahari, Uhuru na haya magazeti yalikuwa yana mkondo wake katika siasa changa za vyama vingi.

Ukifika Zahir asubuhi kunywa chai unapata taarifa zote katika ulimwengu wa siasa za Tanzania.
Salim akiijua saikolojia ya sisi wateja wake.

Wakati mwingine akitutania anasema, "Nimekuwekeeni hizi meza ziwe mbali ili msiibiane sera."
Siku alipotuambia kuwa anairudisha hoteli kwa mwenyewe ilikuwa msiba.

Wateja wote tulitawanyika.
Hatukuwa na mahali pa kukutana.

Mgahawa ulikuwapo lakini haikuwa kama alipokuwa Salim.
Uwanja hakika ulikuwapo lakini magoli yameng'olewa.

Salim akafungua Chef Pride, Chagga Street.
Haba jana.

Tukapata uhai mpya.
Kisha akafungua Chef Pride nyingine Lumumba Avenue karibu na CCM.

Chef Pride hakika leo ni sehemu ya historia ya Dar-es-Salaam.
Hapati mtu mgeni sharti atampeleka Chef.

Chai ya asubuhi haipiti ila inywewe Chef.
Halikadhalika chakula cha mchana na usiku ukiwa na mgeni.

Nimeweka hapo chini picha ya Salim na Dr. Harith Ghassany nilipomfikisha Chef miaka michache ya nyuma nikamjulisha kwa Salim.

Chef ni mahali utamuona kila mtu.
Ni suala la subra na muda.

View attachment 3320767
Kulia Dr. Harith Ghassany na Salim Mahsen
View attachment 3320770
Oh nami umenikumbusha,mimi sheikh said nilikujulia hapo salamander kwa akina hashim sagaf,nilikuwa nakuja hapo na kaka yangu wakati huo nikisoma nje ya nchi,nikawa a bit rafiki kwako kutokana na uwezo wako wako wa kuchambua mambo,pia nikamfahamu jamaa mmoja akiitwa tamim,na kijana mmoja kama msomali hivi akiitwa mohamed akiaandikia magazeti.Kaka yangu akanipeleka hapo chef pride chagga street,aisee kulikuwa na kila aina ya chakula na ndipo nikakutana na watu wengi sana maarufu,na kabla sijasahau pale salamander nilikutana na jakaya na tukawa marafiki sana nadhani wakati huo alikuwa waziri wa madini.

Hapo chef pride nje kulikuwa na shoeshiner wengi na vijana wa kutafuta parking za magari.

Baadae nikamfahamu huyo mmiliki wa chef pride.

Sasa hapo pembeni ya chef pride kulikuwa na tea room mmoja maarufu sana,ambayo ilikuwa maarufu kwa aina fulani ya chai kwenye tu vikombe tudogo na kababu za kunde,aiseeee ile chai haina mfano,watu walikuwa wanagombania nafasi na mara kwa mara nilikuwa nakuta foleni nje.Pia walikuwa na mzee mmoja weita mmoja ambae alikuwa ana kichwa cha kompyuta,bili za watu alikuwa anakariri tu na akiulizwa anatoa hesabu kamili.Miaka ya zamani klabu ya yanga ilikuwa na seneti yake ikiongozwa na mohamed virani,nao walikuwa wakija wote hapo yea room kunywa chai.

Nami hapo nilipata dada mmoja wa kihindi nikazaa nae.Basi sheikh said asante sana kwa uzi wako
 
Tuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.

Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.

Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
Carl Lewis alikuwa mwamba alitingisha sana enzi zake
Aise umenikumbusha mbali sana

Ova
 
Tuwekee historia mkubwa hata picha kama unazo, maana hizi sehemu hawakawii kuzivunja na kujenga parking lot.

Kuna ule mgahawa maarufu wa Salamander hapo Samora Avenue tulikuwa tunakwenda vijana wa mjini kupanga mitkas na jamaa mmoja sasa sijui yuko wapi, tulikuwa tunamuita "Carl Lewis". Mtoto aliyekulia Dar miaka ya mwanzo ya tisini mjanja mjanja wa mjini hapo lazima atakuwa anamjua Carl Lewis ni nani.

Mgahawa una historia ndefu tangu enzi za kupigania uhuru, nasikia wameuondoa na kuweka nini hapo sijui.
Salamander nayo ilishapotea

Ova
 
Kule Arusha meeting point ya waalimu wakipokea mishahara ni Jogoo house karibu na stendi kuu. Waalimu wakuu na watendaji wa kata hukutana Stanley bar. Wanakuwa na mihuri kabisa... kama kuna ishu anakugongea muhuri chap.
Hahah

Ova
 
Back
Top Bottom