KITALIKA Titho E
Member
- Jun 25, 2019
- 14
- 20
KUSUDIO LA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA NAFASI YA KATIBU MKUU BARAZA LA VIJANA WA CHADEMA (BAVICHA).
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Katibu mkuu kimetoa tangazo la uchaguzi wa Chama ngazi ya Taifa utakayoanza tarehe 09 Desemba na kuhitimishwa tarehe 19 mwezi huo huo kwa uchaguzi wa Katibu Mkuu wa Chama na manaibu katibu wawili. Uchaguzi wa taifa utahusisha pia mabaraza ya Chama.
Mimi CPA KITALIKA, TITHO.E nimekusudia kugombea nafasi ya Ukatibu mkuu wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA). Nimejipima mimi mwenyewe pamoja na kupata ushauri kutoka kwa watu wangu wa karibu wanaofahamu uwezo wangu wa kiuongozi na dhamira yangu ya kukitumikia chama na kujiridhisha kwamba nafasi hii ndiyo sahihi Zaidi kwangu.
Nafahamu yapo mafanikio yaliyofikiwa na viongozi walioshika nafasi ndani ya baraza lakini vile vile kuna mambo yanatakiwa kufanyika. Nikifanikiwa kuteuliwa kuwa mgombea nitaeleza dhamira na maono yangu kama nitachaguliwa kuwa katibu mkuu wa BAVICHA.
KAZI NA NAFASI ZA UONGOZI NDANI YA CHAMA
- 2011: Wakati nikiwa mwanafunzi wa A’level wakati wa likizo nilishirikiana na viongozi wa Chama wilaya ya Mufindi Kueneza chama katika majimbo ya Mufindi Kusini na Kaskazini.
- 2012: Niliteuliwa kuwa mwenyekiti wa CHADEMA NI MSINGI kata ya Mtwango katika jimbo la Mufindi Kusini na nimeshiriki kuaanzisha matawi imara na tegemeo kwa chama katika jimbo la Mufindi Kusini mfano Nyololo na Ihowanza.
- 2013: Nimeshiriki katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Themi Jimbo la Arusha Mjini, nilichaguliwa kuwa mwenyekiti wa CHASO tawi la Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), nilishiriki kuanzisha CHASO MKOA WA ARUSHA na kuchaguliwa kuwa mratibu wa kwanza wa CHASO Mkoa wa Arusha.
- 2014: Nimeshiriki kutafuta wanachama na kuwapa kadi katika jimbo la Longido Mkoa wa Arusha, nimeshiriki kampeni za uchaguzi serikali za mitaa katika Jimbo la Nyang’wale, Arumeru Magharibi na Arusha Mjini na nilichaguliwa kuwa mratibu wa CHASO Mkoa wa Arusha kwa mara nyingine.
- 2015: Nilishiriki kampeni za ubunge katika jimbo la Mafinga Mjini kama mjumbe wa kamati ya kampeni na kuzunguka na mgombea ubunge na madiwani katika kata zote sita za jimbo. Na mara kadhaa katika jimbo la Mufindi Kaskazini.
- 2016/2019: Nimeshiriki katika uchaguzi mdogo katika kata ya Saranga jimbo la Kibamba, uchaguzi wa marudio wa jimbo la Kinondoni katika kampeni za nyumba kwa nyumba katika kata ya Hananasifu, magomeni na Ndugumbi
- 2019: Nimeshiriki katika kuwezesha viongozi wa chama kata ya Mtwango Jimbo la Mufindi kusini wanapata wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa na vijiji.
- 2019: Mjumbe wa Kamati Tendaji Jimbo la Mufindi Kusini na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa (Wilaya ya Mufindi)
2013/2015 MRATIBU CHASO ARUSHA.
- Pamoja na viongozi wenzangu tulisaidia kuongea matawi ya CHASO kutoka manne mpaka kumi
- Kuongeza ushiriki wa wanaCHASO katika kujenga chama matharani wanaCHASO kushiriki katika chaguzi ndogo za udiwani katika mikoa ya Tanga, Arusha na Manyara.
- Kuanzisha kanuni za CHASO MKOA zilizozinduliwa na mh.Tundu lissu tofauti na mikoa mingine ambayo hutegemea nyaraka na miongozo kutoka kwa katibu Mkuu BAVICHA.
- Kuwezesha wanaCHASO kushinda nafasi za uongozi katika serikali za wanafunzi katika vyuo mf. IAA, MMU, St Joseph (Kisongo) na Jomo Kenyatta.
- Kuandaa mapendekezo ya KANUNI ZA KUONGOZA CHASO na kuziwasilisha kwa mjumbe wa kamati kuu Prof.Mwesige Baregu.
UONGOZI NJE YA CHAMA
2008/2009- Amekuwa kiongozi katika serikali ya wanafunzi shule ya sekondari Mdabulo
2010/2011- Amekuwa kiongozi wa Afya na Mazingira shule ya sekondari Azani.
2012/2013- Amekuwa mwakilishi wa Taaluma wa Darasa (Uchumi na Fedha) katika Kamati ya Taaluma ya Serikali ya wanafunzi.
2019- -Mjumbe wa Board na mshauri wa kifedha wa NGO iitwayo Every Child Tanzania (ECT)
ELIMU YA MGOMBEA
2018/2019: MBA Corporate Management (IP)-Mzumbe University
2016/2018: Certified Public Accountant (CPA)-National Board of Accountants and Auditors.
2012/2015: Bachelor of Economics and Finance-Institute of Accountancy Arusha
2006/2012: O’level & A ‘level- Mdabulo Secondary School/Azania High School