GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,695
- 6,398
"Whatever you praise, you increase!"
Hiyo kauli ni miongoni mwa nukuu zilizopo kwenye kitabu cha M. R. Kopmeyer.
Kopmeyer, ambaye hujiita pia America's Success Counselor, anaongeza kuwa katika tafiti zilizofanyika, wanawake waliokuwa na tabia ya kusfia maua yao, walikiri kuwa mimea yao ilistawi vizuri sana tofauti na wale ambao hawakuwa wakifanya hivyo.
Mtu mwingine akasema aliotesha miche miwili ya miti, ambapo mti mmoja alikuwa akiulaani kila siku huku mwingine akiubariki. Pamoja na kumwagilizia na kuiwekea mbolea kwa kiwango sawa, ule aliokuwa akiulaani ulikauka baada ya miezi kadhaa huku uliokuwa ukibarikiwa ukiendelea kustawi zaidi.
Katika tukio jingine, mhubiri mmoja alisema kuwa wanasayansi wamegundua kuwa kunapotokea moto msituni, miti mikubwa hutoa maji ya kuihami miti midogo isiungue. Kwa tafsiri ya huyo mhubiri, miti mikubwa inapopata taarifa ya uvamizi wa moto, huitaarifu miti iliyo karibia na "watoto" kuwa kuna hatari hivyo waitengenezee miti midogo mazingira ya usalama. Kwa hiyo, hutoa maji yatakayoisaidia miti midogo isiangamie.
Kuna ukweli katika hiyo mitazamo? Wanasayansi wanasemaje kuhusu mimea?
Inaweza kuwasiliana?
Inaweza kusikia?
Mimea ina masikio?