Mimba. . . . | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba. . . .

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Mar 28, 2012.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  "Hivi mwanaume kakataa mimba we umelea ya nini? Haki ya nani mi mwanaume hajaniachia mimba nikalea, labda aniachie mtoto hapo angalau!"

  Hayo ni maneno ya dada mmoja kwenda kwa mwingine ambae ni mama mtarajiwa. Alikua anamwambia kauli yake ikisuggest kwamba mwanaume anapokimbia/kataa mimba basi kiumbe cha watu kinakosa haki ya kuishi hivyo kitolewe. Hii kitu imenifanya nijiulize. . .

  1.Hivi mimba ni ya nani? Ya mwanaume hivyo asipokua tayari kushiriki katika malezi yake basi iondolewe na kutupiliwa mbali?
  2.Mimba ni ugonjwa usiozuilika hata watu wasijali wakati wa kupata ila wawe tayari kutumia gharama kuziondoa?
  3.Baadhi ya wanawake wa akili za aina gani hata wajiweke katika position za kupata mimba na mwanaume asiyeeleweka huku wakijua fika 'BILA KUWEZESHWA HAWAWEZI'??"

  Nasikitika kuona kwamba wanawake wengine wana fikra zilizokaa kinyume nyume na bila huruma wako tayari kuadhibu viumbe ambavyo havikishiriki kwenye mambo na starehe zao binafsi.
   
 2. j

  joeprince Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wakati akimpa bila kinga alitegemea utamu tuuuu au hajui kuna mimba pia?
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Suali ambalo wengi watakuuliza ni kiumbe tumboni huhesabika kuwa kiumbe kuanzia lini?
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Ngoja tuwasikie kina dada ila sioni haki ya mtu kuamua kupata mimba halafu anakimbilia kutoa. Maana kama unavyosema, mimba sio ugonjwa unaokuja bila taarifa...people work hard for it!!! Kuitoa kwangu mimi ni tatizo...it is a sin and crime!
   
 5. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wakati ana miezi miwili, lakini ukienda deep sana mimba ikisha ingia tu huna haki ya kuitoa.
   
 6. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145

  Nashukuru kwa kuileta mada hii jukwaani. Please see my response below:
  1. Mimba ni ya wote, aliyepewa na aliyetoa
  2. Siku zote huwa naamini kwamba kupata mimba kwa mwanamke wakati haihitaji siyo bahati mbaya, ni uzembe wa wazi. Kuna njia nyingi sana za kuzuia mimba zikiwemo sindano, vipandikizi, cndms nk. Na pia kwa mtu aliyefanya mambo akahisi ilikuwa siku mbaya kuna vidonge vya kutumia baada ya tukio kutendeka. Sasa upatikanaji wa mimba bahati mbaya unakujaje?
  3. Saa nyingine ni ufinyu wa mawazo na wakati mwingine huziruhusu hizo mimba kuingia kwa makusudi kuforce hao maboyfriend wao kufunga nao ndoa. Na kama ukimkuta mwanaume hayuko tayari, basi mimba huishia kukataliwa na kutolewa.

  Niungane na wewe kuwa tabia hii ya kutoa mimba ni mbaya na haipendezi machoni kwa Mungu na wanadamu pia!
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mimba ni ya wote wawili( mwanamke na mwanaume) manake lazima mshirikiane kufanya itokee, mimba sio ugonjwa, inawezekana kuiepuka. Mie ndio mana huwa siamini mtu akisema amepata mimba kwa bahati mbaya. Siamini kama kuna mimba ya bahati mbaya labda kwa mtu 'aliyebakwa' tu.

  Huyo dada angejua kulea mimba sio kazi, kazi ni kulea mtoto wala asingeropoka hayo maneno yake, ila ndio hivyo huezi kujua uhondo wa ngoma kama hujaingia kucheza.
   
 8. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Huna haki kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Lakini Tanzania hakuna sheria ya nchi inayozingatiwa
   
 9. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Kulizungumzia suala ya kutoa mimba kunahitaji tafakuri ya kina na wakati mwingine kuvaa viatu vya wahusika wa suala hilo.

  Hebu fikiria binti ni tegemezi kwa asilimia 100 na familia yake ipo ktk kundi la mafukara, binti amegeuzwa kuwa kiburudisho/mfariji wa ngono na mchovu mwenzake, inatokea mimba anaikana kwa sababu hana uwezo/hataki majukumu Huyo binti afanyeje? hapa ni bora aitoe ili aendelee na maisha yake.

  Pia kwa sehemu kubwa mahusiano ya cku hizi ni ya kuburudishana zaidi ya kujenga familia, vijana(me) wengi bado wapo wapo sana kuhusu suala la kuanza kununua pampas,n.k, na wengine hawataki kabisa kuzaa na watu ambao hawatakuja kuishi nao kwa hiyo mimba ikizalishwa aidha binti akubali itolewe au iwe yake, sasa ni juu ya binti ana uwezo wa kuitunza, familia je-itamuunga mkono au ndo mwanzo wa mateso?
   
 10. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Anaye tunga sheria Tanzania nani?
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,872
  Likes Received: 6,222
  Trophy Points: 280

  kuhusu swali namba 3:

  cha ajabu wanawake miili ni yenu, mimba mnabeba nyinyi lakini hamna uamuzi wa mwisho.... mnamwachia mwanaume aamue kutumia condom au la...matokeo yake mimba, na mwanaume suruali ataishia kukana mimba....kuzuia ukatili maisha ya kiumbe kisicho na hatia ipo mikononi mwa wanawake, na wanaume muache ulaghai, kama huna mpango wa muda mrefu/wa kudumu na mwanamke wa watu hebu cheza kwa step.......


   
 12. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  Hili la mimba nadhani kila mmoja na uelewa wake.

  1. Kuna wanaoamini, haki ya mimba/mtoto huanza baada ya kuzaliwa mtoto, akiwa tumboni hana maisha hata kama ni miezi 7, ndo maana unakuta mtu anatoa mimba ya miezi 7
  2. Kuna wanaoamini hak ya mimba/mtoto kuishi ni pale anapoanza kuwa kiumbe kinachoeleweka akiwa tumboni, kwa hiyo mimba ikiwa chini ya miezi anaona ana haki ya kutoa.

  3. kuna wanaoamini haki ya mimba/mtoto kuishi huanza tu baada ya mimba kutungwa.

  Sidhani kama hii kitu iko moja kwa moja maana kile unachoamini ndio kinakufanya uwe na uchungu wa kutoa mimba au la!

  Kuna baadhi ya watu wameenda mbali zaidi na kusema hata matumizi ya kondomu ni haramu maana yanazuia utungwaji wa mimba.

  Mie huwa nauhusishwa utoaji wa mimba na consious ya mtu.

  Ila kwa nchi kama Tanzania ambapo utoaji wa mimba hauruhusiwi kisheria hadi kwa maelezo ya kitatibu yalothibitishwa, inazidi kuleta mkanganyiko zaidi.

  Ni kujaribu kurithisha unachokiamini kwa kizazi chako, wao wakikua na wao watachagua la kuamini.
   
 13. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,269
  Trophy Points: 280
  Huwa sielewi nikisikia Mwanamke anapata mimba bila kupanga kumbe nilikuwa najidanganya......kuna kisaloon umbeya jiran yangu ndio huwa nanunuwa vocha, basi nilikuta topic kama hii na niliwasema wale wanawake LIVE ni kwa nini mnapata mimba bila kupanga?

  Maskini ya mungu kumbe hawa kina dada/mama walioishia darasa la saba au kukosa elimu ya uzazi wapo wengi kuliko tunavyofikiri tena waliniomba niwapen elimu kwamba nje ya condom na vidonge wanawezaje kuzuiya mimba zisizotarajiwa? imagine hawa wote ni wake za watu kumbe wanazaa hovyo kwa kuto hata kujuwa siku salama kwao ku do unprotected!!
  Ninavyofahamu mimi mwanamke yeyote anayejitambuwa hawezi kupata mimba kama hajamuuwa kuzaa hata mwanaume uweje.
   
 14. WaliNazi

  WaliNazi JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 853
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  ...Unwanted pregnance free generation is possible.... It begins with WOMAN....
   
 15. KIKUNGU

  KIKUNGU JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mmh Lizzy,nitarudi kuchangia hii kitu.Am busy right now.
   
 16. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #16
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nadhani msingi wa tatizo umesha upigilia mstari:
  wanawake wengi wanafikiria hawato weza.
  Bila mwanaume wa kumgharamia mtoto, yeye hawezi.
  Mi niko pro-choice, ila isiwe just sababu mwanaume kakataa.
   
 17. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #17
  Mar 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,069
  Likes Received: 6,529
  Trophy Points: 280
  Nawe wasemaje mrembo.
   
 18. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #18
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kama mwanaume amekataa na umepima mwenyewe umeona huwezi then toa,single parenting is not an easy ride.......
   
 19. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #19
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  tupi kibao lol,ambao hatujui siku zetu zinakwendaje...na kwa wengine nadhani mzunguko unabadilika hivyo inakuwa ngumu kupinpoint siku za kushika mimba,
   
 20. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hapo wanchekesha
   
Loading...