Mimba ya mke wangu inanitesa

Nikawaida mbona. Ni hormones tu hizo. Akishajifungua atarudi kawaida. Kila mimba inakuja tofauti. Vumilia tu, your almost there
 
Ndo raha ya mtoto hiyo asikudanganye mtu ukikumbuka karaha zote hizo ndo unajua thamani ya mtoto atakayezaliwa yaani mimi nikiwaangalia wanangu huwa nafurahiiiiiiiiiiiiii. Nawe vuta subira tu utafurahia sana.

Ila daaa umenizidi kusumbuka, mimi wala sikusumbuka sana mimba zote mbili, ni mapenzi tu yalikuwa yanapungua kiasi tu.
 
hujawahi kuamshwa usiku wamanane unaambiwa "NASKIAJOTO NIPEPEE"muhusika sasa anaepepelewa katoa jicho kama nini olewako speed ipunguee,utakiona utaambiwa unamnyanyasa,mara humpendi...makasheshe kibao

Teeh.... teh...!!!!!Pole yako ulitaka ukimpepea afumbe macho?,
 

Pole ndugu, hiyo ni mimba tu vumilia akishajifungua atarudi kwenye hali yake ya kawaida, mimi nilipokuwa mjamzito mume wangu alikuwa akirudi nyumbani bila mahindi ya kuchoma yaani halali atatafuta popote mpaka apate, siku moja alichelewa kwenye kikao akakuta wachoma mahindi wamefunga, alipokuja nyumbani akanielezea kiukweli sikumuelewa yaani nilianza kulia kama mtoto mdogo.

Akanibembeleza yaani sikujiskia kabisa kunyamaza, ikabidi awashe gari saa nne hiyo akaenda hadi Tegeta akapata mahindi ambayo hayajajomwa akanunua alipofika nyumbani ikabidi tuwashe mkaa tuanze kuchoma yaani yaliiva saa saba usiku ndio moyo wangu ukatulia nikala nikalala.
 
Nilishawahi kuamshwa saa tisa usiku nikanunue chips kavu...thanks God kulikua na bar inayokesha karibu.......Mimba kiboko!:bange:
Bora hizo chips zinapatikana muda wote, miwa ni kimbembe mkuu..,
 
I can see myself in your husband, nashukuru sana kwa mawazo yako, hapo sasa naamini yataisha. Thanks mtende.
 
Kuna jamaa alikurupushwa saa nane za usiku mkewe kamwambia anahitaji matango jamaa akabanwa kweli ikabidi akapige hodi kwa muuza matango kwa bahati nzuri akapewa!

Kuyaleta nyumbani akaambiwa ayakatekate kisha ampe akae nayo awe anayanusa maana anapenda harufu yake!
Chezeiya mimba wewe!
 
Mkuu mbona hayo yako madogo
Mshukuru mungu hujaambiwa kaniamshie jirani nataka kumuona wakati huo ni saa 7 au 8 halafu jirani mwenyewe mwanaume
 
Nilishawahi kuamshwa saa tisa usiku nikanunue chips kavu...thanks God kulikua na bar inayokesha karibu.......Mimba kiboko!:bange:

Poleni sana wa ndugu hizi mimba zinamambo kweli..
 
Mkuu mbona hayo yako madogo
Mshukuru mungu hujaambiwa kaniamshie jirani nataka kumuona wakati huo ni saa 7 au 8 halafu jirani mwenyewe mwanaume
dah! hili alo kiboko jamani...., ila utaenda tu. maana hasira zao ni balaa
 
Yaani huyo wako cha mtoto mimi mama angu alikuwa hataki kusikia harufu yoyote ile ya mafuta miezi tisa yote hakuna kupaka mafuta wala manukato

Pia alikuwa anapenda kula chakula alichopika baba tu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
mpeleke kwao akapumzike na kujifungulia huko:heh:
 
Duh, hii nayo kiboko, mleta uzi, vumilia tu, akishajifungua yote hayo yataisha na wote akili yenu itakuwa kwa new baby
Mkuu mbona hayo yako madogo
Mshukuru mungu hujaambiwa kaniamshie jirani nataka kumuona wakati huo ni saa 7 au 8 halafu jirani mwenyewe mwanaume
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…