Mimba ya ajabu - Mtoto akulia kwenye utumbo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mimba ya ajabu - Mtoto akulia kwenye utumbo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, Feb 26, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Dk. Asser Mchomvu wa Hospitali ya Mission Mikocheni jijini Dar es Salaam,
  akifafanua jambo kwa kutumia mchoro kuhusu mfumo wa uzazi juzi
  baada ya kufanikiwa kufanya operesheni na kukitoa kichanga
  [​IMG]Mtoto akulia kwenye utumbo miezi tisa
  [​IMG]
  Aokolewa kwa operesheni, mama afariki

  Ni maajabu, lakini imetokea jijini Dar es Salaam kwa mimba kutungwa ndani ya utumbo wa kawaida badala ya mji wa mimba na mtoto huyo amezaliwa kwa njia ya operesheni na yuko salama. Kazi kubwa iliyofanywa na jopo la madaktari wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Kairuki likiongozwa na Daktari Bingwa wa Upasuaji katika Hospitali ya Mikocheni jijini Dar es Salaam, ndilo la kushukuriwa kwa kufanikisha uokoaji wa maisha ya mtoto mchanga aliyekuwa kwenye sehemu ya tumbo la chakula juu ya tumbo la mama yake kwa miezi tisa.

  Mimba ya mwanamke huyo mkazi wa Kinondoni, jijini Dar es Salaam, ilijitunga katika utumbo huo kwa kipindi hicho hadi madaktari bingwa hao walipomfanyia upasuaji Jumatano wiki hii na kufanikiwa kuokoa maisha ya mtoto huyo. Hata hivyo, mama mzazi wa mtoto huyo, Elizabeth Kasongo (29), alipoteza maisha muda mfupi baada ya operesheni hiyo kutokana na kupoteza damu nyingi baada ya operesheni hiyo.

  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mikocheni, Dk. Asser Mchomvu, alisema kuwa walimpokea mama huyo hospitalini hapo na kumfanya vipimo na kugundua kuwa mimba yake ilikuwa imejitunga kwenye utumbo. Katika mahojiano maalum na NIPASHE jana hospitalini hapo, Dk. Mchomvu alisema kuwa wakati wa upasuaji huo, madaktari walifanikiwa kuokoa maisha ya mtoto huyo wa kiume, aliyekuwa na uzito wa kilo 2.6. "Tulijitaidi kadri ya uwezo wetu kumwongezea damu mama huyo, tulimwekea chupa za damu zisizopungua nane, lakini kila tukimwongezea damu ilikuwa haikai mwilini inatoka tu, hivyo alifariki muda mfupi baadaye," alisema Dk. Mchomvu.

  Akielezea sababu ya mimba hiyo kujitunga katika utumbo badala ya kwenye mji wa mimba kama inavyofahamika kwa watu wengi, Dk. Mchomvu, alisema kitaalamu mbegu za mwanaume zinapoingia kwa mwanamke na kwenda kurutubisha yai (ovary), yai hilo linaposhindwa kurudi katika mji wa mimba (uterus) kupitia mirija (fallopian tube) inasababisha yai hilo kujitunga katika mirija ya uzazi badala ya kwenye mji wa mimba. Aliongeza kuwa, yai hilo hukua katika mrija huo jambo ambalo husababisha kupasuka na yai hilo kudondokea katika baadhi ya sehemu za ndani ya mwili, ikiwemo kwenye ngozi ya utumbo, utumbo, au kwenye mafuta ya utumbo.

  Dk. Mchomvu alisema kuwa, mara nyingi mimba ya aina hii huchukua miezi mitano hadi sita na kusababisha mtoto kufia tumboni, lakini kwa mama huyo imekuwa tofauti kwani mtoto alikaa miezi tisa hadi siku ya upasuaji. Dk. Mchomvu alisema baada ya upasuaji walimfanyia vipimo mtoto huyo na hakuonyesha dalili zozote za matatizo na kwamba anaendelea vizuri na afya yake ni nzuri. "Mtoto anapozaliwa huwa tunampima kwa score 10, huwa tunamwangalia kama mtoto analia, mwili wake pamoja viungo vyake kama vinachezacheza, kama anapumua vizuri, rangi yake kama iko sawa, kwa mtoto huyu vyote anavyo," alisema Dk. Mchomvu.

  Akifafanua kitaalam zaidi, Dk. Mchomvu alisema, mimba za aina hiyo zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni mimba zinazotungwa katika utumbo mwembamba ambapo yai linadondokea nje ya uzazi na mimba zinazotungwa katika utumbo mpana ambapo kiumbe hutupwa nje ya mji wa mimba kupitia mirija ya uzazi. Alisema mimba za aina hizo zinaitwa ectopic ambazo asilimia 95 zinakuwa zimejitunga katika mirija ya uzazi. Dk. Mchomvu alisema matukio kama haya ni nadra sana kutokea duniani, na anakumbuka kusoma mojawapo lililotokea mwaka 1780. Hakufafanua ni wapi.

  Baba mzazi wa mtoto huyo, Okolewa Amoni, alisema wakati wote wa ujauzito mkewe alikuwa anajisikia vizuri na hakuwa analalamika chochote. "Sikuwahi kumsikia Elizabeth analalamika kama anajisikia vibaya, alikuwa yuko safi tu siku zote, kipindi chote tulipokuwa tunaenda kliniki na hii ndiyo ilikuwa mimba yake ya kwanza," alisema Amoni.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ya mungu mengi aisee ni balaa juu ya balaa...
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Aisee! Sijawahi sikia hii!
  Sasa ectopic inavyouma, huyu dada hadi ikapasua fallopian tube na kujibandika kwenye ukuta usio hata na sifa za kizazi!
  There is a God, I tell you!
   
 4. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #4
  Feb 26, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,481
  Likes Received: 12,756
  Trophy Points: 280
  Omg! Rip mama wa mtt
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kilichonishangaza kidogo ni madaktari kushinwa kuokoa maisha ya mama pia, ingawa ni jambo ambalo wao wenyewe wanajua waliamua kuokoa kiumbe kimoja badala ya kupoteza wote, na katika hao kulikuwa na otption ya kuokoa ambaye uwezekano ni kubwa zaidi wa kuhuika kuliko mwingine ambayo hakuna matumaini ya kuhisha maisha yake.
   
 6. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #6
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tunaopona mambo yanaenda kama yalivyo vila matatizo ya pekee huwa hatuwezi kufikiria matatizo zaidi, lakini kijapo kitu kisicho cha kawada hutufikirisha sana.
   
 7. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #7
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Jamani na hizi hospitali zetu nazo!!Kama mama alikuwa anaenda kliniki,mbona hawakugundua hili tatizo?
   
 8. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #8
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Hata mimi ndo ninapojiuliza, huko clinic walivyokuwa wanapima hdi 9month hawakugundua chochote jamani?

  Pole sana baba mtoto kwa kuptelewa na mke, tena ktk uzazi wa kwanza.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Feb 26, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,182
  Trophy Points: 280
  Some would say if there is a god, he would be more consistent and not this erratic.

  Some would look at this as more evidence for how prone to chance the nature of biological processes is.
   
 10. M

  Manchago Member

  #10
  Feb 26, 2012
  Joined: Feb 18, 2012
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duu! Poleni sana madaktar hiy ni kazi kubwa
   
 11. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  hiyo ni ectopic pregnancy,mara nyingi it doesnt reach 9 months lakini ikifika unazalisha kama laparatomy na sio caeserian section,baada ya hapo placenta unaiacha ndani ya mwili otherwise ukiigusa atableed balaa....rare but not strange
   
 12. Ally Kombo

  Ally Kombo Verified User

  #12
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 11,440
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kwa taarifa tu ...... Hii imetokea Muhimbili na alikuwa mama wa mapacha, mtoto mmoja akiwa katika mfumo wa kawaida na mwingine akiwa nje ya mfumo. Hakuna Dr. yeyote aliyegundua na wote walizaliwa salama wakiwa hai ! Hili liliripotiwa na gazeti la Mwananchi. Kwa Muislaam hili analielewa kwani limo ndani ya Quran.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa kawaida mama mjamzito anapohudhuria clinic walao mara moja katika nchi zetu maskini anatakiwa afanyiwe kipimo cha X-ray kuhakiki mfumo wa kiumbe kipya ni sahihi au laa.

  Kwa matokea haya ni dalili wazi hospitali alikokuwa anafanyiwa clinic ya ujauzito walikuwa wanajaza tu report kwenye makaratasi kwa mazoea badala ya kufanya uhakiki ambao ungeweza kutoa taswira sahihi na hivyo kufanya maandalizi ya muda mrefu kwa mama majamzito na mataktari ili kufanikisha uzazi huo.

  Kwa kawaida mjamzito afikishapo miezi minne hadi mitano kipimo cha X-ray hufanyika ili kubaini hata gender ya kiumbe. Lakini kilichotokea ghafla kugundulika wakati wapo kwenye ya mwisho ya
  delivery baada ya mama kujisikia uchungu ni dhahiri walichofanya madaktari ni zima moto tu matokeo yaliyohitimisha mama kupoteza maisha.
   
 14. Dero

  Dero JF-Expert Member

  #14
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 324
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  sio xray ni Ultrasound
   
 15. Domo Kaya

  Domo Kaya JF-Expert Member

  #15
  Feb 27, 2012
  Joined: May 29, 2007
  Messages: 530
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  X-Ray kwa wajawazito?????????????????, hii bado sikia kabisa tangu nazaliwa
   
 16. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #16
  Feb 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hii imetokea kwasababu clinic hawakufanya kazi yao ipasavyo kwanini ultrasound haikufanyika ?.Utakuta kadi ya clinic imejaa lakini hakuna vipimo vya maana.
   
 17. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #17
  Feb 27, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii ingetokea kwetu Ludewa ingekuwaje. Baridi ya kule si ndiyo ingekuwa balaa??
   
 18. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #18
  Feb 27, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Dah! Inasikitisha kwakweli.
  ''kazi ya Mungu haina makosa''.
   
 19. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #19
  Feb 27, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tatizo teknolojia ya hapa ni duni, nchi zilizoendelea wangegundua tatizo mapema na kuokoa maisha ya mama na mtoto.
   
 20. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #20
  Feb 27, 2012
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  :shock::lol::lol::lol::lol::lol::lol::lol:
   
Loading...