Zifahamu dalili zinazoashiria mwanamke ni mjamzito

Unanikumbusha pindi nalea mama watoto, nenda hospitali ndugu, miezi ya mwanzo kusema kweli inavituko vingi sana.
Nenda hospitali ukapate ushauri
 
Kitaalam tunasema hamna mimba ya mwezi mmoja. Anyway prd yako ya mwisho ilianza lini?hiyo damu ni matone machache (spoting) au mabonge? Inawezekana ni yai linajiimplant kwenye uterine wall but to be on the safe side wahi hospitali.
 
images (2).jpg Slide1.JPG images.jpg images (1).jpg ​


MWANAMKE anapopata ujauzito kwa kawaida huwa anaanza kuona dalili ambazo si za kawaida. Na ni wakati huo ambao ni muafaka kwake kuanza kuuchunguza mwili wake.

"Homoni zinazosambaa mwilini mara tu unapopata ujauzito husababisha mabadiliko kadhaa mwili ambayo yanaweza kugundulika kabla hata ya uchunguzi halisi kujua kama una ujauzito au la," anasema Melissa Goist, Profesa na Mtaalamu wa Masuala ya Uzazi wa Chuo Kikuu cha Ohio, Marekani.

Maumivu kwenye matiti

Hii ni dalili ya kawaida ya ujauzito ambapo nguvu za homoni mwilini huongezeka wakati yai linavyopata "rutuba", jambo ambalo huongeza wingi wa damu na kuyafanya matiti ya mwanamke kuvimba na kuwa makubwa isivyo kawaida.

Maumivu mwilini

Utaanza kusikia maumivu kama vile unataka kuingia katika siku zako. Kwa kawaida hali hii hutokea wakati yai likiwa linasafiri kwenda katika chumba cha mimba. Hivyo, hali hiyo husababisha sehemu hiyo itanuke taratibu na kusababisha maumivu hayo.

Kutokwa damu bila kutegemea

"Wanawake wengi hufikiria kutokwa na damu kidogo ni dalili ya kuwa katika siku zao. Lakini, katika hali halisi, kutokwa damu kusikotegemewa, huwakumba asilimia 25 ya wanawake wakati wa kurutubika kwa yai," anasema Goist. Anaongeza kwamba iwapo utaona hedhi yako inakuwa fupi au inafanyika katika hali ambayo si ya kawaida, unashauriwa kwenda kufanya kipimo cha ujauzito.

Kuchoka

Unapojisikia kuchoka na kukosa raha, au kutaka hata kulala wakati ukiwa kazini, lazima ufahamu kwamba mwili wako unajirekebisha kuingia katika kipindi kipya cha mabadiliko.


"Tambua kwamba katika kipindi cha mwanzo cha ujauzito ni muda ambao mtoto tumboni huanza kutumia sehemu ya nguvu zako na hivyo kukuletea uchovu na usingizi," anasema Goist.

Chuchu kuwa nyeusi

Chuchu huanza kubadilika rangi yake kutokana na chembechembe za uhai (seli) kuanza kufanya kazi kwa nguvu zaidi. Hata hivyo, Goist anasema: "Wanawake wenye ngozi nyeusi hawawezi kuiona dalili hii mapema hadi muda wa kama wiki kumi zipite."

Kichefuchevu

Hali hii huwapata asilimia 85 ya wanawake wanapopatwa ujauzito, ambapo nyakati za asubuhi ndipo hasa hujionyesha.

Mwili kuvimba

Kuna wakati kupungua kwa nguvu za uyeyushaji chakula kunaweza kukusababishia kuona tumbo limevimba na nguo zikawa zinakubana kutokana na chakula kujaa katika utumbo. Lakini hali hiyo ikiendelea, na ukaona siku zako haziji, basi ni vyema ukatambua kwamba tayari una ujauzito, na kinachokupasa ni kwenda kuhakikisha.

Kwenda haja ndogo mara kwa mara

Kwenda haja ndogo kila mara ni dalili kwamba kibofu chako kimeanza kufanya kazi ya ziada, ambapo huwa kinafanya kazi ya kuondoa maji kwa uthabiti zaidi wakati wa ujauzito. Hali hii pia hujitokeza mwishoni mwa ujauzito, ambapo kibofu kitakapokuwa kinarudia hali yake ya kawaida baada ya kufanya kazi kwa muda mrefu.

Tamaa ya vitu mbalimbali

Kutokana na mwili kuwa na ‘mzigo' wa ujauzito na hivyo kuchoka, hali hiyo humfanya mwanamke kutamani vitu mbalimbali ili kukidhi mabadiliko yaliyojitokeza katika mwili wake. Hii ni pamoja na kutaka, kwa mfano, aina fulani ya vyakula, au kufanya mambo ambayo hapo nyuma alikuwa hayapendi.

Kuumwa kichwa

Kuongezeka kwa damu kunaweza kusababisha kichwa kuuma japokuwa si sana, hususan katika wiki za mwanzo za ujauzito. Hata hivyo, hali hii hukoma mwili unapojirekebisha na mzunguko wa homoni unaotokana na ujauzito.

Kufunga choo

Homoni ambazo husababisha mwili kuvimba pia husababisha kufunga choo kutokana na mfumo wa kuyeyusha chakula kutofanya kazi vyema. Hata hivyo, hali hii inaweza kujitokeza zaidi wakati ujauzito unaendelea kukua.

Kuwa na hasira

"Kutokana na kuongezeka kwa homoni za utendaji kazi mwilini, hali hiyo itakusababishia uchovu, na kukufanya kuwa na hasira," anasema Goist

Kuongezeka kwa joto mwilini.

Kipimo cha joto la mdomo ni muhimu katika kutambua hali ya ujauzito. Kwa kawaida joto huongezeka kwa nyuzi moja au zaidi wakati yai likiwa linatunga mimba. Hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya wiki mbili, itakuwa inaonyesha dhahiri kwamba kuna ‘mtoto anakuja'.


Baadhi ya dalili za nje zinazoonyesha uwezekano wa kuwa na mimba ni pamoja na:
  • maziwa kujaa na kuwa magumu kidogo.
  • kunenepa ghafla kutokana na kuongezeka vikoleza mimba mwilini.
  • mabadiliko kitabia ya ghafla yasiyozoeleka.
 
Baadhi ya dalili za nje zinazoonyesha uwezekano wa kuwa na mimba ni pamoja na:
  • Maziwa kujaa na kuwa magumu kidogo.
  • Kunenepa ghafla kutokana na kuongezeka vikoleza mimba mwilini.
  • Mabadiliko kitabia ya ghafla yasiyozoeleka.
 
basi sawa ngoja nianze kujichunguza

Kama umefanya uhusiano na mwenzi wako bila kinga na kipindi ambacho ni cha rutuba basi huna budi kuwa na wasiwasi kama hukupanga itokee hivyo si vibaya ukifanya uchunguzi na uonapo dalili zaidi ya moja zinajitokeza ujue kuna uwezekano yai limerutubishwa.
 
Wakuu Heshima yenu

Nina mpezi wangu ambaye siku za karibuni alinijulisha kuwa anaujazito wangu lakini umetokea kwenye mazingira ambayo siyaelewi kabisa.

Tulifanya mapenzi tarehe 23/7 alikuwa siku za hatari yani siku ya 12 mzunguko wake ni siku 28 nikamuomba tutumie kinga akagoma akasema yeye mwenyewe anajua hawezi pata mimba anajua anachofanya nikamwini basi tarehe 1/8 akanijulisha anaujazito wangu nikamwambia wewe uliniambiaje?

Nilichokuja kuuliza huku ni kuwa Mimba inachukua siku ngapi mpaka ionekane kwa vile vipimo vya kujipima mwenyewe nyumbani?

> Pia kwa siku hizo ni kweli zinaonyesha dalili kuwa mimba ni yangu au nimebambikiwa


NB: Naomba usinitukane nipe ushauri tu Asante.
 
Kipimo cha kawaida kile kinaanza kuonyesha kuanzia siku ya 11 ya ujauzito lkn mwanamke akipitiliza siku 4-5 kutoka siku alotakiwa kuona siku zake bac mimba huanza kuhisiwa kwanza kabla ya matatizo mengine.
 
Hilo ndo kosa tunalofanya wengi,unamuuliza mwenzio kuwa mtumie kinga au la wakati mmeshafika kiwanjani!majibu ya hapo sio ya kuyaamini hata siku moja,hapo kila mtu anazungumza uongo ili lengo lake litimie na akili inarudi baada ya kumaliza.
 
kipimo cha kawaida kile kinaanza kuonyesha kuanzia siku ya 11 ya ujauzito lkn mwanamke akipitiliza siku 4-5 kutoka siku alotakiwa kuona siku zake bac mimba huanza kuhisiwa kwanza kabla ya matatizo mengn..

Asante sana Mkuu sasa kwa case yangu hapo ni siku Nane tu vip kuna ukweli amenimebambikiwa mkuu
 
Asante sana Mkuu sasa kwa case yangu hapo ni siku Nane tu vip kuna ukweli amenimebambikiwa mkuu

Mkuu hapo kujua ukweli kua umebambikiwa au la kwa sasa hivi mi nafikiri ni vigumu sana, kwa hio mi nakushauri uvumilie tu hadi mtoto atakapozaliwa utajua tu aidhs kwa kumuangalia au kwa kupima dna.
 
Pamoja na majibu mengi utakayopata la nyongeza ni kwamba in most cases siku ya kutunga mimba hua inajidhihiridha....kuna kuwa na hali tofauti kabisa katika kudo kwenu, ni hali ambayo huwa haielezeki, wenye uzoefu watakubaliana nami

Lingine ni kwamba msijaribu kuitoa hiyo mimba, kama ni yako utajua tu na kama sio yako pia utajua tu...cha kufanya mchukue mwende mahali mkae pekeyenu mpe anachohitaji kishapo muulize huku ukimwangalia moja kwa moja machoni "una uhakika huo ujauzito ni wa kwangu?" Uliza kwa sauti ya kawaida kabisa na usije kuendeleza maswali.
 
Option nyingine nenda maabara kapimeni.hapo utaambiwa mimba ina siku ngap then utalinganisha na siku mmefanya.ikiyumba hata siku moja hapo unadanganywa othrws huwa inaleta siku exactly. Kama ikaleta siku ileile chance ya kuwa umebambikiwa ni kama mwanamke alitembea na watu wawili tofaut hyohyo siku moja.
 
Cjakuelewa kijana. Huamini kuwa ana mimba au huamini kama mimba ni yako?

once unamwita mpenzi wako ina maana una mwamini 90% once (ume duu kavu kavu) so hutaweza kujua mtoto ni wako au la till azaliwe na muende pale nyuma ya ocean road hospital kuna ofisi za msema kweli.....but uwe jasiri kupokea majibu ya DNA
 
Back
Top Bottom