Habarini wakuu,
Bila kupoteza muda kama kichwa cha habari kinavyojieleza, ni jamaa yangu mmoja alinifuata na kuniambia kuwa wana ugomvi na mke wake juu ya mimba aliyonayo kwani mazingira aliyoipata hiyo mimba hayana udhibitisho au uhalali wa jamaa kuwa mmiliki.
Labda nieleze kwa kifupi juu ya mazingira menyewe, Kwa mujibu wa maelezo ya jamaa yangu, Jamaa ni mtu wa kusafiri safiri sana. Jamaa aliondoka nyumbani kwake tangu mwezi wa pili Mwaka huu 2016, mpaka sasa hajarudi nyumbani, na aliacha hali ikiwa shwari kabisa wala hakukuwa na dalili zozote za ujauzito.
Sasa juzijuzi tu mke wake amempigia simu akamwambia ana ujauzito wa miezi minne, jamaa alichanganikiwa na kukawa na mvutano mkali sana kati yake na mkewe, jamaa alihoji, mimba ina miezi minne hujaniambia kwanini? Jibu la mwisho la jamaa lilikuwa kama ilivyoandikwa kwenye kichwa cha uzi huu yaani "Mimba hiyo siitambui" Ikumbukwe kuwa mpaka saizi hajarudi nyumbani, wanawasiliana kwa njia ya simu tu, vilevile wana mtoto mmoja kwenye ndoa yao ambaye ana umri kati ya miezi 10 hadi 12.
Je, Kwa wataalamu wa mahusiano na sayansi ya uzazi na wale wenye uzoefu, pia wanawake wenyewe inawezezekana kweli kukaa miezi minne bila kujitambua kuwa una mimba?
Karibuni tunusuru ndoa ya huyu jamaa.
Nawasilisha.