Million 6 kuagiza Toyota Starlet Japan

Udochi

JF-Expert Member
Jul 25, 2015
784
1,055
Habarini wakuu,

Kuna jirani yangu Unahitaji kuagiza Toyota starlet kutoka Japan,
Bajeti yake ni shilingi milioni 6 mpaka kuanza kulitumia.

Matumizi yake ni kuendea kazini Siku 5 kwa wiki
(kutoka Kisarawe hadi Tegeta).

Pia kwenda nayo nyumbani kwao Babati
(angalau mara mbili kwa mwaka).
_______
Nimemwambia ngoja niwaulize wakuu wa JF na wenye uzoefu wa watoe msaada Juu ya haya mambo matatu I.e
1. Bajeti ya kununulia,
2.Uimara wa Hii gari kwa hayo matumizi &
3.Upatikanaji wa spea zake.

Msaada wenu Unahitajika wakuu.
 
GARI YA BEI YA CHINI KABISAAA KUAGIZA JAPAN NI KIRIKUU NAYO NI MILIONI SABA NA NUSU(7500000). ILA KAMA ATANUNUA HAPA TZ KUTOKA MIKONONI KWA MTU YAPO MAGARI HATA YA 2M.
 
Hiyo pesa haitoshi,ajiongeze hadi milioni nane,anaweza kuimiliki.
Kuhusu imara ,hata juta
 
Inategemea kuagiza ni gharama sana hata hapa town zipo bei poa tu mfano mm nnamjua mtu anayo yakwake no CEV anataka 5.5 fixed na haijawah hata kugongwa
 
Au kama hana hela ya IST aagize Vitz ndiyo succeser ya Starlet na ni fuel efficiency kuliko vitz. IST bei yake ni kubwa kuliko Vitz.
 
Starler ni ngumu kuliko ist, spare availability ipo poa na fuel consumption ipo poa sana, hiyo akitaka kwenda babati kwa kina gekul hata kila wiki anaenda
 
Starler ni ngumu kuliko ist, spare availability ipo poa na fuel consumption ipo poa sana, hiyo akitaka kwenda babati kwa kina gekul hata kila wiki anaenda
Uko sawa mkuu, watu wanaongea ushabiki tu, IST na Virtz huwezi linganisha uimara wake na Starlet hata kifogo. Spea zipo tele na ulaji wa mafuta almost the same kutegemea ni Starlet ya 1300cc or 1500cc. Muhimu ni kwamba kwa vile utaenda nayo mpaka babati basi tafuta yenye gia 5 or kwa jina lingine yenye overdrive gear na 1500cc. Highway mwendo ni mkali kidogo ukitumia ya gear 4 utakuta inakula mafuta sana ukilinganisha na ya gear 5 kwa vile itabidi uikandamize mafuta ili iende fasta. Hili ndio tatizo linawapataga wengi waliokimbilia gari za 4 cyl 1880cc na kuacha 6 cyl 1980cc kwa kisingizio cha mafuta. Utakuta wanajaribu kushindana mbio na 6 cyl matokeo yake engine hufa mapema.
 
Inategemea kuagiza ni gharama sana hata hapa town zipo bei poa tu mfano mm nnamjua mtu anayo yakwake no CEV anataka 5.5 fixed na haijawah hata kugongwa

Au kama hana hela ya IST aagize Vitz ndiyo succeser ya Starlet na ni fuel efficiency kuliko vitz. IST bei yake ni kubwa kuliko Vitz.

Starler ni ngumu kuliko ist, spare availability ipo poa na fuel consumption ipo poa sana, hiyo akitaka kwenda babati kwa kina gekul hata kila wiki anaenda

Mwambie jamaa yako starlet zimeacha kutengenezwa kitambo.... badala yake aongeze mpunga aagize ist

Wasiwasi ni kwamba mara nyingi magari tunayouziana hapa mjini mengi huwa na matatizo mbalimbali na hivyo watu huuza kwa kuwa wenyewe yamewashida.

Hivyo kwa tusiokuwa na uzoefu wa hayo mambo tunapigwa sana,
Mwishowe gari inaozea gereji.
 
Kwa uimara ni imara , spea zinaoatika kiurahisi lakini kwa pesa yake hataweza kupata kwani haitoshi. Kuagiza tu japan itamgharimu $1500 ambayo ni sawa na 3.3m ushuru wa starlet wa chini ni 3.5m hapo bado gharama za bandari na wakala wa meli na kumlipa agent ambayo inafika kama 650,000. View attachment 343943
 
Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1462091225.232258.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1462091225.232258.jpg
    29 KB · Views: 79
Back
Top Bottom