Kijana alianza vizuri lakini kwa sasa ameanza kuyumba, na endapo akitokea mtu mwingine au media nyingine nzuri anaweza akapotezwa
Millard kwa sasa ameanza mambo ya ubaguzi kwenye media yake, habalance tena habari zake, anapost mikutano ccm lakini habari za upinzani ameacha kupost, jana amepost mkutano wa ccm morogoro lakini kuhusu upinzani ameliruka
Kwa sasa hamna watu wanaofuatiliwa mitandaoni kama kundi la WCB lakini Millard haandiki kabisa habari zao kitu ambacho sio kizuri kwa mwandishi wa habari, ameshindwa kujifunza kwa wasafi media ambao wamekuwa hawana ubaguzi kwenye habari za wasanii na kucheza nyimbo zao
Kijana wetu anatakiwa abadilike la sivyo atajiharibia mwenyewe, sababu kazi ya uandishi haitaki ubaguzi kwenye swala la kureport habari, angalieni TBC baada ya kuacha kubalance habari na kugeuka kuwa tv ya kusifia sasa imepoteza watazamaji kabisa
Millard badilika