SI KWELI PreGE2025 Millard Ayo amechapisha taarifa ikisema 'Sugu kujiunga rasmi CHAUMMA

SI KWELI PreGE2025 Millard Ayo amechapisha taarifa ikisema 'Sugu kujiunga rasmi CHAUMMA

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
IMG_1319.JPG
 
Tunachokijua
Joseph Mbilinyi anayejulikana zaidi kwa jina la 'Sugu' ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Nyasa ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Pia aliwahi kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kwa vipindi viwili, mwaka 2010 hadi mwaka 2020. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulimuondoa Sugu katika nafasi hiyo baada ushindi wa Tulia Akson aliyekuwa akigombea kupitia Chama Tawala CCM.

Kwa sasa chama chake kinaendesha ajenda ya 'No reform no election' yenye lengo la kuhamasisha mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi kabla ya kufanya uchaguzi mkuu 2025. Ajenda hiyo imekuwa na mapendekezo mbalimbali yanayopaswa kufanyika ili kuwe na uchaguzi huru na wazi na kwamba hawatashiriki uchaguzi mpaka kufanyike kwa mabadiliko hayo.

Madai

Ipo taarifa inayosambazwa katika mtandao wa Facebook inayodaiwa kuchapishwa na Millard Ayo ikisema 'Sugu kujiunga rasmi CHAUMMA'


Uhalisia wa Chapisho


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa na Millard Ayo kwenye kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii bali machapisho hayo ni ya kutengenezwa na wapotoshaji waliotumia utambulisho huo kupotosha.​
Back
Top Bottom