Milio ya risasi yasikika usiku Bujumbura

Milio ya risasi yasikika usiku Bujumbura

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2014
Posts
3,344
Reaction score
2,537
Jeshi limegawanyika, asubuhi hii mapigano makali sana yamezuka mji mkuu wa Burundi kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais na wale watiifu kwa Jenerali aliyepindua...mapigano hayo yanaripotiwa kuzuka karibu na State media house ambayo toka jana ilikuwa chini ya watiifu wa Rais...

===========================
150514042624_meja_jenerali_niyombare_512x288_bbc_nocredit.jpg

Meja jenerali Godefroid Niyombare

Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza.

Rais huyo ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa kanda, baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.
Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao na kwamba udhibiti wa nchi uko mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wa nchi hiyo ,Bujumbura.

Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga. Mwandishi wa BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa.

Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.

Chanzo: BBC
 
Wanajeshi wanaounga mkono mapinduzi na wale wanaomtii Nkuruzinza nchini Burundi wamerushiana risasi kwenye kituo cha TV cha Taifa. Pia milipuko imesikika sehemu mengine za Bujumbura.
 
katiba ni ya kuchunga kwelikweli.........na lazima ifatwe!
 
Jeshi limegawanyika, asubuhi hii mapigano makali sana yamezuka mji mkuu wa Burundi kati ya wanajeshi watiifu kwa Rais na wale watiifu kwa Jenerali aliyepindua...mapigano hayo yanalipotiwa kuzuka karibu na State media house ambayo toka jana ilikuwa chini ya watiifu wa Rais...

Hao watiifu wa rais feki wapigwe tu, maana sasa tumechoka na wavunja katiba.
 
Kumbe kuna watu na akili zao wanamtii huyi mhuni...
 
Tatizo la jesh wanapokea amri kama mbwa, kumtii Piere ni ujinga mtupu
 
Inasemekana Kuwa Serikali Ya Museven Inajiandaa Kupeleka Jeshi Kubwa Kwa Ajili Ya Kuzima Mapinduzi Duru Zinase Piere Yuko Salama Katika Jiji La Kampala.
 
Wanajeshi wanaounga mkono mapinduzi na wale wanaomtii Nkuruzinza nchini Burundi wamerushiana risasi kwenye kituo cha TV cha Taifa. Pia milipuko imesikika sehemu mengine za Bujumbura.

Source: BBC news.

Iwe iwavyo jeshi limeasi hataweza kutawala tena Burundi hata kama wanaomtii watashinda. Busara ni muhimu kuliko mali kwani Nkurunzinza angekubali kutii Katiba na kustaafu angekuwa na heshima ya Rais Mstaafu na maslahi yake mazuri. Kwa sasa ni shida sidhani hata kama anaweza kuwa na familia yake tena na bado anaweza kuburuzwa ICC muda wowote kuanzia sasa.
 
Dah
Nimesikia BBC pia asubuhi wanasema kumbe rais piere jana hakufanikiwa kuondoka Tz kwenda Burundi!
Yeah...its very tricky! Waliofanya jaribio hawawezi kukubali kushindwa kirahisi maana wanajua consequences za kujaribu kupindua. Nkurunziza na genge lake pia hawatakubali kushindwa kirahisi. Ni lazima anatafuata namna ya kurudi (hata kwa bodaboda!)...tukumbuke kuwa nao walikuwa msituni kwa muda mrefu tu na hivyo shuruba kwake haitakuwa jambo jipya.

Kama ningekuwa mshauri wa Nkurunziza, ningemwambia aachane na kugombea muhula mwingine (hata kama katiba inamruhusu) for the sake of greater good to his country. Awaachie wengine kwa heshima naye ataheshimiwa. Inawezekana ameshachelewa kufanya maamuzi sahihi
 
Mapigano makali yanaendelea muda huu baana y jeshi tiifu na wale waliotangaza mapinduzi
chanzo AL JAZ
ILLAH
 
Back
Top Bottom