Milio ya Risasi yasikika mitaa ya Mwenge, Bodi ya Mikopo

Milio ya Risasi yasikika mitaa ya Mwenge, Bodi ya Mikopo

LENDEYSON

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2013
Posts
2,996
Reaction score
2,659
Wadau,nipo kwangu hapa Mori,nasikia Milipuko ya Mabomu nadhani ya machozi,sijui nini kinaendelea.Mwenye taarifa zozote please!

Hapa Mwenge karibu na ofisi za Bodi ya Mikopo askari wanapiga risasi juu, Kuna magari ya polisi aina ya difenda yakiwa na askari wa kutosha. Mpaka sasa ishasikika milio sita ya risasi. Watu wametahamaki na kuanza kukimbia hovyo kuokoa maisha yao.

Tutaendelea kujuzana...
Mkuu,

Mimi nilikuwepo eneo la tukio mwanzo mwisho leo pale kulikwa na mechi kwenye uwanja wa vinyago na timu 1 wapo ilikuwa ya jeshi.

So kulikuwa na wanajeshi wamevalia kiraia wakati game ikichezwa kuna polisi waliingia wamevaa kiraia na kukamata watu sasa walipiga risasi 1 na kuanza kukamata watu balaa. Na milipuko ya risasi ililindima baada ya polisi moja kumkamata MP na hapo ndipo vituko na picha ya ngumi kama za kwenye video ilitokea.

MP alitembeza kichapo kwa baadhi ya polisi waliokuwa wameshika bunduki jamaa kapigana na polisi walikuwepo defender 1 land cruser na Noah 1 wao wanampiga na vitako vya bunduki yy anapiga ngumi hatimaye alizidiwa nguvu na wananchi walikuwa wanamtetea yule mwanajeshi na baadhi ya raia wamekamatwa.

Cha kushangaza na cha hatari wakati polisi wanapiga risasi, hakuna raia aliyekuwa anakimbia hata 1 wala kuogopa zaidi ya kuwazomea na kuwazonga. Hii ni hatari sana.

Polisi ilibidi wapige risasi nyingi zaidi ili kuwatawanya raia sababu walizuia magari yasitoke na watu waliowakamata
 
Utasikia watu wameshakimbilia uvunguni na chini ya meza, mi nipo!
 
Ngoja wanaume wa pande hizo wataenda eneo la tukio na kutupia updates hapa.
 
Labda wanaapishwa wenyeviti wa mitaa.......lol
 
Hahahhaaahaah Hivi dar huwa kuna Maandamano kweli maana mikoa mingine Risasi kitu cha kawaida..... mabomu ya machozi watu washaona Moshi wa sigara
 
Yaani kila siku mabomu na risasi Dar,sijui huko mbele itakuaje.
 
Hahahhaaahaah Hivi dar huwa kuna Maandamano kweli maana mikoa mingine Risasi kitu cha kawaida..... mabomu ya machozi watu washaona Moshi wa sigara
Teh teh mabomu ya goms tu ilihamishia watu taifa,wacha waje tu panya road akili zizibuke...
 
wanaume wa daslamu waoga!puh
_

Tupo dar kiutafutaji zaidi sio bugudha za hawa wapuuzi,kuna haja gani ya kujibishana nao ilihali utaishia kupoteza maisha au viungo?
 
Mm niko mwenge stand nimesikia milio ya risasi lkn sijajua tukio ni niini?
 
Ni mechi ilikuwa inachezwa uwanja wa mwenge lakini ndani yake palikuwa na watuhumiwa wa panya road ambao walipanga uporaji baada ya mechi ndio wamewahiwa na kukamatwa.
 
Hiyo milio ya risasi inatoka hapo mwenge vinyago... nn chanzo? I will be back soon.
 
Wadau,nipo kwangu hapa Mori,nasikia Milipuko ya Mabomu nadhani ya machozi,sijui nini kinaendelea.Mwenye taarifa zozote please!

Hapa Mwenge ofisi za Bodi ya Mikopo askari wanapiga risasi juu, Kuna magari ya polisi aina ya difenda yakiwa na askari wa kutosha.Mpaka sasa ishasikika milio sita ya risasi. Watu wametahamaki na kuanza kukimbia hovyo kuokoa maisha yao.

Tutaendelea kujuzana...

Kama ni askari polisi basi nitashangaa sans ilikuwaje sikuPanya road waljvuokuwa mtaani hawa hawa polisi walijificha.
 
Back
Top Bottom