Koffi Annan
JF-Expert Member
- Dec 23, 2018
- 1,235
- 3,194
Kwenye jamii ya leo kumekua na mila mbalimbali ambazo zimekuwa zikifanywa na wazee wetu ila ujio wa dini umefanya tuzisahau. Je, mambo kama haya yapo au umeshawahi kushuhudia?
Nitaweka hapa visa vichache ambavyo nimeshawahi kusimuliwa na kushuhudia jinsi mila zinavyofanya kazi hata sasa katika familia zetu.
Kisa cha kwanza kuna ndugu yangu yeye alioa mwanamke na yule mwanamke alikua kila akipata ujauzito unatoka au mtoto kufariki wakati wa kuzaliwa mimba tatu mfululizo, wazee wakasema kuwa huyo mwanaume ana kaka yake aliyefariki tokea akiwa mdogo hivyo anatakiwa amkabidhi huyo mke kwa kaka yake ndipo atapata mtoto, jamaa akaenda akafanya mila na kunena tu maneno kwamba fulani(akataja jina la huyo kaka yake aliyefariki) nimekukabidhi huyu mke ni wako. Tokea hapo akawa anapata uzazi kama kawaida.
Kisa cha pili ni kuhusu Bibi mmoja wa jirani na home, huyu bibi alikua anataka kumpa mtoto wake wa kike shamba ila mume wake akakataa, akawapa tu watoto wa kiume, yule mume wake alipofariki bibi alikua na shamba lilibaki hivyo akataka kumpa huyo mtoto wa kike napo watoto wa kiume wakakataa.
Yule bibi akaenda kulaani kwenye lile shamba akasema hamna mtu atavuna kitu hapa na atakayekula chochote hapa atakufa, kesho yake akaenda kukata ndizi kwenye lile shamba alilolaani akapika akala, asubuhi tu alivoamka akatoka kibarazani akaanguka akafa hapo hapo wazee wakasema ile laana yake ndo imemchukua maana alisema mtu akila kitu hapo shambani afe.
Kisa kingine kule Uchagani kuna utaratibu wa kufanya sherehe ya kumbukumbu ya marehemu baada ya muda fulani tokea kifo cha marehemu wenyewe wanaita matanga, basi unaambiwa baadhi ya marehemu wasipofanyiwa matanga huwatokea ndugu zao au wanaukoo, kuna huyo alikuwa anamtokea mdogo wake wa kiume usiku anamchapa fimbo mpaka siku alipofanyiwa matanga ndo hiyo kitu ikakoma.
Wazee wanakwambia kuna vitu unaweza kufanya usifanikiwe kumbe kuna roho zipo nyuma yako may be zinateseka hivyo ukifanya kitu fulani zile roho za wale watu zinapata amani na wewe utaishi kwa amani.