CharmingLady
JF-Expert Member
- Apr 16, 2012
- 18,304
- 12,999
Kina msosi wa ndizi na maharage huko Kibosho, Utadhani ni keki!
Mimi mambo ya kimila na utamaduni naona kama kuzinguana. Vitu vingine kuachana navyo tu.
wakwe wa siku hizi wanataka smartfone na maipad hayo mengine tupa kule lol!!!! TGIF though....
Wengine tumechanganya makabila mpaka tumedata....
Ila mojawapo la kabila kwa wali na samaki weeeeeeeeeeeee
Yaani kama kaja kwako hajala wali samaki ujue hujamlisha........
Kabila nyingine nilizomix sisemi
Thanks
God
its Friday
Hamjambo
Back to Topic: Nchi yetu ya Tanzania imejaaliwa kuwa makabila mengi sana
zaidi ya mia moja kama sikosei. Katika haya makabila huwa kuna mila na
desturi mbalimbali ambazo mtu akifanyiwa huwa anaona kama amepewa
heshima ya pekee.
Mfano: Katika kabila nitokalo mimi, mkwe akienda kusalimia kwao na mkewe
huandaliwa uji wa aina fulani ambao umetengenezwa kwa unga wa ulezi na
mafuta ya ng'ombe, Almaarufu kama "Ikirunguri cha Bhairwa" yaani mkwe
akipewa huu uji huwa anakuwa amapewa HESHIMA ya PEKEE. Hiyo ni kifungua
kinywa.
Baada ya hapo atapewa togwa "Ubhusara" tena kichwaji hiko kitakuwa
kimewekwa kwenye "Ikisonzo" (nimekosa kiswahili chake) wakati akisubiri
chakula cha mchana.
Chakula cha mchana anapikiwa ugali wa Udaga, ugali huu utakwua umepikwa
kwa kutumia unga wa mtama uliochanganywa na muhogo, Pia ugali huu
ukitengwa mezani utakuwa umeweka namna hii.
ugali huu utaliwa kwa nyama ya ng'ombe au mbuzi bila kusahau "Kichuri"
pembeni.
HAYA MNAWEZA KUTUPIA CHAKULA AMBACHO NI CHA HESHIMA AU JAMBO LOLOTE LA
HESHIMA AMBALO MGENI ANAWEZA KUFANYIWA PINDI AFIKAPO NYUMBANI
CL
Mkuu hata uchanganye vp bado lipo moja lenye nguvu nalo ni la baba wa baba yako na ndio kabila lako, tz tumechanganyika sana makabila hadi inafikia ukiulizwa kabila unajibu "mimi mswahili" lakini bado asili ipo tu mkuu huwezi kuiepuka na ndio asili yako.
mgeni atapewa maziwa yatawekwa kwenye kibuyu( ekyanzi) kinang'aa na
kunukia vizuri. mbuzi au ng'ombe ni lazima achinjwe.maziwa ni lazima
sana na vyakula vingine vya kisasa+ kimila
Ni kweli mkuu hebu BADILI TABIA tuambie mila na desturi za kwao baba wa babu yako zipoje??