Mikutano ya Tundu Lissu pekee ndio ina uhalisia hapa Bongo, hainaga Maigizo. Huwa ananikumbusha Mikutano ya Nyerere

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Ni Ukweli ulio wazi Mikutano ya Tundu Antipas Lissu huwaga na Uhalisia na hata kama kuna sehemu BAVICHA wanamtengenezeaga Maigizo basi huwa wanatumia akili Kubwa.

Mara nyingi Tundu Lissu akisimama jukwaani kwenye mkutano huwa ananikumbusha Mikutano ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Mungu wa Mbinguni awabariki 😀
 
Shida hana mamlaka ya utekelezaji zaidi ya kutamka maovu ya sirikali na ahadi bila zisizo na uhakika, wananchi hawapendi hayo saaana!

Mwenzie wa CCM anatoa ahadi na utekelezaji wa matumaini, utasikia anamwambia "waziri nakupa mwiki tatu umeme umefika/maji yamefika/stend imeboreshwa"
Basi wananchi wanafurahia mpk kububujikwa na machozi 😃

CCM kuchomolewa madarakani bado sijaona nguvu hiyo.
 
Kule Marekani kwasasa mikutano ya Trump wananchi wanaudhuria kwa ajili ya kusikiliza kitu gani?
Wananchi wasiyo na uelewa wa namna serikali inavyoendeshwa hawawezi kuelewa maana ya kuudhuria kwenye mikutano ya adhara.
 
Ni Ukweli ulio wazi Mikutano ya Tundu Antipas Lissu huwaga na Uhalisia na hata kama kuna sehemu BAVICHA wanamtengenezeaga Maigizo basi huwa wanatumia akili Kubwa.

Mara nyingi Tundu Lissu akisimama jukwaani kwenye mkutano huwa ananikumbusha Mikutano ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Mungu wa Mbinguni awabariki 😀
Wewe jamaa uko kama kinyonga vile.

Hueleweki rangi yako. Na watu wa namna yako huwa hawaaminiki sana.

LAKINI KWA HILI, umesema kweli tupu. Huyu jamaa (TL) si tu mikutano yake ni halisi, haina upuuzi, mazingaombwe, uongo uongo mwingi na ulaghai wa ki - CCM na ki - Makonda..

Bali pia, huyu jamaa ana public audience communication skill ya kuvutia. Mtu yeyote hupenda na hachoki kumtazama na kumsikiliza..

Kama mpaka Ramadhan Kishimba (Mbunge wa Kahama - CCM) alitoroka kazini kwake kwenda kumsikiliza TL kwenye mkutano wake wiki kadhaa zilizopita alipokuwa mkoa wa Shinyanga na Kahama ndo ujue kuwa ipo siku Paul Makonda atakuja kuahirisha mikutano ili mradi akamsikilize TL kwenye mkutano wake!!
 
Msema kweli mpenzi wa Mungu 😀
 
Shida hana mamlaka ya utekelezaji zaidi ya kutamka maovu ya sirikali na ahadi bila zisizo na uhakika, wananchi hawapendi hayo saaana!

Mwenzie wa CCM anatoa ahadi na utekelezaji wa matumaini, utasikia anamwambia "waziri nakupa mwiki tatu umeme umefika/maji yamefika/stend imeboreshwa"
Basi wananchi wanafurahia mpk kububujikwa na machozi 😃

CCM kuchomolewa madarakani bado sijaona nguvu hiyo.
Kwakuwa box la kura haliheshimiwi, na watu Bado wanatumia njia ya kura kuwatoa ccm, basi ni kweli hawatatoka.
 
Ebu tuchambulie manufaa ya mikutano ya Tundu Lissu kwa mwananchi wa kawaida?

Ni lipi la kumsaidia mwananchi ambalo Lissu huwa analionhelea mikutanoni mwake?

Zaidi ya kutembea akieneza Chuki na Uhasama?
Lissu huwa anaongea matatizo bila njia mbadala ya utatuzi wake!

Ni upumbavu uliopitiliza kuweza kumfananishs Baba wa Taifa na hawa wanasiasa wachumia matumbo yao!

Ni lini Baba wa taifa alihutubia taifa na kisha kukimbilia ughaibuni?
 
Ni Ukweli ulio wazi Mikutano ya Tundu Antipas Lissu huwaga na Uhalisia na hata kama kuna sehemu BAVICHA wanamtengenezeaga Maigizo basi huwa wanatumia akili Kubwa.

Mara nyingi Tundu Lissu akisimama jukwaani kwenye mkutano huwa ananikumbusha Mikutano ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Mungu wa Mbinguni awabariki 😀
Opposition ya Tz mzuri sana, the same party can oppose for themselves
 
Ebu tuchambulie manufaa ya mikutano ya Tundu Lissu kwa mwananchi wa kawaida?

Ni lipi la kumsaidia mwananchi ambalo Lissu huwa analionhelea mikutanoni mwake?

Zaidi ya kutembea akieneza Chuki na Uhasama?
Lissu huwa anaongea matatizo bila njia mbadala ya utatuzi wake!

Ni upumbavu uliopitiliza kuweza kumfananishs Baba wa Taifa na hawa wanasiasa wachumia matumbo yao!

Ni lini Baba wa taifa alihutubia taifa na kisha kukimbilia ughaibuni?
Nimesema Mikutano ya baba wa Taifa

Sidhani kama utaelewa tofauti 😂
 
Ebu tuchambulie manufaa ya mikutano ya Tundu Lissu kwa mwananchi wa kawaida?

Ni lipi la kumsaidia mwananchi ambalo Lissu huwa analionhelea mikutanoni mwake?

Zaidi ya kutembea akieneza Chuki na Uhasama?
Lissu huwa anaongea matatizo bila njia mbadala ya utatuzi wake!

Ni upumbavu uliopitiliza kuweza kumfananishs Baba wa Taifa na hawa wanasiasa wachumia matumbo yao!

Ni lini Baba wa taifa alihutubia taifa na kisha kukimbilia ughaibuni?

Sidhani kama ulielewa mada au umekuja kuandika haraka haraka baada ya kuona jina la TL . Chuki ndio imefikisha siasa zetu hapa tulipo . Jadili hoja jamvini
 
Shida hana mamlaka ya utekelezaji zaidi ya kutamka maovu ya sirikali na ahadi bila zisizo na uhakika, wananchi hawapendi hayo saaana!

Mwenzie wa CCM anatoa ahadi na utekelezaji wa matumaini, utasikia anamwambia "waziri nakupa mwiki tatu umeme umefika/maji yamefika/stend imeboreshwa"
Basi wananchi wanafurahia mpk kububujikwa na machozi

CCM kuchomolewa madarakani bado sijaona nguvu hiyo.
Hatima ya hiki chama kinachoonekana kudumu milele kina mwisho. Hakuna marefu yasiyo na mwisho. Itafika siku ambayo ulimwengu utashangazwa na kitakachotokea, hata wao wenyewe watashangaa mno. Hili jambo hakuna anaeweza kuamini. Kwa kuwa mtandao ni kumbukumbu isiyofutika, ipo siku mtu atataka kusikia maneno haya
 
Back
Top Bottom