Mikutano ya CHADEMA nchi nzima yazimwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikutano ya CHADEMA nchi nzima yazimwa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Donyongijape, Nov 24, 2010.

 1. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2010
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  MSIMAMO wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kutoyatambua matokeo ya urais huku kikidai Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, umemtikisa Rais Jakaya Kikwete na chama chake, kiasi cha kuanza kuzuiliwa kufanya mikutano yake ya hadhara ya kuelimisha wananchi juu ya misimamo ya chama hicho.

  Hatua ya wabunge kususia hotuba ya Rais Kikwete na kutoka nje ya ukumbi wa Bunge wiki iliyopita, imeelezwa kuwatia hofu vigogo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), kwa sababu ya kile kilichoelezwa kuwa maslahi ya sasa ya chama chao na serikali yake yatakuwa mashakani ikiwa wananchi watazidi kuelewa manufaa ya hoja hizo za CHADEMA kwa taifa.

  Taarifa za kuaminika kutoka vyanzo vyetu mbalimbali zimethibitisha kuwapo kwa njama za kuizuia CHADEMA kufanya shughuli kubwa za kisiasa hususan mikutano ya hadhara, huku Jeshi la Polisi likidaiwa kutumiwa kufanikisha mpango huo.

  Mtoa taarifa wetu ndani ya makao makuu ya CHADEMA jana alilithibitishia kuwa tayari chama hicho kimeshazuiwa kufanya mikutano ya hadhara katika mikoa mbalimbali nchini iliyokuwa ihutubiwe na wabunge na viongozi wake wa mikoa.

  Mikoa inayotajwa kuzuiliwa kwa mikutano ya hadhara ni pamoja na Mbeya, Arusha, Mara, Manyara, Iringa na Mwanza ambayo wabunge wa chama hicho kupitia viongozi wa mikoa, waliomba vibali toka polisi kuruhusu kufanyika kwa mikutano hiyo.
  "Kuna mkakati umeanza na kutekelezwa na Jeshi la Polisi kwa kutumiwa na CCM kuidhibiti CHADEMA isikutane na wananchi, sababu ni hofu. Wanahofia wananchi watazidi kuelewa madai ya chama, watazidi kuyaunga mkono na kuwa madai ya kitaifa.

  "Wabunge wetu kwa kushirikiana na viongozi wa mikoa walipanga kufanya mikutano hiyo ambayo pia ililenga kuwashukuru wananchi kwa kutuunga mkono…Iringa mjini wamezuiwa…Arusha mjini, Musoma, Mbeya, Mwanza na kule Manyara, kote kulikoombwa vibali Jeshi la Polisi limekataa kuruhusu mikutano hiyo.
  "Lakini sababu wanayotoa wao ni kwamba hali ya usalama nchi nzima ni tete hasa baada ya chama hicho kutoa msimamo wa kutotambua matokeo ya urais na kwamba bado serikali haijaundwa, hivyo hawawezi kuruhusu uvunjifu wa amani," alisema mtoa taarifa huyo.

  Tulipojaribu kuwasiliana na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuhusiana na chama chake kuzuiliwa kufanya mikutano ya hadhara, simu yake iliita mara nyingi bila kupokelewa.

  Jitihada za kumtafuta katibu mkuu wake, Dk. Willbrod Slaa, pia zilikwama baada ya kujibiwa na mmoja wa maofisa wa makao makuu ya chama hicho kuwa alikuwa kwenye kikao kirefu.

  Hata hivyo, hatua ya Jeshi la Polisi kuizuia CHADEMA kufanya mikutano ya hadhara kwa madai ya kuwapo hali mbaya ya usalama nchini, inaonekana kutokuwa na mashiko hasa ikizingatiwa kuwa rais hajatangaza hali ya hatari.

  Mchambuzi mmoja wa masuala ya kisiasa na utawala kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alipoombwa kutoa ufafanuzi wake juu ya hatua hiyo ya Jeshi la Polisi alisema:
  "Kama wamezuia mikutano kwa sababu hiyo basi wamewaonea, rais hajatangaza hali mbaya ya usalama kama linavyodai jeshi hilo. Ni lazima hali hiyo itangazwe na mkuu wa nchi kwa mujibu wa Katiba…vyama vya siasa vina haki ya kufanya siasa, kukutana na wananchi na kunadi sera zao. Huwezi kuibana haki hii kwa kisingizio cha uvunjifu wa amani ambao haujulikani," alisema msomi huyo huku akihofia kutajwa jina lake.
  Kwa mujibu wa Ibara ya 32 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, rais anaelekezwa kutangaza hali ya hatari kwa kutuma nakala ya tangazo lake kwa Spika wa Bunge ambaye baada ya kushauriana na kiongozi wa shughuli za Bunge ataitisha kikao cha Bunge kujadili hali hiyo kabla ya kuiidhinisha.

  Ibara hiyo inasema, "Endapo inatangazwa kwamba kuna hali ya hatari katika Jamhuri ya Muungano nzima, au katika Tanzania Bara nzima au Tanzania Zanzibar nzima, Rais atatuma mara moja nakala ya tangazo hilo kwa Spika wa Bunge ambaye, baada ya kushauriana na Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, ataitisha mkutano wa Bunge, ndani ya siku zisizozidi kumi na nne, ili kuitafakari hali ya mambo na kuamua kupitisha au kutopitisha azimio, litakaloungwa mkono na kura za wajumbe wasiopungua theluthi mbili ya wajumbe wote, la kuunga mkono tangazo la hali ya hatari lililotolewa na Rais."

  Aidha, ibara hiyo imefafanua kuwa rais anaweza kutangaza hali ya hatari ikiwa nchi iko katika vita, inakaribia kuvamiwa na kuingia katika hali ya vita au kuna hali halisi ya kutoweka kwa usalama wa jamii katika Jamhuri ya Muungano au sehemu yake yoyote kiasi kwamba ni lazima kuchukua hatua za pekee ili kurejesha amani na usalama.

  Kiongozi mmoja wa makao makuu ya Jeshi la Polisi kwa sharti la kutotajwa jina lake aliliambia gazeti hili kuwa sababu ya kuwapo ‘hali tete ya usalama' nchini iliyotolewa na jeshi hilo si ya kweli kwani hali hiyo inapaswa kutangazwa na kuidhinishwa rasmi.
  Hatua ya CCM kuzuia maandamano yaliyoandaliwa na uongozi wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, inadaiwa kuwa ni maandalizi ya kuhalalisha Jeshi la Polisi kuzuia mikutano hiyo ya CHADEMA.

  Source: Tanzania Daima

  Mytake: Serikali ya CCM itatumia kila hila na hujuma kuzuia mabadiliko yasitokee lakini wamesahau kuwa nguvu ya UMMA ni zaidi ya Dola. Hoja ya chadema imekuwa mwiba kweli kweli tofauti na watu wengi walivyofikiria, sasa kila mtanzania (mwelewa) anatamani kuwa sehemu ya mabadiliko hasa ya katiba na tume huru. baada ya kufunguliwa macho na kujua kumbe hata wao ni sehemu ya hayo..Siku CHADEMA wakianza hii Mikutano yao,CCM watakuwa wamelamba garasa..!
   
 2. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,583
  Likes Received: 1,944
  Trophy Points: 280
  Habari yenyewe ni tete.....
  Hata hivyo habari hiyo hiyo inaeleza kuwa hali hiyo ya "utete" wa hali ya usalama imesababishwa na...
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  CCM isidhani itaendelea kuishi kwa amani kwa kuminya uhuru wa vyama vingine kukutana na wananchi. Huo ni uwoga wa kijinga (siyo kipumbavu). Hata wakichelewesha mikutano lazima itafanyika tu. Wananchi wanawasubiri kwa hamu sana viongozi wa chadema ili kuhabarishwa namna uchakachuaji ulivyofanywa na majambazi wa demokrasia.
  wananchi
   
 4. m

  mamtaresi Member

  #4
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Tunasubiri baraza la mawaziri liundwe na kuapishwa.

  Kama wataendelea kuwabania CHADEMA wasifanye mikutano yao, basi tutakuwa tumejua hii nchi inaongozwa kwa mfumo wa udikteta.

  CHADEMA wataieleza dunia nzima kuwa tanzania ina experience dictatorship.

  Vilevile na sisi wapenda mageuzi tutakuwa tumeyaona yanayofanyika, ujumbe utafika kwa wananchi hata bila mikutano kufanyika.
   
 6. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  yaani ccm wangejua jinsi tulivyochoka!...........hivi wabunge wa ccm bado wanaamini kuwa wanachaguliwa kwasababu ni wajuzi wa kuitetea sisiemu na si kuwatetea watz.............????????,......HUKUMU YAO YAJA
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Nov 24, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kwani sheria zinasemaje wanasheria wekeni sawa tujuwe

  mapinduziiiii daimaaaaaaa
   
 8. Konakali

  Konakali JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Umeanza kuwaendea wachanga, wajawazito, na wanyonge woote....!? Tafadhali, sana bila haki usitegemee amani...! Vinginevyo, kaseme....!
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  wapenda amani au majizi ya kura
   
 10. K

  KIBE JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hizo mbwembwe tu watabana wataachi si wananchi tunaelewa na tunajua hata wakibana bado cdm mbele kwa mbeleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 11. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #11
  Nov 24, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,419
  Likes Received: 3,767
  Trophy Points: 280
  Sitegemei STATEMENT tofauti na hii toka kwako.................
   
 12. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #12
  Nov 24, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Hilo ni kwelu na nimelithibitisha kwa diwani wangu mteule wa kimandolu kuwa wameandikiwa barua kwanza ya kuambiwa kuwa shughuli ya kutafuta diwani imeahirishwa hadi watakapopewa taarifa na pia hawaruhusiwi kufanya mkutano au maandamano yoyote yale.

  Sasa hili la udiwani nasikia wanataka kuleta wale wadada wa viti maalumu waingie huku kwenye vikao vya udiwani ili waweze kuwa na kura nyingi za umeya... Sasa sijui itakuwaje...

  Hili ya mikutano wamegoma leo ila wataachia tu..
   
Loading...