Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 54,605
- 27,414
Mikosi yazidi kumwandama Nazir Karamagi
Kizitto Noya na Boniface Meena
MGOMO uliodumu kwa siku nne katika Kampuni Kutoa Huduma mizigo Bandarini Tanzania (TICTS) umetikisa huduma za upakuaji wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam hadi serikali ikaamua kuingilia kati.
Habari zilizopatikana na kuthibitishwa jana na Waziri wa Miundombinu, Shukuru Kawambwa, zimesema kuwa mgomo huo wenye lengo la kushinikiza nyongeza ya mishahara, ulianza Jumanne iliyopita na kwamba umeshusha upakuaji mizigo kutoka makontena 25 hadi matatu kwa saa.
Hata hivyo, serikali juzi ilingilia kati kupitia kwa Katibu wa Wizara ya Miundombinu, Omar Chambo na kuwaomba wafanyakazi hao kuahirisha mgomo huo hadi Jumanne wakati uongozi TICTS utakapokutana na wafanyakazi.
Tangu kuanza kwa mgomo huo kiwango cha utendaji wa wafanyakazi kimeshuka na hivyo kusababisha makontena ya mizigo kujazana bandarini hapo kusababisha usumbufu mkubwa kwa wafanyabiashara.
"Mgomo huu wa sasa ulikuwa ni rasha rasha lakini kama Jumanne hakitaeleweka kitu, tutagoma moja kwa moja," alisema mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake gazetini.
Alisema mgomo huo una lengo la kushinikiza nyongeza ya mishahara ili uwe na uwiano sawa na mishahara wanayolipwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
Kawambwa alisema tayari ofisi yake imeanza uchunguzi wa kina kuhusu madai ya wafanyakazi hao ikiwamo kupitia mikataba ili kuona kama wana hoja za msingi kudai nyongeza.
"Taarifa ninayo na tayari nimetuma maafisa kufanya uchunguzi ili tubaini ukweli na chanzo cha tatizo kabla ya hatujatoa taarifa ramsi ya serikali," alisema.
Madai hayo ya wafanyakazi yamekuja wakati vumbi la malalamiko dhidi ya mkataba wa uwekezaji wa TICTS kuwa uliongozwa muda kimyemela halijatua. Hata hivyo, Ikulu ilimtetea Karamagi kuwa hatua zote zilifuatwa kuiongezea kampuni yake mkataba kabla ya ule wa awali kumalizika.
TICTS ni kampuni binafsi ambayo mmoja wa wamiliki wake na mbaye alikuwa mwenyekiti wake wa bodi ni aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.
Karamagi alikuwa Mwenyekiti wa TICTS kabla ya kuondolewa Mei 8, mwaka huu, lakini akiendelea kumiliki asilimia 30 ya hisa katika kampuni hiyo kupitia Kampuni ya Port Holdings Limited. ??TICTS imekuwa ikitajwa katika vyombo vya habari na mijadala ya Bunge katika siku za karibuni, baada ya wabunge kulalamikia hatua ya kuongezwa kwa mkataba wake kwa miaka 15 zaidi, huku wakidai ufanisi wake siyo mzuri.