Kinaeleweka
Senior Member
- Nov 10, 2014
- 145
- 104
Habarini wapendwa,
Naomba niende moja kwa moja kwenye maada husika kwa kutumia uzoefu kutoka kwangu mwenyewe lakini na baadhi ya watu wa karibu wanaonizunguka.
Katika mihangaiko yetu ya kimaisha tunapitia mambo mengi tukiwa makazini katika biashara ,ujasiriamali na hustle nyingine.Kuna mengine yanatupelekea kuwa na ukwasi wa kutaka kujilimbikizia mali nyingi na hasa pasipo njia halali.Mie mwenyewe nimeshawahi kuajiliwa shirika fulani na nikajaribu kutengeneza myanya ya kupiga hela kama Tsh.35m.Hizo niliwekeza kwenye mashamba ya miti heka 30 huko Iringa na nyingne nikaanzisha kilimo cha vitunguu maji nikiamini vyote au kimojawapo kitanitoa.
Nilijitahdi sana kufuatilia kwa ukaribu hiyo miradi yote miwili,kwa maana ya kuhudumia miti kwa palizi na kuwekà mipaka ya kuzuia majanga ya moto lakini hasa kilimo cha vitunguu ambacho kilihtaji kuhudumiwa kwa karibu zaidi kwa maana ya umwagiliaji,palizi,madawa,mafuta ya diesel ya kuwashia pump ya kumwagilia na kadhalika na kilikuwa kinaendelea vizuri sana.
Kufupisha tu,miti ilipofika miaka 10 nikapata majanga ya moto ambao uliunguza karibu shamba lote.Moto unasemekana ulitokea shamba la jirani na kurukia shambani kwangu.Nilikatishwa sana tamaa na hasa nikizingatia gharama na muda niliopoteza katika kuwekeza hiyo miti.Pia shamba la vitunguu sikuwahi kupata faida licha ya kutumia gharama kubwa sana za uendeshaji.Mfano kuna kipindi nilitumia million 8 gharama zote nikaja kupata mil.1.5.Nikaja nikatumia mil.5 nikapata laki 6 nakuendelea.
Isitoshe,kuna mazingira mengine unapiga hela ya dili,lakini mikosi unayokutana nayo.Unakuta mara umepata ajari.Hiyo fedha unakuta inashia kwenye hiyo ajari.
Lakini kuna ushuhuda kwa watu wengine pia,jamaa mmoja alipiga deal hela ya maana akajenga apartments na kuweka wapangaji ila unakuta wapangaji hawalipi kodi,na akiwatimua na kuweka wengine unakuta hali inajirudia.Aliwekeza kwenye viwanja pia lakini kuna migogoro ilitokea ambayo ilimfanya apoteze hela nyingi mahakamani kwa kuweka mawakili.Lakini bado mgogoro haujaisha.
Hitimisho,nimekuja kugundua kuwa vitu visivyo halali havina baraka mbele ya mwenyezi Mungu.Utakosa amani binafsi lakini pia mradi hautakuletea faida utayotegemea baadae.Hapo nakumbuka mafundisho ya Yesu kwa mitume wake,kuwa tusisumbukie maisha ya kuwa tutakula nn au tutavaa nn,kwani Mwenyezi Mungu anajua shida zetu tayari.Tazama ndege wa angani hawalimi wala kuvuna lakini wanaishi vizuri.Je,sisi si zaidi ya hao ndege.
Baraka kamili za Mungu zinapatikana kwa kushika amri zake na hasa kupitia Malaki 3:8-10. Ahsante