Mikopo ya wafanyakazi wa benk

Ramosi255

Member
Aug 24, 2016
11
45
Naomba kuuliza wadau wa sheria. Niriajiriwa bank na baada ya miezi sita nikapewa mkopo wa 10m na nikawa nalipa nikiwa mfanyakazi hapo bank. Nikapata fursa ya kuitwa na mwajiri wangu wa zamani kwa maana bank ajira ilikuwa kwenda polisi any time na dau la mara hii likawa zuri nikaenda. Bank wakaniondolea rate yao ya ufanyakazi wakaweka riba ya mtu wa kawaida. Nikalipa deni kwa miaka miwili kama nusu hvi ila sasa huku kazi nimepunguzwa baada ya kampuni kukosa tender. Kifupi sina kipato kabisa na mkopo haukuwa nadhamana zaidi ya salary. Bank wana nipigia simu sana na kuniambia watanikamata na kutaifisha mali au kitu ninachomiriki hata kama nimesha lipa 50% ya loan yao. Nifanyeje hapa sasa kosheria. ??
 
Voiced Voice

JF-Expert Member
Feb 1, 2018
248
250
labda niongelee nililojifunza hapo. Tamaa mbaya. Unapopata hata kilicho kidogo ridhika, haya maswala ya kuhama hama kazi kiala siku sio kabisaa. Kwanza nao benki hawako serious. Utamkopeshaje mtu ndio anaajiriwa tu? Nadhani walikuthamini kwa kuwa ulikua mfanyakazi wao ila wewe hukuwathamini. Kasome masharti ya mkopo yatakusaidia kujua hatma yako kabla hawajakufilisi
 
Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,698
2,000
Badili no ya simu... Tafuta kazi nyingine ukipata utaendelea kulipa. Hiyo benki hawana hata uwezo wa kukunyang'anya kalamu kwa kuwa hukusaini fomu ya zamana. Ishi kwa amani kabisa wala usiwe na hofu. Hizo ni kelele za chura.
 
Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,291
2,000
Naomba kuuliza wadau wa sheria. Niriajiriwa bank na baada ya miezi sita nikapewa mkopo wa 10m na nikawa nalipa nikiwa mfanyakazi hapo bank. Nikapata fursa ya kuitwa na mwajiri wangu wa zamani kwa maana bank ajira ilikuwa kwenda polisi any time na dau la mara hii likawa zuri nikaenda. Bank wakaniondolea rate yao ya ufanyakazi wakaweka riba ya mtu wa kawaida. Nikalipa deni kwa miaka miwili kama nusu hvi ila sasa huku kazi nimepunguzwa baada ya kampuni kukosa tender. Kifupi sina kipato kabisa na mkopo haukuwa nadhamana zaidi ya salary. Bank wana nipigia simu sana na kuniambia watanikamata na kutaifisha mali au kitu ninachomiriki hata kama nimesha lipa 50% ya loan yao. Nifanyeje hapa sasa kosheria. ??
Waambie humiliki chochote
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom