Mikopo ya vyuo tayari. Semeni lingine tena tuone

Mikopo ya vyuo tayari. Semeni lingine tena tuone

Kuna watu wamejipanga kukosoa serikali mpya. Sasa soma taarifa hii mpaka mwisho uone inavyoshughulikia matatizo ya Wtanzania
SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA
Ndugu wanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo kikuu cha Dar es Salaam,wanafunzi wa vyuo vyote nchini na watanzania kwa ujumla, serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam inapenda kuwajulisha kuwa inayo taarifa juu ya sintofahamu nzito kuhusu suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wa mwaka wa kwanza wa masomo 2015/2016 ambapo idadi kubwa ya wanafunzi waliodahiliwa na vyuo mbalimbali nchini wamekosa mkopo. Mfano katika chuo kikuu cha Dar es salaam ni wanafunzi 684 tu waliopata mkopo kati ya wanafunzi zaidi ya 6,000 waliodahiliwa na chuo mwaka wa masomo 2015/2016.
Kutokana na hali hiyo, serikali ya wanafunzi (DARUSO ) kwa umoja wetu kupitia wizara ya mikopo, tuliamua kuungana na kuchukua hatua za kukutana na mamlaka husika ili kuhoji na kushinikiza utolewaji wa haraka wa pesa za mikopo kwa kundi kubwa la wanafunzi wenye sifa waliokosa mkopo katika chuo kikuu cha Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla ambapo kwa mujibu wa bodi ya mikopo (HESLB) ilionesha kuwa waliomba mkopo walifikia idadi ya wanafunzi zaidi ya 70,000 na walioonekana kuwa na sifa za kupata mkopo walikuwa 58000. Lakini katika hali ya kushtua, kushangaza na kusikitisha ni wanafuzi 12,000 pekee ndio waliokuwa wamepatiwa mkopo nchi nzima. Hivyo hatua zifuatazo zilichukuliwa ili kukabiliana na changamoto hii.
Mnamo tarehe 04/11/2014 Serikali ya wanafunzi ikiwakilishwa na kamati maalumu ya viongozi tulifika katika makao makuu ya bodi ya mikopo HESLB na kuzungumza nao kinagaubaga kuhusu uhalisia wa jambo hili na wao wakatupa majibu kuwa walipeleka maombi ya wanafinzi 58000 waliokuwa na sifa za kupata mkopo kwenda wizara ya elimu lakini cha kusikitisha ni kuwa ni wanafunzi 12,000 pekee ndio waliweza kupewa mkopo nchi nzima hivyo kuwalazimu HESLB kutoa mkopo kwa wanafunzi wachache katika kila chuo. Kutokana na majibu haya tulilazimika kuonana na katibu mkuu wa wizara ya elimu ili kujua kulikoni hali hii ikatokea.
Mnamo tarehe 06/11/2015 serikali ya wanafunzi kupitia kamati maalum tumeweza kufika wizara ya elimu na kukutana na kaimu mkurugenzi wa masuala ya elimu ya juu Dr. Mbwambo na kuzungumzia suala hili naye akatupa majibu yaliyokuwa pacha na majibu yaliyotolewa na bodi ya mikopo kuwa kulikuwa na upungufu wa fedha zinazofikia kiasi cha billion 132 ili kuwezesha wanafunzi wote nchini wenye sifa za kupata mkopo waweze kunufaika na mkopo huo, hivyo kutokana na maelezo hayo tulilazimika kuonana na katibu mkuu wa wizara ya elimu ili kuweza kujua ni hatua zipi zimechukuliwa ili kuweza kupata kiasi hicho cha fedha kilichopungua. Lakini tunasikitika kuwa hatukuweza kukutana na katibu mkuu licha ya ukweli kwamba tuliweza kuacha ujumbe wetu kwa katibu wake binafsi. Baada ya hatua hii tuliona ipo sababu pia ya kujua ni nini kinachowakwamisha hazina kutoa pesa hizo.
Hivyo siku hiyo hiyo ya tarehe 06/11/2015 tulifika katika ofisi za hazina na kuzungumza na kamishina wa bajeti nae akatuomba tumpe mda wa kufanya kikao na watendaji wa wizara ya elimu pamoja na bodi ya mikopo na akaahidi kutupa majibu kwa njia ya simu siku hiyohiyo ya tarehe 06/11/2015 mara tuu baada ya kikao.
Hivyo, waziri wa mikopo chuo kikuu cha Dar es salaam MH SHITINDI VENANCE ameweza kupokea simu ya mkononi kutoka kamishina wa bajeti nchini tarehe 06/11/2015 muda wa saa 12:25 jioni na alimpa taarifa kuwa katika kikao cha kamishna na bodi ya mikopo pamoja na wizara ya elimu wameafikiana kutoa fedha ndani ya masaa 48 kwa wanafunzi wote nchini wenye sifa na vigezo vya kupata mkopo lakini majina yao hayakuwamo katika majina yaliyokuwa yametajwa hapo awali.
Hivyo wizara ya mikopo katika selikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam(DARUSO) Inapenda kuwatangazia wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla kuwa tutaendelea kusimamia kila hatua mpaka hatua ya mwisho ya mchakato huu pale pesa zenu zitakapo patikana ili muweze kuipata elimu ya chuo kikuu pasi na kikwazo chochote.

IMETOLEWA NA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO)
UNITY IS POWER.
wewe kweli hamnazo mimi nikajua majina tayari
 
Karibu sana UDOM.It is the "Home Of Excellence In Africa"

Waache wajigambe ila sisi tukifika pale hatuhitaji maelezo wala majadiliano, Ni pesa mkononi basi then tunasukuma kitabu. Wakizingua na sisi tuko tayari kutibua. Waongeze mida wa Likizo tu ila tukifika pale kila kitu kiwe oky
 
Yaani heading na kilichopo tofauti. Unasema mikopo ya chuo tayari wakati inashughulikiwa! Heb change title mkuu.
 
Sa mbona umeandika ukiwa umepanic kwani ilo tamko ndo utekelezaji wewe mbona unakuwa na fikra finyu kiasi hicho subiri utekelezaji uje hapa ujipige kifua tuliahidiwa mangap hayakutekelezwa? Kama ni lugha ya kisiasa tu utajuaje uwe unaweka akiba ya maneno usikurupuke tu hata madereva wakati wanagoma waziri alienda akahidi matatizo yao yangeshughulikiwa lakin unajua nini kimeendelea mpka leo?

Shut up...subiri utekelezaji wa hayo yaliyoandikwa urudi hapa

Kula "LIKE" yangu
 
Mleta thread alivyokurupuka nkajua vijana wamepata mpunga!!! Hiyo taarifa sasa ndo hela ama? Vijana wanataabika sana. Ukifika UDSM ndo utajua hali halisi.
 
Ni kweli nilivyo soma heading nikajua tayari serikali imeshapeleka hela kwa wanetu kumbe ni porojo tupu. Sasa vijana wakianza kuandamana tutasingizia upinzani ndy wanao wahamasisha wagome na waandamane. Ushauri wangu ni bora hazina waseme ukweli kama hela ipo au haipo na kama ipo ni lini hao vijana watapata hiyo mikopo yao. Watanzania tunataka kuona komitments zilizo semwa majukwaani wakati wa kampeni. HAPA NI KAZI TU!
 
Izi hela wangekuwa wanazitoa mifukoni mwao sijui ingekuwaje hawa jamaa ukakasi umewajaa kama ela zao.
Ivi nao wangenyimwa mikopp wamefika walipo Leo.
JPM hawa ndo wa kuanza nao hawa kwa kuwasababishia sintofahamu wanafunzi kiasi wengine washarudi makwao
 
Karibu sana UDOM.It is the "Home Of Excellence In Africa"

najlaumu kusoma udom bora ningesoma kwa mama ngoma mwenge nyuma ya uwanja wa mpora, udoso ndo akuna kitu kabisa vichwa maji badala wafatile mikopo ya wadogo zetu ndo kwanza wamelala
 
najlaumu kusoma udom bora ningesoma kwa mama ngoma mwenge nyuma ya uwanja wa mpora, udoso ndo akuna kitu kabisa vichwa maji badala wafatile mikopo ya wadogo zetu ndo kwanza wamelala
Hahahaa...dah! Kikoozi upo udom tena siku iz..
 
Uyu mtu anajiita kikoozi usikute mkata mkaa tu...manake kila chuo kasoma yeye!
 
Ukishakaa hapo miaka miwili hii kauli utaifuta, ingia ukutana na mazengwe chungu mzima

ngoja aanze kukutana na fitina za lecturers ndo aone uchungu wa UDSM...... wahadhiri wana roho mbaya wale sijawah ona kudadek
 
Waache wajigambe ila sisi tukifika pale hatuhitaji maelezo wala majadiliano, Ni pesa mkononi basi then tunasukuma kitabu. Wakizingua na sisi tuko tayari kutibua. Waongeze mida wa Likizo tu ila tukifika pale kila kitu kiwe oky

kabisaa maana koleji zote lazima kinuke
 
Yaani heading na kilichopo tofauti. Unasema mikopo ya chuo tayari wakati inashughulikiwa! Heb change title mkuu.
Hapo hata mie nimechanganyikiwa heading inaonyesha maneno tayari yameshakuwa sawa halafu content inaelezea mchakato wa ufuatiliaji ambao bado haujazaa matunda mpaka sasa
 
Back
Top Bottom