Mikopo ya vyuo tayari. Semeni lingine tena tuone

Mikopo ya vyuo tayari. Semeni lingine tena tuone

Potelea Mbali

Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
46
Reaction score
5
Kuna watu wamejipanga kukosoa serikali mpya. Sasa soma taarifa hii mpaka mwisho uone inavyoshughulikia matatizo ya Wtanzania
SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO)
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU MIKOPO KWA WANAFUNZI WA MWAKA WA KWANZA
Ndugu wanafunzi wa mwaka wa kwanza Chuo kikuu cha Dar es Salaam,wanafunzi wa vyuo vyote nchini na watanzania kwa ujumla, serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam inapenda kuwajulisha kuwa inayo taarifa juu ya sintofahamu nzito kuhusu suala la mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu wa mwaka wa kwanza wa masomo 2015/2016 ambapo idadi kubwa ya wanafunzi waliodahiliwa na vyuo mbalimbali nchini wamekosa mkopo. Mfano katika chuo kikuu cha Dar es salaam ni wanafunzi 684 tu waliopata mkopo kati ya wanafunzi zaidi ya 6,000 waliodahiliwa na chuo mwaka wa masomo 2015/2016.
Kutokana na hali hiyo, serikali ya wanafunzi (DARUSO ) kwa umoja wetu kupitia wizara ya mikopo, tuliamua kuungana na kuchukua hatua za kukutana na mamlaka husika ili kuhoji na kushinikiza utolewaji wa haraka wa pesa za mikopo kwa kundi kubwa la wanafunzi wenye sifa waliokosa mkopo katika chuo kikuu cha Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla ambapo kwa mujibu wa bodi ya mikopo (HESLB) ilionesha kuwa waliomba mkopo walifikia idadi ya wanafunzi zaidi ya 70,000 na walioonekana kuwa na sifa za kupata mkopo walikuwa 58000. Lakini katika hali ya kushtua, kushangaza na kusikitisha ni wanafuzi 12,000 pekee ndio waliokuwa wamepatiwa mkopo nchi nzima. Hivyo hatua zifuatazo zilichukuliwa ili kukabiliana na changamoto hii.
Mnamo tarehe 04/11/2014 Serikali ya wanafunzi ikiwakilishwa na kamati maalumu ya viongozi tulifika katika makao makuu ya bodi ya mikopo HESLB na kuzungumza nao kinagaubaga kuhusu uhalisia wa jambo hili na wao wakatupa majibu kuwa walipeleka maombi ya wanafinzi 58000 waliokuwa na sifa za kupata mkopo kwenda wizara ya elimu lakini cha kusikitisha ni kuwa ni wanafunzi 12,000 pekee ndio waliweza kupewa mkopo nchi nzima hivyo kuwalazimu HESLB kutoa mkopo kwa wanafunzi wachache katika kila chuo. Kutokana na majibu haya tulilazimika kuonana na katibu mkuu wa wizara ya elimu ili kujua kulikoni hali hii ikatokea.
Mnamo tarehe 06/11/2015 serikali ya wanafunzi kupitia kamati maalum tumeweza kufika wizara ya elimu na kukutana na kaimu mkurugenzi wa masuala ya elimu ya juu Dr. Mbwambo na kuzungumzia suala hili naye akatupa majibu yaliyokuwa pacha na majibu yaliyotolewa na bodi ya mikopo kuwa kulikuwa na upungufu wa fedha zinazofikia kiasi cha billion 132 ili kuwezesha wanafunzi wote nchini wenye sifa za kupata mkopo waweze kunufaika na mkopo huo, hivyo kutokana na maelezo hayo tulilazimika kuonana na katibu mkuu wa wizara ya elimu ili kuweza kujua ni hatua zipi zimechukuliwa ili kuweza kupata kiasi hicho cha fedha kilichopungua. Lakini tunasikitika kuwa hatukuweza kukutana na katibu mkuu licha ya ukweli kwamba tuliweza kuacha ujumbe wetu kwa katibu wake binafsi. Baada ya hatua hii tuliona ipo sababu pia ya kujua ni nini kinachowakwamisha hazina kutoa pesa hizo.
Hivyo siku hiyo hiyo ya tarehe 06/11/2015 tulifika katika ofisi za hazina na kuzungumza na kamishina wa bajeti nae akatuomba tumpe mda wa kufanya kikao na watendaji wa wizara ya elimu pamoja na bodi ya mikopo na akaahidi kutupa majibu kwa njia ya simu siku hiyohiyo ya tarehe 06/11/2015 mara tuu baada ya kikao.
Hivyo, waziri wa mikopo chuo kikuu cha Dar es salaam MH SHITINDI VENANCE ameweza kupokea simu ya mkononi kutoka kamishina wa bajeti nchini tarehe 06/11/2015 muda wa saa 12:25 jioni na alimpa taarifa kuwa katika kikao cha kamishna na bodi ya mikopo pamoja na wizara ya elimu wameafikiana kutoa fedha ndani ya masaa 48 kwa wanafunzi wote nchini wenye sifa na vigezo vya kupata mkopo lakini majina yao hayakuwamo katika majina yaliyokuwa yametajwa hapo awali.
Hivyo wizara ya mikopo katika selikali ya wanafunzi chuo kikuu cha Dar es salaam(DARUSO) Inapenda kuwatangazia wanafunzi wote wa mwaka wa kwanza katika chuo kikuu cha Dar es salaam na Tanzania kwa ujumla kuwa tutaendelea kusimamia kila hatua mpaka hatua ya mwisho ya mchakato huu pale pesa zenu zitakapo patikana ili muweze kuipata elimu ya chuo kikuu pasi na kikwazo chochote.

IMETOLEWA NA SERIKALI YA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO)
UNITY IS POWER.
 
Sa mbona umeandika ukiwa umepanic kwani ilo tamko ndo utekelezaji wewe mbona unakuwa na fikra finyu kiasi hicho subiri utekelezaji uje hapa ujipige kifua tuliahidiwa mangap hayakutekelezwa? Kama ni lugha ya kisiasa tu utajuaje uwe unaweka akiba ya maneno usikurupuke tu hata madereva wakati wanagoma waziri alienda akahidi matatizo yao yangeshughulikiwa lakin unajua nini kimeendelea mpka leo?

Shut up...subiri utekelezaji wa hayo yaliyoandikwa urudi hapa
 
najivunia kuwa udsm...na kukutana na vchwa hatar km hvi vya kimapinduz
 
Ukweli ni kuwa serikali haina pesa. Ila pamoja na kutokuwa na pesa nina imani Mh. Rais ataliona hili na kuagiza wanafunzi kupewa pesa kwa kubana matumizi mengine ya serikali yasiyokuwa ya lazima sana au yasiyokuwa ya haraka sana.
 
Tatizo nyie madogo huwa hamjielewi ni kwamba nature ya serikali yetu kufanya kazi mpaka isukumwe kwa maandamano au kelele kwenye social network ndio utawaona vigogo wanafanya kazi kwa kujituma mfano ni ajira za walimu 2015 watu walipiga kelele sana na hili la HESLB kwa hiyo watu wanapoikosoa serika ili itekeleze majukum yake kwa wakati utaona wapumbafu wanaanza kuitetea serikali hao ni wasaliti wabinafsi na wasiotakia wenzao mema wasome serikali ikikosea tuungane kwa saut moja kusema mfano kama huyu mpuuz anaeanza kwa kusema "cimnasemaga serkal haifanyi kazi' huyo ni namuita hajitambui na anaroho ya kichawi huwezi ona mtu hana mkopo afu uciseme
 
Tunataka ziingie kwenye akaunti za wanafunzi siyo maneno maneno tu! Hivi wale was awamu ya kwanza wameshaingiziwa kwenye akaunt zao?
 
Wengi wao ni ufinyu wa fikra alafu hawa watoto ni maselfish sana yani unaweza kuta ambae ameweka bandiko hapa yeye amepata mkopo tayari na ndo maana anaanza andika haya angelikuwa kwenye lile kundi la wengi waliokosa angekuwa anapost lawama tu hapa, huu ni upuuzi uliotukuka kuleta ahadi ambazo hazipo hata kwenye maandishi na kusema tayari utekelezaji umeanza subirini wenzenu wapate pia hiyo mikopp ndo mje hapa kwa madaha mkiisifia serikali sio unaisifu kwa sababu tu wewe sio muhanga acheni ujinga kun watoto wengi sana wa masikini huko vijijin hawapati mikopo badala yake wanapewa ambao wazazi wao wakovizuri kifedha na wanaweza wasomesha watoto wao ila wanapata tu kwa sababu wao wanajuana na watu huko board hili ndo sisi hatulitaki kuliona na sio hizi soga mnazotuleta hapa.

Mleta mada umeshajiuliza ni wanafunzi wangap wamebaki vijijin kwao kwa sababu hawajapata mikopo?

Tumuombee mungu magufuli afanye kitu hii board ni uhozo mtupu, hakuna kitu huwa kinaniuma kama kusikia mwanafunzi amehairsha mwaka kwa sababu ya mkopo wakati huo huo kuna ambao wapo vizuri kifedha wanapata boom 100%
 
Hapa mpaka neno NOT SECURED liondoke katika akaunts za baadhi ya wengi ndo kitaeleweka lakini hayo maneno matupu si lolote si chochote
 
Nkajua tayari wanafunzi wamepewa mikopo kumbe lipo kwenye utekelezaji mmmh ishu nyeti kama hii haihitaji kuandikwa kiudaku udaku


Huyu jamaa hajielewi kabisa ni wakupuuzwa tu maana amefanya kucopy mrejesho wa viongozi wa daruso na kuongezea maneno yake ya kipuuzi tena ya kishabiki ilihali hii ni sensitive issue
 
acheni upumbafuuu..... ata aalija tekelezwa mshaa keelele kelele, za kifumbafuu....


����
 
Acha upuuzi wko, sasa apo kilichifanyika ni nini? C ahadi zilezile, km hawakutoa mwazo ndani ya saa 48 wataztoa wapi? Acha kutetea upuuz mtoa mada
 
Mtaisoma namba sana..ccm ndio Ile Ile hakuna cha mkopo hao 83% imekula kwao.
 
Back
Top Bottom