SoC01 Mikopo ya Biashara ya Vijana Serikalini

Stories of Change - 2021 Competition

flulanga

JF-Expert Member
Jul 1, 2016
4,861
6,342
Serikali kupitia mapato ya halmashauri kumekuwepo na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo kwa vijana na watu wenye ulemavu.

Wimbi kubwa la vijana kulalamika ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji ya biashara, kilimo na shuuri nyingine za kuwaingizia vipato hii ndio ilikuwa suluhisho endapo kama ingetumika vyema.

Kumekuwepo na habari kuhusu utoaji wa hiyo mikopo lakini uchangamfu wa vijana kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo imekuwa ndogo. Na serikali imekuwa haitoi elimu hiyo.

Naongelea uhalisia wangu mimi kama kijana. Ishawahi kumvaa mkuu wa mkoa na akanielekeza niende kwa muhusika na namba yake nikapewa. Nilimpata muhusika na muongozo mzima alinipatia, nikarudi mtaani ili niweze kufanya kile nilichoelekezwaaa.

Niliambiwa nifanye haya;

- Niunde kikundi cha watu kuanzia wa tano,

- Tuchague uongozi wa muda,

- Tuunde katiba yetu ambayo ndio utakuwa muongozo wetu,

- Tuchague uongozi kulingana na katiba tuliyoiunda,

- Tuanzishe mradi wowote kama ni kilimo au ufugaji, au biashara, au hata kiwanda kidogo.

- Na mwisho tufungue akaunti bank.

Baada ya vyote hivyo twende kwa afisa mtendaji wa eneo letu kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa kwaajili ya kupatiwa barua ya utambulisho twende nayo halimashauri kwaajili ya hatua nyingine zaidi.

Niliporudi mtaani ili niunde hicho kikundi cha watu kuanzia watano ndipo nilipogundua vijana wengi hawana muamko kuhusu hii mikopo ya serikali. Wengi ambao nilihisi nikiwapelekea hili wazo watalichangamkia ila kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Kila mtu alitoa neno lake analolijua yeye;

Kuna mwingine alisema 'serikali haiwezi kutoa pesa zake zaidi watatupotezea muda wetu bure'

Mwingine akasema ' hiyo mikopo inatoka kimjuano'

Mwingine akasema 'hatuwezi kupata pesa mpaka nasisi tuwe na pesa ya kuweka kwenye akaunt kwahiyo yeye hana hiyo pesa.

Na wengine walitoa kauli zakufanana na hizo. Na mwisho wa siku nikapata kijana mwenzangu mmoja tu kwahiyo kigezo cha kwanza cha kuwa na kikundi cha vijana watano kikatuangusha.

Nini kifanyike ili vijana waielewe hii fursa;

- Halimashauri zitenge muda wa kukutana na vijana na kuwapatia elimu kuhusu hii mikopo na iwahakikishie kuwa mikopo ipo na wala sio uraghai kama vile baadhi ya vijana wanavyoamini.

- Serikali za mitaa iwe na orodha ya vijana wanaojitambua na ambao tayari wameshaanzia chini na hatua waliofikia wanahitaji kuwezeshwa kupitia hiyo mikopo. Hii itajenga uhakika wa marejesho ya mkopo husika.

- Serikali ianze kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja kama vile ilivyo mikopo ya chuo elimu ya juu. Hii itapelekea kijana kupambana na marejesho yake bila kuhisi kuwa akikwama yeye basi wenzie watamlipia kupitia kikundi chake. Hili lilinikwamisha baada ya kukosa vijana wenzangu ila pangekuwepo na mkopo wa mtu mmoja mmoja uenda labda ningepata mkopo.

- Serikali itoa mikopo kwa wakati. Pamekuwepo na malalamiko mikopo ya serikali haitoki kwa wakati kama mlikuwa na wazo la biashara basi mpaka wazo hilo litapitwa na wakati ila mkopo bado.

- Mikopo itolewe kwa biashara ya mtu mmoja mmoja na wala sio kwa kikundi ili kukwepa vijana kutokuaminiana. Hii miradi ya vikundi pamekuwepo na kuzurumiana sanaaaa kwa baadhi ya wanakikundi kutokuwa waaminifu kwahiyo serikali iliangalie hili.

MWISHO; Serikali itoe elimu ya mikopo ya biashara kwa vijana kama vile inavyotoa elimu kuhusu uombaji wa mikopo ya elimu ya juu. Na vijana tuchangamkie fursa hizi na kama kuna vikwazo katika upatikanaji wa hii mikopo basi ni bora tukajionee wenyewe kuliko kusikiliza habari za mitaani.
 
Hii mikopo ina vikwazo sana. Lakini ipo na pesa zinatoka.

Mwezi ulioisha nilitamani kuanzisha kikundi, nikakutana na jamaa zangu, tukiwa ndugu kama watatu, tutakutana na huyo afisa, akatupa somo zuuri tu, tatizo likaja katika umri, ni kuanzia miaka 18 mpaka 35. Niliamua kuachananao baada ya kuona umri wangu ni zaidi ya miaka 35 nimevuka hapo..basi mm nikajitoa na nikawaachia wale wengine.

Wamepewa milioni 10. Lakini wanachokifanya si kile walichoandika katika ule muhtasar wakati wanaomba mkopo, kila mtu anafanya biashara zake..

Wakifanikiwa kulipa sawa, na wasipofanikiwa dijui hatma yao, lakini dalili sizioni.

Cha ajabu zaidi, kuna kikundi nimeona kina watu wana miaka 45 na kuendelea wamechukua pia mil 15, aah nikajis3mea kumbe mimi ni mdwanzi eeh? Basi ndo hivyo mzee baba nakomaa tu na hali yangu, lakini pesa zipo na zinatoka..

Kila la kheri mkuu.
 
Kikundi chenu baada ya wewe kujitoa kilibaki na watu wangapi? Je iliwachukua mda gani mpaka wakapata huo mkopo
 
Baada ya mimi kujitoa walibaki watu watano, maana awali nitafuta watu tulikuwa sita, baada ya mimi kujitoa walibaki watu watano, na ilichukua wiki 3 kuanzia mchakato mpaka kupata huo mkopo, mambo mengi ya mdingi alimaliza yule afisa mikopo! Kama kuandaa muhtasar, mwanasheria katiba na harakati zingine, gharama ilikuwa kama 60 tu..watu wakavuta mpunga, lakini sijui kama wataweza rudisha pesa ya watu wale madogo, maana naona wametoka nje ya lengo
 
Sawasawa. Kwa upande wa kurudisha au kutokurudisha mda ndio utaongea sio rahisi kupata jibu la moja kwa moja. Ubarikiwe mkuu kwa uzoefu wako mdogo umetoa mwanga kuwa mikopo ipoooo
 
Naam na walipewa miezi 15 ikiwemo miezi 3 ya mwanzo ambayo haina marejesho, baada ya miezi 3 ndipo marejesho yanaanza kama sijakosea..pamoja mkuu
 
Serikali kupitia mapato ya halimashauri kumekuwepo na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo kwa vijana na watu wenye ulemavu.

Wimbi kubwa la vijana kulalamika ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji ya biashara, kilimo na shuuri nyingine za kuwaingizia vipato hii ndio ilikuwa suruhisho endapo kama ingetumika vyema.

Kumekuwepo na habari kuhusu utoaji wa hiyo mikopo lakini uchangamfu wa vijana kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo imekuwa ndogo. Na serikali imekuwa haitoe elimu hiyo.

Naongelea uhalisia wangu mimi kama kijana. Ishawahi kumvaa mkuu wa mkoa na akanielekeza niende kwa muhusika nanamba yake nikapewa. Nilimpata muhusika na muongozo mzima alinipatia, nikarudi mtaani ili niweze kufanya kile nilichoelekezwaaa.

Niliambiwa nifanye haya;

- Niunde kikundi cha watu kuanzia wa tano,

- Tuchague uongozi wa muda,

- Tuunde katiba yetu ambayo ndio utakuwa muongozo wetu,

- Tuchague uongozi kulingana na katiba tuliyoiunda,

- Tuanzishe mradi wowote kama ni kilimo au ufugaji, au biashara, au hata kiwanda kidogo.

- Na mwisho tufungue akaunti bank.

Baada ya vyote hivyo twende kwa afisa mtendaji wa eneo letu kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa kwaajili ya kupatiwa barua ya utambulisho twende nayo halimashauri kwaajili ya hatua nyingine zaidi.

Niliporudi mtaani ili niunde hicho kikundi cha watu kuanzia watano ndipo nilipogundua vijana wengi hawana muamko kuhusu hii mikopo ya serikali. Wengi ambao nilihisi nikiwapelekea hili wazo watalichangamkia ila kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Kila mtu alitoa neno lake analolijua yeye;

Kuna mwingine alisema 'serikali haiwezi kutoa pesa zake zaidi watatupotezea muda wetu bure'

Mwingine akasema ' hiyo mikopo inatoka kimjuano'

Mwingine akasema 'hatuwezi kupata pesa mpaka nasisi tuwe na pesa ya kuweka kwenye akaunt kwahiyo yeye hana hiyo pesa.

Na wengine walitoa kauli zakufanana na hizo. Na mwisho wa siku nikapata kijana mwenzangu mmoja tu kwahiyo kigezo cha kwanza cha kuwa na kikundi cha vijana watano kikatuangusha.

Nini kifanyike ili vijana waielewe hii fursa;

- Halimashauri zitenge muda wa kukutana na vijana na kuwapatia elimu kuhusu hii mikopo na iwahakikishie kuwa mikopo ipo na wala sio uraghai kama vile baadhi ya vijana wanavyoamini.

- Serikali za mitaa iwe na orodha ya vijana wanaojitambua na ambao tayari wameshaanzia chini na hatua waliofikia wanahitaji kuwezeshwa kupitia hiyo mikopo. Hii itajenga uhakika wa marejesho ya mkopo husika.

- Serikali ianze kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja kama vile ilivyo mikopo ya chuo elimu ya juu. Hii itapelekea kijana kupambana na marejesho yake bila kuhisi kuwa akikwama yeye basi wenzie watamlipia kupitia kikundi chake. Hili lilinikwamisha baada ya kukosa vijana wenzangu ila pangekuwepo na mkopo wa mtu mmoja mmoja uenda labda ningepata mkopo.

- Serikali itoa mikopo kwa wakati. Pamekuwepo na malalamiko mikopo ya serikali haitoki kwa wakati kama mlikuwa na wazo la biashara basi mpaka wazo hilo litapitwa na wakati ila mkopo bado.

- Mikopo itolewe kwa biashara ya mtu mmoja mmoja na wala sio kwa kikundi ili kukwepa vijana kutokuaminiana. Hii miradi ya vikundi pamekuwepo na kuzurumiana sanaaaa kwa baadhi ya wanakikundi kutokuwa waaminifu kwahiyo serikali iliangalie hili.

MWISHO; Serikali itoe elimu ya mikopo ya biashara kwa vijana kama vile inavyotoa elimu kuhusu uombaji wa mikopo ya elimu ya juu. Na vijana tuchangamkie fursa hizi na kama kuna vikwazo katika upatikanaji wa hii mikopo basi ni bora tukajionee wenyewe kuliko kusikiliza habari za mitaani.
Umeandika vyema sana
Mungu akubariki sana mkuu
 
Ubarikiwe na wewe pia mkuu

Kura yako muhimu mkuu
Nilikua ofisi ya kata kwa Afisa maendeleo jamii kupata huo utaratibu changamoto zipo pande mbili mimi navyofikiria
1. Upande wa Halmashauri hautoi elimu ya kutosha juu ya hii mikopo
2.Sisi vijana pia hatupo tayali.katika kujiajiri ndo mana ulikutana Na majibu tofauti tofauti
3.Lingine hili jambo mafanikio yake yanachagizwa Na ukada wa chama kwa 50%
Maoni yangu hayo mkuu
 
1 na 2 naungana na wewe ila namba 3 sina uhakika nalo
 
Back
Top Bottom