SoC01 Mikopo ya Biashara ya Vijana Serikalini

Stories of Change - 2021 Competition

flulanga

JF-Expert Member
Jul 1, 2016
4,861
6,342
Serikali kupitia mapato ya halmashauri kumekuwepo na asilimia 10 ya mapato ya ndani kwaajili ya mikopo kwa vijana na watu wenye ulemavu.

Wimbi kubwa la vijana kulalamika ukosefu wa ajira na ukosefu wa mitaji ya biashara, kilimo na shuuri nyingine za kuwaingizia vipato hii ndio ilikuwa suluhisho endapo kama ingetumika vyema.

Kumekuwepo na habari kuhusu utoaji wa hiyo mikopo lakini uchangamfu wa vijana kujitokeza kuchangamkia fursa hiyo imekuwa ndogo. Na serikali imekuwa haitoi elimu hiyo.

Naongelea uhalisia wangu mimi kama kijana. Ishawahi kumvaa mkuu wa mkoa na akanielekeza niende kwa muhusika na namba yake nikapewa. Nilimpata muhusika na muongozo mzima alinipatia, nikarudi mtaani ili niweze kufanya kile nilichoelekezwaaa.

Niliambiwa nifanye haya;

- Niunde kikundi cha watu kuanzia wa tano,

- Tuchague uongozi wa muda,

- Tuunde katiba yetu ambayo ndio utakuwa muongozo wetu,

- Tuchague uongozi kulingana na katiba tuliyoiunda,

- Tuanzishe mradi wowote kama ni kilimo au ufugaji, au biashara, au hata kiwanda kidogo.

- Na mwisho tufungue akaunti bank.

Baada ya vyote hivyo twende kwa afisa mtendaji wa eneo letu kupitia kwa mwenyekiti wa mtaa kwaajili ya kupatiwa barua ya utambulisho twende nayo halimashauri kwaajili ya hatua nyingine zaidi.

Niliporudi mtaani ili niunde hicho kikundi cha watu kuanzia watano ndipo nilipogundua vijana wengi hawana muamko kuhusu hii mikopo ya serikali. Wengi ambao nilihisi nikiwapelekea hili wazo watalichangamkia ila kwa bahati mbaya ikawa kinyume chake. Kila mtu alitoa neno lake analolijua yeye;

Kuna mwingine alisema 'serikali haiwezi kutoa pesa zake zaidi watatupotezea muda wetu bure'

Mwingine akasema ' hiyo mikopo inatoka kimjuano'

Mwingine akasema 'hatuwezi kupata pesa mpaka nasisi tuwe na pesa ya kuweka kwenye akaunt kwahiyo yeye hana hiyo pesa.

Na wengine walitoa kauli zakufanana na hizo. Na mwisho wa siku nikapata kijana mwenzangu mmoja tu kwahiyo kigezo cha kwanza cha kuwa na kikundi cha vijana watano kikatuangusha.

Nini kifanyike ili vijana waielewe hii fursa;

- Halimashauri zitenge muda wa kukutana na vijana na kuwapatia elimu kuhusu hii mikopo na iwahakikishie kuwa mikopo ipo na wala sio uraghai kama vile baadhi ya vijana wanavyoamini.

- Serikali za mitaa iwe na orodha ya vijana wanaojitambua na ambao tayari wameshaanzia chini na hatua waliofikia wanahitaji kuwezeshwa kupitia hiyo mikopo. Hii itajenga uhakika wa marejesho ya mkopo husika.

- Serikali ianze kutoa mikopo kwa kijana mmoja mmoja kama vile ilivyo mikopo ya chuo elimu ya juu. Hii itapelekea kijana kupambana na marejesho yake bila kuhisi kuwa akikwama yeye basi wenzie watamlipia kupitia kikundi chake. Hili lilinikwamisha baada ya kukosa vijana wenzangu ila pangekuwepo na mkopo wa mtu mmoja mmoja uenda labda ningepata mkopo.

- Serikali itoa mikopo kwa wakati. Pamekuwepo na malalamiko mikopo ya serikali haitoki kwa wakati kama mlikuwa na wazo la biashara basi mpaka wazo hilo litapitwa na wakati ila mkopo bado.

- Mikopo itolewe kwa biashara ya mtu mmoja mmoja na wala sio kwa kikundi ili kukwepa vijana kutokuaminiana. Hii miradi ya vikundi pamekuwepo na kuzurumiana sanaaaa kwa baadhi ya wanakikundi kutokuwa waaminifu kwahiyo serikali iliangalie hili.

MWISHO; Serikali itoe elimu ya mikopo ya biashara kwa vijana kama vile inavyotoa elimu kuhusu uombaji wa mikopo ya elimu ya juu. Na vijana tuchangamkie fursa hizi na kama kuna vikwazo katika upatikanaji wa hii mikopo basi ni bora tukajionee wenyewe kuliko kusikiliza habari za mitaani.
 
mie ni mnufaika pia wa hii mikopo ni juzi tu tumepewa hela tuko watu sita na afisa maendeleo wetu wa kata alitupa ushirikiano mwanzo mpaka mwisho ila tulivyoona balance inasoma benki Afisa wetu alituambia turudi kwa mtendaji kuna form za kusign dooh bado nuau tughairishe kila mtu afanye mambo yake kaka wa watu akasimama kidete na sisi na hela tukaipata
 
Kwa wilaya za mijini labda ndio shida, wewe upo mjini?
 
mie ni mnufaika pia wa hii mikopo ni juzi tu tumepewa hela tuko watu sita na afisa maendeleo wetu wa kata alitupa ushirikiano mwanzo mpaka mwisho ila tulivyoona balance inasoma benki Afisa wetu alituambia turudi kwa mtendaji kuna form za kusign dooh bado nuau tughairishe kila mtu afanye mambo yake kaka wa watu akasimama kidete na sisi na hela tukaipata

Mkuu
Mi pia nahitaj kuwa mnufaikaji wa huu mkopo wa serikali vipi unaweza nisaidia japo kwa elimu mlifanyaje
Naomba unichek namba 0711633656 km hutojali
 
Halmashauri niliyopo kuna ukiritimba Sana katika kupata hii mikopo.
Bila rushwa hutoboi .
Kuna kikundi kimoja cha kina mama wameteseka Sana zaidi ya miezi sita ila walipata mkopo.
Na wamefungua mradi wa Kutengeneza sabuni.
Ukijua abc za kupata mkopo hauteseki .
Ngoja naweka mwongozo wa pdf hapa
 
mie ni mnufaika pia wa hii mikopo ni juzi tu tumepewa hela tuko watu sita na afisa maendeleo wetu wa kata alitupa ushirikiano mwanzo mpaka mwisho ila tulivyoona balance inasoma benki Afisa wetu alituambia turudi kwa mtendaji kuna form za kusign dooh bado nuau tughairishe kila mtu afanye mambo yake kaka wa watu akasimama kidete na sisi na hela tukaipata
Ilichukua muda gani kuipata
 
Ni kweli kabisa, ila mkopo wa mtu mmoja mmoja ni mtiahani sana kwa serikali...
Sheria na kanuni, bado zinafanyiwa kazi kwa mkopo wa mtu mmoja mmoja.
Wanaolalamika kuwa wanakosa wakiona, tatizo sio maombi. Maombi yakiwa mengi wapo watakaopata na watakapata. Maafisa Maendeleo ya Jamii ndiyo wanaohusika na mikopo hii. Mikopo hii, haina upendeleo.
Vijana muwe waaminifu kurejesha mkikopa
 
Ni kweli kabisa, ila mkopo wa mtu mmoja mmoja ni mtiahani sana kwa serikali...
Hili swala kinaweza kushughulikiwa na wabunge wetu .. only if vijàna Tukiwa Tunatambua nini tunahitaji , na kila tukiitwa kwenye vikao na wabunge siyo kwenda kung'aa sharubu .

Tuwe na utaratibu wa kuhoji na kutoa mapendekezo mapya namna yakutatua changamoto zetu .

Nilizungumza na mmoja wa watunga sera , alisema wanalijua hili ila lipo kimkakati zaidi .
 
Back
Top Bottom