Mikopo umiza yavunja ndoa

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Mikopo imetungiwa majina ''Kausha damu'' na ''chupi mkononi''

Wanaume wana la kujifunza hapa kwa wake zao kuhusu vikundi na wanawake kujiunga na haya madhehebu yanayochepuka kama uyoga yanayowapa watu cheo cha unabii sio mungu na kuwauzia watu mafuta ya upako na maji ya chumvi kwe bei kubwa bila kutoa kodi serikalini

sasa tuendelee...

Mikopo ya mitaani maarufu “kausha damu” imeendelea kusababisha migogoro katika familia baada ya mwanamume mmoja mkoani hapa kuamua kumuacha mke wake na kubomoa nyumba waliyokuwa wakiishi ili kumkomoa mwanamke huyo anayedaiwa Sh13 milioni.

Familia hiyo imeingia kwenye mzozo huo baada ya mwanamke kukopa fedha kwa watu tofauti na kujikuta akilimbika madeni ambayo hawezi kuyalipa, jambo hilo limemkasirisha mume wake na kuamua kubomoa nyumba waliyokuwa wakiishi.

Akizungumzia alivyoingia kwenye madeni hayo, mwanamke huyo, Agnes Gasper alisema alilazimika kukopa fedha hizo kwa sababu mume wake amekuwa akitoa fedha ndogo ya matumizi ya nyumbani ambayo haitoshelezi mahitaji, hivyo akajikuta na hali ngumu ya kimaisha.

Alisema nyumba hiyo iliyovunjwa na mume wake walijenga wote, hivyo kwa hali yoyote anayopitia, ana haki ya kuishi kwenye nyumba hiyo.

Agnes alikiri kudaiwa Sh13 milioni, hata hivyo alisema sehemu ya fedha hizo alikuwa akiwakopea watu wengine, wakiwemo rafiki zake lakini yeye alikopa Sh1.5 milioni ambazo anadai alizitumia kwenye kilimo cha mahindi.

“Ni kweli nadaiwa fedha nyingi nilizokopa kwa watu mbalimbali, ikiwemo mikopo ya ‘kausha damu’ na katika madeni hayo Sh13 milioni nilikopa kwa mama mmoja, nyingine hazikuwa zangu, sijui nitalipaje,” alisema Agnes.

Hata hivyo, alisema mbali na deni hilo, anadaiwa pia na taasisi nyingine za kifedha zilizopo mitaani kwake “kausha damu” na “chupi mkononi”.

Alisema kwa sasa hana kazi wala biashara, hivyo anaishi kwa kufanya vibarua kwenye mabanda ya mamalishe katikati ya mji.

Kwa upande wake, mume wa mdaiwa huyo, Said Mkwizu, mkazi wa Morogoro, alisema amefikia uamuzi ya kubomoa nyumba yake yenye vyumba vitatu baada ya makundi ya watu kwenda nyumbani kwake kumdai mke wake fedha zao huku mwanamke mmoja anayedai Sh13 milioni akitaka aachiwe nyumba hiyo ili asamehe deni.

Mkwizu alisema mbali na madeni anayodaiwa, mke wake ana tabia ya kutoka usiku na kurejea nyumbani asubuhi na akimuuliza anasema alikwenda kufanya vibarua kwenye mabanda ya mamalishe maeneo ya Kahumba na Msamvu.

Alisema kutokana na madeni ya mke wake, baadhi ya watu wamekuwa wakitoa vitisho kwamba watamfanyia vitendo vibaya ambavyo hatasahau, hivyo aliamua kuvunja nyumba hiyo akihofia kudhuriwa ikiwa ni pamoja na kuchomewa nyumba.“Mwenzangu halali hapa nyumbani, ikifika usiku anaoga anajipodoa na kuondoka zake, humu ndani nalala na mwanangu tu na tayari vitisho vimeshatolewa, sasa niliona bora nivunje hii nyumba ubaki uwanja, mimi nikaishi na mwanangu na yeye achukue ustaarabu wake, kiwanja hakiozi mtoto akikua atakuja kujenga mwenyewe,” alisema Mkwizu.

Alisema baada ya kuvunja nyumba hiyo amekwenda kupanga chumba kimoja ambacho anaishi na mtoto wake na anapokuwa kwenye shughuli zake za umachinga pale stendi ya mabasi ya Msamvu, huwa anamuacha kwa majirani anaowaamini.

Hata hivyo, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Lukobe iliyopo manispaa ya Morogoro, Mariam Rajabu alimpa wiki mbili kijana huyo kujenga upya nyumba hiyo ili mke wake na mtoto waweze kuishi.

Rajabu alisema licha ya madeni anayodaiwa mwanamke huyo, Mkwizu hana haki ya kuvunja nyumba kwa kuwa nyumba hiyo ni mali ya mtoto wao ambaye anasoma darasa la kwanza.

"Changamoto hizi za madeni anayodaiwa mke, zisimuathiri mtoto ambaye hana hatia. Mtoto anahitaji kuishi kwa amani na sehemu salama, kitendo cha kuvunja nyumba kimemfanya mtoto aishi kwa mashaka na katika mazingira ya utata kwa sababu sasa hivi anahifadhiwa na majirani.

“Serikali hatutakubali, huyu mtoto kwa sasa anaathirika kimwili na kisaikolojia, naagiza kama kiongozi wa Serikali mwenye mamlaka, huyu Mkwizu anatakiwa ajenge hii nyumba ndani ya wiki mbili, kama ana hasira basi anaweza kumuacha huyu mwanamke na madeni yake,” alisema.

Akizungumzia tukio hilo, kamanda wa polisi wilaya (OCD), Laurent Samson alisema kuna haja ya kuwatafuta watu na taasisi zinazomdai mwanamke huyo (Agnes) ili waweze kueleza kama wana uhalali wa kukopesha watu, ikiwemo kuwa na leseni za Benki Kuu.

Source Mwananchi
 
"Serikali hatutakubali, huyu mtoto kwa sasa anaathirika kimwili na kisaikolojia, naagiza kama kiongozi wa Serikali mwenye mamlaka, huyu Mkwizu anatakiwa ajenge hii nyumba ndani ya wiki mbili, kama ana hasira basi anaweza kumuacha huyu mwanamke na madeni yake,” alisema

Serikali haitaki watoto wateseke, ni hii ja Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
 
Kahumba tena ? Anajiuza huyo !!
Mkuu unauliza nn hapo? Huoni huyo Mke wa Jamaa anajiuza kitambooo !!.

Na anajiuza ili alipe madeni ya watu.


Ukiona mwanamke mkeo au Mpenzi, anafanya Matumizi ya Fedha ,na ukopaji wa Pesa kimya kimya bila kukushirikisha.


Mpige marufuku, akishupaza shingo achana naye.


Huwa Kuna wakati wanaweka Rehan Mali zenu ,Kwa ubinafsi wake.
 
Mtendaji wa kata anampa kijana wiki mbili awe amesimamisha nyumba ningekuwa ndio mimi ningemuuliza kama yeye anaweza

Mtendaji nae mwehu tu

Two weeks si bora uchukue hiyo hela uokoe jahazi au uitunze ujenge kwingine
 
Hawa viumbe sijui akili zao zipo wapi
Kila kukicha wanazusha mapya
Unakopa kurejesha huwezi
Hizi taasisi za kuwatetea
Iko siku zitautua
Huo mzigo
 
Back
Top Bottom