Habari zenu wakuu,
Siku ya Ijumaa ya tarehe 2/9/2011 TCU kwa kushirikiana na HESLB walitoa majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwango cha mikopo ambacho watapatiwa. Ambacho sikuweza kukielewa ni jinsi mgawanyo wa mikopo ulivyofanyika kwa sababu kwanza badala ya kuonesha kwa asilimia wao waliweka kiwango cha fedha ambacho mwanafunzi husika atapatiwa. Sasa swali langu ni kuwa je hizi fedha zilizoandikwa ni kiasi ambacho mwanafunzi atapatiwa kwa muda wote wa kipindi cha masomo atakapokuwa chuoni?? au ni kwa mwaka wa kwanza peke yake??
Kwa mfano nina mdogo wangu ambaye amechaguliwa katika kozi ambayo ada yake ni TZS 1,400,000/= kwa mwaka na ameandikwa kuwa atapatiwa mkopo wa TZS 3,995,500/=. Sasa sijaelewa kama hii fedha ni jumla ya fedha yote atakayopatiwa kwa muda wa miaka mitatu ya kozi yake au vinginevyo. Vilevile je fedha hizi zinajumuisha malipo fedha ya kujikimu na malazi?
Wakuu hapo nimekwama na kwa bahati mbaya sana jamaa wa HESLB inaonekana wako bize sana kiasi kwamba inakuwa vigumu kwa wao kujibu maswali yetu sisi wananchi tuliowaajiri.
Nawasilisha hoja.