Bibi Mikopo
Senior Member
- May 15, 2015
- 180
- 35
Wadau,
Tangu HESLB watoe majina ya wadaiwa ambao walikopeshwa na hawajaanza kulipa kumekua na kelele nyingi -- nyingi kutoka wale waliokopa na hawajawahi kulipa hata senti moja. Hatuwezi kuendelea hivi. Kelele nyingine hazina hoja kabisa, kwa mfano:
1. Mbona hatujaambiwa tunadaiwa shilingi ngapi? Wametoa majina tu. -- Uliyekopa ni wewe, ulikua na wajibu wa kwanza wa kulipa. Umeutekeleza? Umewahi kuchukua jitihada zozote za kujua unadaiwa shilingi ngapi na kwa sababu gani?
2. Eti, ninalipa kodi kwa hiyo siwezi kulipa deni hilo. -- Huu nao ni uchovu wa zama zilizopita. Kukopa harusi, kulipa matanga. Sio zama hizi. Wajibu wea msingi wa mkopaji na kulipa -- popote duniani. HESLB wawape haya majina TRA, Uhamiaji, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Chama cha Waajiri, professional bodies n.k -- wakose pa kutokea. Tuachane na siasa, mikopo irejeshwe na wengine wanufaike.
3. Eti, niliuliza deni langu mwaka juzi nikaambiwa Shs 4milioni, mwaka huu naambiwa shs 5milioni. Siwezi kulipa. -- Ulivyoambiwa ni shs 4 milioni ulifanya nini? Kama hukuanza kurejesha imekula kwako. Kuna penalti na tozo nyingine -- na hizi sio mpya -- muhimu ni kuwa pata deni lako, anza kulipa na hakikisha unapata uthibitisho kuwa umemaliza kulipa kutoka HESLB.
4. Eti, salary slips zangu zinaonyesha nilimaliza kukatwa zamani -- sasa inakuwaje naambiwa mimi mdaiwa sugu? -- Hii nayo ni siasa. Mkopaji ni wewe. Unayekatwa ni wewe. Mwajiri ni 'agent' tu. Tunawajua waajiri wetu. Ni vema kujiridhisha kuwa makato yako yanafika HESLB, NSSF, PSPF, LAPF n.k Waulizeni UDASA au wahadhiri wa SAUTI Mtwara!
5. Mimi nilishamaliza zamani, inakuwaje wananidai tena! -- Ukimaliza kulipa, HESLB wanatoa Clearance Certificate -- wewe unayo? Wadai kwa nguvu!
Mwisho, ukweli ni kwamba wabongo tulizoea business as usual kwa miaka 10 iliyopita. Ngoja twende sawa.