Mikopo Elimu ya Juu - Nini kifanyike kuiboresha?

SMU

JF-Expert Member
Feb 14, 2008
9,616
7,863
Nimeona kwenye baadni ya magazeti ya leo tume inaomba wananchi na wadau wa elimu ya juu kwa ujumla kuchangia mawazo ya namna ya kuboresha utoaji wa mikopo wa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu hapa nchini.

Naamini humu pia tumo wadau wengi, hebu tujaribu kutumia angalau dakika chache kutoa mawazo yetu hapa: Ushauri na Mapendekezo | Tume Mikopo

Basically, kuna maswali mawili:

1. Kuzingatia ongezeko la wanafunzi wengi wahitaji wa elimu ya juu, ni mambo gani yafanyike ili suala la mikopo liwe endelevu na lenye ufanisi katika uchangiaji wa elimu ya juu?

2. Una mapendekezo gani yoyote ya ziada yatakayosaidia kuboresha mfumo wa kugharimia elimu ya juu na utoaji wa mikopo?
 
1). Gharama ya elimu ya juu pia ichangiwe na wazazi/walezi kwa asilimia kulingana na uwezo wao. Kutokana na idadi ya wanafunzi wanaofikia kuhitaji elimu ya juu, serikali peke yake isiwe ndio kugharamia hii cost.
Kwa wale wasiokuwa na uwezo, basi serikali ndio itakayogharamia 100%. Lakini malipo ya mkopo uwe pale pale.

2). System ya kutoa hii mikopo iboreshwe kuhakikisha kuwa wale wanaopata huu msaada ndio wanaostahili. Adhabu kubwa iwepo kama onyo la kukiuka hii arrangement.

3). Mikopo itolewe kwa muda unaostahili. Ikiwezekana, kabla ya session ya chuo kuanza. Malipo yote yakamilike.

4). System ya kuhakikisha mikopo inalipwa na ufuatiliaji wake. Kama malipo yanapitia kwa mwajiri basi ijulikane, ni lazima mwajiri afahamishwe na mwajiriwa/serikali kuwa kuna mkopo unahitaji kulipwa. Hapa pia iwe ni kosa kukwepa hili jukumu.

5). Twende na wakati! Computer system (online) kwa mwenye mkopo ku'manage account yake online. Ikionyesha mikopo/malipo na schedule ambazo amekubaliana nayo kuhusu mkopo. Hapa anahitaji kuonyesha anapopata ajira kwa kuandika details za mwajiri, na pia anapobadirisha ajira.
Muda wote mwanafunzi ana salio la mkopo, hii system inatakiwa kuwa a MUST. Inabidi mabadiliko yoyote yanayotokea ambayo yatauhusu huo mkopo mfano: kubarika kwa contact details, simu, anuani ni lazima yawekwe kwenye system.
Kutokana na kuwepo idadi kubwa ya wenye mikopo. Iwe ni lazima, mwajiri apate details kama mwajiriwa ana mkopo au la kwa kuwepo na utaratibu wa ku'search hii system.

6). Pendekezo: mwenye mkopo. Please lipa, wadogo zako tunahitaji kupata fursa hii pia....
 
1). Gharama ya elimu ya juu pia ichangiwe na wazazi/walezi kwa asilimia kulingana na uwezo wao. Kutokana na idadi ya wanafunzi wanaofikia kuhitaji elimu ya juu, serikali peke yake isiwe ndio kugharamia hii cost.
Kwa wale wasiokuwa na uwezo, basi serikali ndio itakayogharamia 100%. Lakini malipo ya mkopo uwe pale pale.

Kama hatuna uwezo wa kupambanua kwa haki kabisa nani an uwezo na nani hana, suluhisho bora pengine ilikuwa ni kwa serikali kutoa mkopo kwa kila mwanafunzi aliyedahiliwa na anayetaka kukopa. Naamini serikali kama ikiamua kwa dhati inaweza kujenga uwezo huu wa kukopesha. Kunaweza kuwa na mikopo ya aina mbili...ile ya ada na malipo mengine yanayoendana na shule moja kwa moja na ile kwa ajili ya chakula na malazi (accomodation).

Mikopo kwa ajili ya ada itolewe kwa asilimia mia moja kufuatana na ada na gharama za chuo (vya hapa nchini tu) husika na hii inaweza kulipwa chuoni moja kwa moja lakini kwa kumshirikisha mwanafunzi mwenyewe. Lakini pia kuwe na close monitoring ya viwango ya ada zinzowekwa na vyuo husika.

Mikopo ya chakula na malazi inaweza kuwa na upper cap ya amount per day (say kama ni elfu 10 kwa siku) na ikizingatia muda wa masomo wa chuo husika (say urefu wa semester). Hii maana yake ni kuwa mwanafunzi anaweza kukopa kiasi chochote kisichozidi elfu 10.

Katika kulipa pia wangeweka grace period ya say miaka mitatu bila riba lakini ikizidi hapo unaanza kulipa na riba. Hili likienda sambamba na kuweka utaratibu ambao utalazimisha watu kulipa mikopo.

Pia ni vema kuanza kuwajenga wanafunzi mapema ili waone umuhimu wa kukopa, umuhimu wa kutumia mikopo vizuri na umuhimu wa kulipa mikopo kwa wakati. Hili litasadia wanafunzi kulipa mikopo mapema baada ya kumaliza vyuo ili wengine pia waweze kukopa.
 
..............

Basically, kuna maswali mawili:

1. Kuzingatia ongezeko la wanafunzi wengi wahitaji wa elimu ya juu, ni mambo gani yafanyike ili suala la mikopo liwe endelevu na lenye ufanisi katika uchangiaji wa elimu ya juu?

2. Una mapendekezo gani yoyote ya ziada yatakayosaidia kuboresha mfumo wa kugharimia elimu ya juu na utoaji wa mikopo?

Mkuu aksante sana nadhani kuna zaidi ya maswali mawili wakitaka kupata mawazo endelevu

Kwanz kwa kutumia taaluma yangu ICT( System development) Mpaka wanaleta hii request ina maana kuna problem

Na problem inatakiwa kuwa identified ili kubaisnisha true probmle form effect of the poblem.

Kwa kuwa binafsi sijafanya analysis na sina detail na data za kutosha nitachambua kijuu juu but inaweza kuwapa mwanga wale wenye data au kupata data kufikia maamuzi sahihi ya kutatua tatizo halisi

Wote tunakubalina kuwa finacial resources zilizopo haziwezi kutosheleza maombi yote na kukidhi kila mtu.

Kwa hiyo siyo sahihi kuhusanisha tatizo hili na kuongezeka idadi ya wanafunzi . Tunataka wanafunzi wawe wengi hilo sio tatizo . tatizo au issue iliyopo ni ni vipi pesa iliyo buddget igawanywe kwa wanafunzi hawa wengi. SO tatizo ni ufinyu wa bajeti na kuigawa hiyo bajeti kwa wanfuzi

  • Option A
Ni kusema kama bajeti ya kukopesha wanafuzni ni shilingi 1000 na wanafuzi waliokidhi vigezo wakomba elfu moja basi kila mwnafunzi apewe shilingi moja. hii sio endelevu


  • Option B
Ni kuweka vigezo vya kimkoa au kiwilaya walipo wazazi au walezi wa wanafunzi. Au shule wanayotoka wanafunzi. Mfano mwanafuzi aliyemaliza mtwara , Kigoma, Kasulu sekondary. tamazidi mwanafunzi aliyemaliza Tambaza, Mwanza Sekondary, Arusha Sekondary na shule za mjini

Mfano huu natoa najua hata serikali mfanyakazi anaposafiri kwenda baadhi y mikoa anapewa perdiem ndogo wakati akained amikoa mingine anapewa perdiem kubwa.


  • Option C
Ni ifanyike classifcation ya shule za A walizotoka wanafuzi. Mwanafunzi alitoka mzizima Sekondary huyo anaweza kuwa ni Class D. Aaliyemaliza tambaza anaweza kuwa Class C. Aliyemaliza mwanerumango huyo anaweza kuwa Class A kwenye Mkopo.

Kwa kuwa wanafuzi wametengwa katika makundi kwa ile bajeti ya shilingi 1000 bodi itaamua kwa kuwa kuna wanfuzi 1000 basi wale wa Class A watapewa mkompo wa shilingi 2. na wale wa Class D watapewa mkopo wa shilingi 1.

So kufanya hiyo kitu iwe endelevu inawezekana zikipatikna data na wakipatikana analyst wa kuzichambua na kuzifanyia kazi.

Kuna mambo mengi yakujua kabla ya kutaka ushauri wenye akili kama hizi option nimeweka hapa ni chache.

  • Kujua bajeti ya Bodi kwa mwaka na kwa may be miaka mitano ijayo
  • Kujua idadi ya wanafuzi kwa mwaka na trend ya kuongezeka kwao
  • Kujau kiasi cha mikopo inayolipwa na wale waliomaliza
  • Kujau idadi ya vyuo vinavyokubalika na bodi , vilipo, kiwango cha maisha mikoa vilipo vyuo hivyo ?
Simply kwangu naona vinatakiwa vitengenzwe vigezo au wanafuzi watengwe kwenye makundi. Zikipatina data zote wachambuzi ndo wanwezza kushauri ni makundi mngapi au vigezo gani vitumike.
 
Back
Top Bottom