TANZIA Mikola Mahiga afariki dunia kwa ajali ya gari nchini Uswisi. Ni mtoto wa kwanza wa Marehemu Augustine Mahiga

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525
Mtoto wa kwanza wa marehemu Balozi Augustine Mahiga aitwaye Mikola Mahiga, maarufu kama "Mike" amefariki dunia kwa ajali ya gari huko Geneva, Uswiss alipokuwa akifanya kazi katika Taasisi mbalimbali za Kifedha na Masoko ya Mitaji akiwakilisha nchi kadhaa za Asia na Afrika.

mahiga.JPG

Mikola Mahiga

Chanzo: Milard Ayo (Twitter )
 
Watoto wa vigogo wanakuwaga na kazi nzuri nzuri. RIP

Ndiyo inavyokuwa! Siku zote kila mtu hula kwa urefu wa kamba yake. Huwezi kumkuta mtoto wa kigogo kwenye shule ya kata akifundisha! Huko utawakuta watoto wa maskini pekee!

Hao mara zote utawakuta kwenye ofisi zenye viyoyozi tu! Hata wawe na ufaulu hafifu kiasi gani!

Namtakia pumziko la milele.
 
Acha uongo yani uwe na uwezo mdogo alafu ufanye kazi kwenye taasisi kubwa nje?
 
Watoto wa vigogo wanakuwaga na kazi nzuri nzuri. RIP
Wengi ni losers tu, we angalia lemutuz na washkaji kibao waliopelekwa ulaya enzi zile… sasa hivi wachovu tu!!

ILA hao unaowaona wanapata ni Kwa sababu Muda wao kwenye majungu na kulalamika ni Mdogo sana… they work hard, study hard and do justice to advantage waliyopewa na Mungu

Sio kama mimi na wewe kutwa kulalama tu
 
Pengine kuna wakati angekuja kugombea ubunge au kupewa ugavana. Wenyewe wanasema kuwa kwenye system. HONGERA NA ASANTE BWANA MUNGU .chonde Chonde kama kifo kibaya alaumiwe mungu huu ni mtizamo wangu tu wa chuki.
 
Back
Top Bottom