Mikataba ya madini , gesi mafuta yafaa iwe hivi

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
Mh Rais mie nafaikiri unajiongezea mzigo mkubwa sana kuingia mikataba na kuanza ku monitor ulipaji wakodi. Na hiyo kodi ili upate lazima ipite mikononi mwa wezi wengi wanaoinyemelea, na ukishaipata remants baada ya kupigwa ndiyo unakuja kujenga barabara kiduchu ama reli kiduchu. Binafsi nafikiri mikataba ingekuwa imeandikwa karatasi mbili tu na iwe hivi:

Chukua Gesi mtwara kadri ya uwezavyo ktk vitalu kadha wa kadha, ila nijengee mitambo ya umeme (neuclear) na miundo ya usambazi inayotoa umeme wa kutosha kuendesha nchi zote hizi za SADC.

Mwingine chukua Tanzanite unavyotaka ktk vitalu kadhaa wa kadhaa, nijengee reli na treni ya umeme inayounganisha mikoa yote ya Tanzania na nchi jirani.

Wewe chukua Bulyakulu chimba peleka hata visuguu unakojua, ila nijengee bandari kabambe ktk miji kumi kadhaa wa kadhaa.

Mwingine chukua geita mining, ila nijengee viwanja vya ndege vya uhakika 10 kila kanda kiwanja kikubwa cha kutosha.

Mwingine, wewe chukua Buzwag nijengee miundo mbinu ya elimu kote nchini na iwe ktk shape nzuri.
Ukimaliza hayo, shusha tax bandari zote hadi iwe single digit, na cooperate tax ya makampuni iwe hadi 5%. Fanya pia namna interest za bank ziwe maximum 9%. Ukifanya hivi naamini tutapiga maendeleo haraka sana, na hutaangaika sana kuchungulia bandarini na wizi mwingine.

Ukifanya hivi kodi kubwa sana itaiingia zaidi ya trillion 500 kwa mwaka, na wala hutakuwa na haja ya kukimbizana na wafanyakazi kuripa kodi ama hawa wafanya biashara wadogo wadogo.
 
Bandarini wala hakuna haja ya kutafuta sijui nchi jirani sijui nani wa kupitisha mizigo, cha kufanya pale ufanye ni mass market.
Shusha kodi bandarini mpaka 8%, mtanzania anunue gari kwa bei ya milion 4, hiyo gari aiuze uganda, rwanda, burundi , zambia kwa milion 20. Hapo kila mtanzania unamuongzea purchasing power, na mizigo yote inapita hapa Tanzania yani principally unaua bandari zingine zote za nchi jirani.

NJia ni rahisi kama hatuwezi export bidhaa zetu kuingiza dola kama import, fanya vifaa vije kirahisi kwa kodi rahisi pale bandarini, harafu mnaviuza nchi zingine hivyo vitu hapo mnakuwa kama mna export bidhaa zenu na dola zinaiingia kama tume export vile bidhaa zetu, kumbe kiuhalisia tumekuwa ma middle men tu. Tukajifunze Dubai waliweza je kuwa free port na wakatengeza fedha nyingi kuliko walivyokuwa watoza kodi kubwa.
 
a"
 
Attachments

  • IMG-20170402-WA0009.jpg
    IMG-20170402-WA0009.jpg
    106.8 KB · Views: 39
Nakupongeza kwa hii ni principle ya biashara inayofanya kazi mahali popote duniani. Miaka kadhaa niliisoma kwenye Masters of International Business MIB
Either unakusanya kodi kidogo kutoka kwenye mizigo michache.
Au unakusanya kodi nafuu kutoka kwenye mizigo mingi itayoleta yafuatayo
1.nafasi nyingi za ajira
2.mapato makubwa
3.hali nzuri ya kiuchumi kwa raia wako
4.kukuza viwanda
5.kuboresha miundombinu

Mkuu ni kweli kabisa.
Tatizo binafsi naliona, nafikiri watunga sheria hizi za mapato na uchumi wanajikita zaidi kutumia zile theory za vitabuni sana bila kwendana na reality on the ground. Tunakuwa bogged down ktk uchumi kwa kutumia sheria ama kanuni ambazo ziko very rigid, na wenda zinakuwa si muafaka sana kutumika kwa wakati huo.

Lazima tufike mahala tukubaliane ya kwamba kutoza kodi kubwa yani rate kubwa haisaidii ktk kuujenga uchumi, bali inaubomoa bomoa uchumi wa nchi husika. Na pia inatengeneza jamii ama inawalazimisha wananchi kutoa rushwa ama kuwa wajanja wajanja wakwepaji wakutoa kodi.

Fikiri umenunua gari la milion 100, na unaambiwa kodi kwa ujumla ni milioni 100 ama zaidi. Huyu mtu hata kama ni mlokole, wenda atapitiwa na kashetani kutafuta namna ya kuikwepa kutoa hiyo kodi. Rais mwenyewe amejionea, pale bandarini watu kwenye kontena wameweka mitumba badala ya gari.

Toza kodi ndogo bandarini atmost 8% ili watanzania waweze ku participate ktk ujenzi wa uchumi kwa kuagiza vifaa kutoka nje na wao kuviuza nchi zinazotuguka. Fanya Tanzania kuwa HUB ya kwamba Mzambia, mcongo mlawi anaona hakuna haja ya kununua vitu kutoka Japan badala yake inavinunua Tanzania.

Ukifanya hivyo na ukapata Watanzania milion 10, na wakawa wanalipa kodi kwa wastani wa milion 2 tu kwa mwezi kungiza pale bandarini, maana yake unapata trilion 2 kwa mwezi. Na wakisha viuza tena hivyo vifaa nchi jirani unakuwa ume export unapata tena trion 2 zingine. Lakini kinyume chake, weka import % kubwa bandarini, utapata watu mia moja na hata wakilipa milion 100 kwa mwezi utapata bilion 100 tu kwa mwezi. Na vile vile, wananchi wengi wanakuwa hawashiriki ktk ujenzi wa uchumi na wanabaki kwa dimbwi la umasikini.
 
Nafikri ni wakati muafaka wa kuipa serikali mawazo mbadala ili wenda watabadili namna ya kupambana na uchumi wa dunia hii mpya kwa njia tofauti.

Kulipisha kodi kubwa maana yake ni kubomoa uchumi wa nchi na kisha unawa train wananchi wako mwenyewe kukwepa kulipa kodi, na hiyo training ndiyo zao la rushwa. Hivyo, ktk ku handle hizi kodi unakuwa ume handle mambo mengi sana na rushwa ikiwemo.

Ndivyo hivyo kwa mikataba hakuna haja sana ya kuingia mikataba ili walipe kodi na kisha tuje tujenge miundo mbinu. Tumeshaelewa malengo yetu ni kwa mfano kujenga miundo mbinu basi hakuna haja ya kumwambia alipe kodi, hyo process iwe transformed juu kwa juu kwa kuibadili hayo madini na kuyaleta ktk services charge hapo ndo tutapata kodi nzuri.
 
uko vizuri yote yanawezekana.
Ingawa lazima muwekezaji achunguze aone kama deal inalipa au itakula kwake au kwetu...
 
Harvard graduate aliiweka siri kubwa for a reason....JPM anajaribu kuamsha mashetani yaliyolala....makosa yalifanywa toka enzi zile za watangulizi wake
 
Harvard graduate aliiweka siri kubwa for a reason....JPM anajaribu kuamsha mashetani yaliyolala....makosa yalifanywa toka enzi zile za watangulizi wake

Mkuu
Uko sawa kabisa, basi tufanye jitihada za kuwaambia namna ambavyo wakati ule ilipaswa na sasa ni cha paswa kufanyika. Maana hata kama wasiposikiliza mawazo mema na ya dhati humuingia mtu hata mhusika asipokubaliana nayo. Yatakuwa yanazunguruka tu ndani ya masikio mpaka ataamua kuyafanyia kazi.
 
Mh Rais mie nafaikiri unajiongezea mzigo mkubwa sana kuingia mikataba na kuanza ku monitor ulipaji wakodi. Na hiyo kodi ili upate lazima ipite mikononi mwa wezi wengi wanaoinyemelea, na ukishaipata remants baada ya kupigwa ndiyo unakuja kujenga barabara kiduchu ama reli kiduchu. Binafsi nafikiri mikataba ingekuwa imeandikwa karatasi mbili tu na iwe hivi:

Chukua Gesi mtwara kadri ya uwezavyo ktk vitalu kadha wa kadha, ila nijengee mitambo ya umeme (neuclear) na miundo ya usambazi inayotoa umeme wa kutosha kuendesha nchi zote hizi za SADC.

Mwingine chukua Tanzanite unavyotaka ktk vitalu kadhaa wa kadhaa, nijengee reli na treni ya umeme inayounganisha mikoa yote ya Tanzania na nchi jirani.

Wewe chukua Bulyakulu chimba peleka hata visuguu unakojua, ila nijengee bandari kabambe ktk miji kumi kadhaa wa kadhaa.

Mwingine chukua geita mining, ila nijengee viwanja vya ndege vya uhakika 10 kila kanda kiwanja kikubwa cha kutosha.

Mwingine, wewe chukua Buzwag nijengee miundo mbinu ya elimu kote nchini na iwe ktk shape nzuri.
Ukimaliza hayo, shusha tax bandari zote hadi iwe single digit, na cooperate tax ya makampuni iwe hadi 5%. Fanya pia namna interest za bank ziwe maximum 9%. Ukifanya hivi naamini tutapiga maendeleo haraka sana, na hutaangaika sana kuchungulia bandarini na wizi mwingine.

Ukifanya hivi kodi kubwa sana itaiingia zaidi ya trillion 500 kwa mwaka, na wala hutakuwa na haja ya kukimbizana na wafanyakazi kuripa kodi ama hawa wafanya biashara wadogo wadogo.

Unafikiri Maisha ni rahisi kihivyo? Kama ingekuwa hivyo si Dunia nzima ingekuwa ni first World countries tupu? Au unafikiri Tanzania ndiyo peke yetu tuna hizo Rasilimali? Kila nchi ina Rasilimali hapa Afrika na Dunia nzima tena nyingi tu, hatuna upekee wowote ule!
 
JPM ni Kwa mara ya kwanza kama kiongozi anathubutu kuhoji watanzania wanapata nini. Lawyer wa Harvard hakuujua huo msamiati
 
Back
Top Bottom