Mikasa ya kusisimuwa Jini Mahaba linanitesa!-6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikasa ya kusisimuwa Jini Mahaba linanitesa!-6

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Oct 11, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Nilimwambia sikuwa na tatizo la kwenda kwao isipokuwa aniwezeshe kimaisha ili nami niwe na maisha mazuri, akaniambia jambo hilo liliwezekana nisiwe na wasiwasi.

  Maimuna aliniambia licha ya kuwa na uwezo wa kunifanya niwe tajiri mkubwa ninayeheshimika, hatofanya hivyo isipokuwa atahakikisha napata riziki yangu ya kila siku bila matatizo.

  Baada ya kuongea naye kwa muda aliniaga na kuahidi kuja kunichukua ili nikakufahamu nyumbani kwao kabla ya kufunga naye ndoa kisha akatoweka kwa kupitia kwenye pembe ya nyumba.

  Maimuna alipoondoka, nilijilaza kitandani na kutafakari hatima ya maisha yangu itakuwaje baada ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na jini huyo. Nilipomamka sikumsimulia mama habari za jini huyo ndipo nilijiandaa na kwenda shuleni, nikiwa shuleni sikuwa na raha badala yake nilitumia muda mwingi nikimtafakari jini Maimuna.

  Kama ilivyokawaida ya vijana kuwa na wapenzi, nami nilitokea kumpenda sana msichana mmoja tuliyekuwa tunasoma naye ambapo nilimtongoza na kumweleza nia yangu ya kumuoa mara tutakapohitimu masomo.

  Msichana huyo ambaye alikuwa akiishi na bibi yake alinipenda sana, lakini hatukuwahi kufanya mapenzi licha ya mara kwa mara kuwa karibu. Kutokana na ukaribu wetu, sikuona sababu za kumficha habari za jini aliyekuwa akinisumbua ndipo siku moja baada ya kutoka shuleni nilimweleza habari za Maimuna.

  Mpenzi wangu huyo alistaajabu sana ndipo alikwenda kumfahamisha bibi yake, baada ya kupita siku kadhaa bibi yake aliniita na kuniambia angenifanyia dawa ambayo ingemkimbiza jini huyo.

  Nilipoelezwa hivyo nilifurahi kwani nilihitaji sana kubaki huru, nikiwa kwa bibi huyo ambaye alikuwa akielewa tiba za asili alitengeneza hirizi kubwa nyeusi akanivalisha katika mkono wangu wa kushoto. Baada ya kunivalisha alinieleza nisiivue hata siku moja wala nisimuoneshe mtu yeyeto na kusisitiza kwenda kinyume na maagizo yake ningempa nafasi jini huyo kuendelea kunisumbua.

  Niliporudi nyumbani sikumfahamisha mama kama nilifungwa hirizi katika mkono wangu, usiku ulipoingia nilianza kuumwa kichwa pamoja na mwili wote.

  Ukiacha maumivu ya sehemu hizo, niliishiwa nguvu ndipo mama alinitafuta dawa za malaria nikameza. Licha ya kutumia dawa hizo hali yangu ilizidi kuwa mbaya.

  Kutokana na hali hiyo, nilikaa nyumbani siku tatu bila kuhudhuria shuleni na sikuthubutu kuvua shati kwa kuhofia mama angeiona hirizi niliyofungwa na bibi wa mpenzi wangu.

  Siku ya nne nikiwa nimezoofu mama aliingia chumbani kwangu na kuniona nikiwa nimefungwa hirizi, alipigwa butwaa na kuniuliza niliitoa wapi ndipo nilimweleza ukweli.

  Mama alikasirika sana na kusema ndiyo iliyokuwa ikisababisha maradhi yaliyonisumbua, aliikata na kwenda kuichoma moto.

  Muda mfupi baada ya kufunguliwa hirizi hiyo, nilipata nafuu ndipo mama alimfuata yule bibi na kumuuliza sababu za kunifunga hirizi bila idhini yake.

  Kwa kuwa mama alichukizwa sana na kitendo hicho, ulizuka ugomvi mkubwa katika yake na yule bibi ambapo alimuonya kutorudia tena mchezo huo.

  Tangu siku hiyo yule bibi na mama hawakuelewana, ambapo mama alinionya nisiendelee kuwa na uhusiano na mjukuu wake.

  Kwa kuwa nilikuwa nampenda sana nilikubali mdomoni lakini moyoni nilipanga kutomuacha msichana huyo, sikuwa tayari kumpoteza kirahisi.

  Usiku wa siku hiyo nikiwa nimelala, nilisikia sauti nzuri ya msichana akiimba wimbo wa kihindi Nikiwa najiuliza msichana huyo alikuwa nani ndipo nilishangaa kumuona Maimuna akiwa amesimama pembeni ya kitanda changu.

  Jini huyo aliyekuwa amependeza sana na kunukia manukato mazuri alinisababi kwa kusema; "Asalam alaykhm?" Nikaitikia; "Alaykhum salamu!"

  Itaendelea wiki ijayo,usikose.
  Baada ya salamu alinipa pole kwa kuumwa kisha alinieleza kila kitu kuhusu yule bibi aliyenifunga hirizi na kuniambia kwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kumfukuza yeye angemtambua.

  Maimuna alinionya niache kujihusisha na yule msichana wangu, kwa kuwa nilikuwa nampenda sana binti huyo nilimwambia ingekuwa vigumu kumuacha.

  Jini huyo aliniuliza ugumu ulikuwa wapi,nikamwambia wenzangu wote walikuwa na wapenzi wao sasa ningeishije bila kuwa na mpenzi ndipo alinieleza alikuwepo yeye.

  Nilimwambia yeye hakuwa binadamu wa kawaida hivyo ingekuwa vigumu kuwa naye wakati wote tofauti na mpenzi wangu ambaye tuliishi jirani.

  Maimuna alisisitiza niachane na msichana huyo lakini niligoma ndipo alinieleza nitaona, nilipomuuliza alimaanisha nini alisema nisubiri kushuhudia ambacho angemfanya.
  Itaendelea wiki ijayo.
   
Loading...