Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA KWANZA - Sehemu ya 5.


Inaendelea.............




Yule Mtoto wa nzee Mniko alifika pale nyumbani ilikuwa mida ya saa 9 kuelekea saa 10 jioni maana wakati anafika mimi sikuwepo, nilienda kufata maziwa,kuna mji haukuwa mbali sana na hapo nyumbani kwetu ambao tulikuwa tukifata maziwa ya ng'ombe kwa ajili ya matumizi ya hapo nyumbani ikiwemo chai,sasa wakati narudi ndiyo nikamkuta hapo nyumbani,alikuwa keshaanza kuwasimulia dada zangu masahibu yaliyompata mzee Mniko.Kwa mujibu wa huyo kijana wa mzee Mniko,alisema mzee wao alifika nyumbani akiwa na hasira sana siku hiyo na haikuwa kawaida yake,sasa baada ya kuwa amesalimia hapo nyumbani ilibidi awaage akawaambia anakwenda kununua miwa kwa ajili ya kwenda kuuza,Eziekel akaendelea kusema kwamba,mara nyingi huyo mzee Mniko anapo kuwa ametoka hapo nyumbani kwa shughuli ya ulinzi usiku, kazi ambayo huwa anaifanya siku zote ni uuzaji wa miwa na anasema ndiyo ilikuwa ikiwaweka mjini yeye na ndugu zake(wadogo zake).

Sasa Ezekiel anasema kwa mujibu wa mashuhuda ni kwamba baada ya yule mzee kuwa ameshachukua ile miwa na kuifunga na kamba akijiandaa kuondoka,wakati amebeba ile miwa akivuka barabara unaambiwa pale pale mzee alishtuka yuko chini akiwa nyang'anyang'a kwani aligongwa na gari iliyokuwa spidi kali sana,Kwa wenyeji wa Tarime nadhani watakuwa wanaielewa ile njia inayoelekea Sirari inayopitia nje ya mji,Pale Tarime ukiwa unatokea Musoma kama unataka kwenda Sirari si lazima upite mjini,kuna njia ilikuwa inapitia nje ya mji huko mto Msati,Sasa huko ndiyo yule mzee Mniko alipogongwa na gari mpaka kifo chake.


Kiukweli zile taarifa zilituhuzunisha sana maana masaa machache yaliyopita tulikuwa na mzee hapo nyumbani lakini sasa hivi tunaambiwa habari za kifo chake!,Kila mtu alibaki anashangaa,nakumbuka yule dada yangu niliyekuwa nikimfuatia alilia sana hasa ukizingatia alikuwa akimpenda sana yule mzee na alishamzoea!,kwahiyo Ezekiel alikuja kutoa taarifa pia akasema kama kuna pesa ambayo mzee wake alikuwa akidai basi apewe kwa ajili ya kwenda kufanyia msiba.Dada yetu mkubwa ilibidi aondoke na Ezekiel wakaenda mpaka zilipokuwa ofisi za kampuni ya mama, kuna mama mmoja alikuwa ni mhazini wa ile kampuni,mama aliwahi kutueleza kwamba kama kutakuwa na shida ya aina yeyote basi tuwe tunaenda kumwona yule mama,tulikuwaga tunamuita mama mdogo lakini yeye aliitwa mama Bona maana alikuwa na binti akiitwa Bona,basi baada y dada yetu mkubwa kufika kule hata akili pia zilifunguka kwani alimpigia mama simu akamueleza visa vilivyotokea toka siku ya kwanza mpaka muda huo,kwa mujibu wa maelezo ya dada,mama alikuwa amesema angekuja haraka iwezekanavyo.

Basi mama akawa ameelekeza kwamba huyo Ezekiel apewe pesa ya mzee aliyokuwa akidai,Ila mama alimzuia dada yetu mkubwa asiende msibani abaki na sisi hapo nyumbani,dada alivyorudi nyumbani alitueleza kila kitu kilivyoendelea huko.Kuanzia huo usiku hali haikuwa nzuri maana ukizingatia nje hakukuwa na mlinzi na ndani pia roho hazijatulia,sasa kila mtu aliwaza kivyake,yawezekana mzee Mniko alivyosema jioni angerudi asimkute dada Ashura pengine aliuliwa kabla ya kutekeleza adhma yake,au wakati anavuka barabara alikuwa na mawazo na alishindwa kuangalia kulia na kushoto ndiyo maana akagongwa na gari!,nilibaki na mawazo kichwani yasiyoisha!.

Asubuhi kulivyo kucha yule mama Bona alikuja pale nyumbani kwa ajili ya kutujulia hali,nadhani mama alimwambia aje atuangalie,alipofika pale nyumbani baada ya kusalimiana naye alituita wote sebuleni kwa ajili ya kufanya maombi,huyu mama alikuwa mlokole,hivyo alipenda sana kuomba,na huu ulikuwa utaratibu wake kila alipokuwa akitutembelea lazima afanye maombi ndiyo aondoke,hata wazazi wangu walishamzoea hivyo!,basi maombi yakaanza,muda huo dada Ashura yupo chumbani kwake maana yeye na maombi ilikuwa kama Paka na Panya!.Baada ya maombi mama Bona alimwachia dada yetu mkubwa hela na kuna maelezo alimpatia.Ilipofika mida ya saa 9 alasiri tulisikia mtu analia chumbani kwa dada Ashura kwa kigugumizi,ilibidi dada zangu waende wakaangalie.

Kumbe alikuwa dada Ashura akilia na inaonekana alianza kulia tangu zamani maana macho yalikuwa mekundu,alikuwa kavimba uso mpaka umekuwa mwekundu sana ukizingatia namna alivyokuwa mweupe!,nikaanza kusikia anamwambia dada mkubwa "Kwanini mnataka kuniua?" .

Kila mtu alipigwa na butwaa,ndipo dada yangu mkubwa akamuuliza "kina nani wanataka kukuua Ashura?".

Akamjibu akasema "Yaelekea una kiburi sana,basi utafurahi na roho yako".

Hayo maneno kiukweli yalimfadhaisha sana dada yangu ukizingatia alikuwaga ni mpole asiyekuwa na makuu na mtu.

Akarudia akamwambia "Unakumbuka siku baba na mama yangu walipokuja hapa nyumbani walikuambia nini?".

Dada akajibu "Ndiyo,nakumbuka".

Akamuuliza "Sasa kama unakumbuka wewe umefanya nini?".

Labda tu niwakumbushe,mnakumbuka hapo nyuma nilisema kwamba baada ya hao aliyowaita wazazi wake kuja kuna sauti ya kiume ilisikika na kuna mambo walimueleza dada yangu mkubwa?,miongoni mwa mambo au masharti hayo aliambiwa,itakapofika ijumaa ya wiki hiyo ambayo walikuwa wamekuja aache kufanya anavyofanyaga vinginevyo angepotezwa vibaya,sasa kumbe dada yangu kule ndani kwake huwaga alikuwa akisoma Maandiko Matakatifu na kumuomba Mungu,na kila Ijumaa alikuwa akifunga na kuomba,sasa kumbe dada Ashura na hao wazazi wake walikuwa hawapendi ile hali,sasa kumbe kipindi tunafanya pale maombi na mama Bona,dada yetu alijisahau na alishaonywa!.

Ashura alimwambia "wewe wazazi wangu wameweka nadhiri kwako na vile ulivyofanya unataka kuniua,mimi sitakufa ila usipokuwa makini utatangulia kwanza wewe maana yaelekea unadharau kiapo!"

Dada alimwomba msamaha dada Ashura lakini alikuwa amefura kama chura aliyemeza kinyonga!.Basi baada ya ukimya kadhaa Ashura alimwambia "usirudie tena!".

Baada ya hilo tukio kila mtu aliendelea na mambo yake,mimi nilitoka nikaenda kucheza mpira maeneo ya jirani na niliporudi nyumbani kama kawaida nikaingia kuoga na usiku ulipofika kila mtu alifanya analojua yeye,wa kuangalia luninga alibaki kwenye luninga nawa kwenda kulala alienda kulala,usiku huo ulikuwa mrefu sana maana zilisikika milio ya ndege wa ajabu hapo nyumbani na mauzauza yasiyoisha.Dada mkubwa usiku huo akaenda kuoga,mara ghafla tulisikia alitoka bafuni amekurupuka akipiga mayowe!,kila mtu alishituka,mimi ilibidi nitoke chumbani kwangu kuelekea sebuleni nikamkuta dada akishangaa,kwa mujibu wa maelezo yake ni Kwamba wakati anaoga alipigwa viboko vya mgongo na mtu asiyemuona!.

Mimi kwasababu akili zilikuwa bado za kitoto ilibidi nianze kucheka,nimecheka sana mpaka machozi yakawa yananitoka,japo nilikuwa namuhurumia lakini sikuacha kucheka!,ndipo dada Ashura alitoka chumbani kwake na kuuliza "kuna nini?".

Dada alimsimulia kila kitu ndipo akamwambia "Niliwaambia mkitaka kuoga mchukue sabuni yangu lakini inaonekana mna viburi,mtakoma".

Ilibidi kila mtu aelekee kulala na kiukweli sidhani kama dada yangu alioga tena, baada ya siku mbili mbele mama yangu alifika kutoka safari.


Itaendelea.....................
Aisee huyo Ashura mimi ningeenda naye sambamba
Ningeongeza ratiba na Muda wa kuomba..ningeomba sana na nisingefwata masharti yake tuone nani mjanja.
 
Mkuu LwandaMagere ,nadhani ile dawa ya bakora za kimkakati ya mzee Chibaronda bado utakuwa nayo hata baada ya kumpokea Yesu maana sikuona mahala popote kama inahusiana na nguvu za giza ulizokuwa nazo bali ni mitishamba ya kawaida tu. Kama niko sahihi,tangaza biashara hiyo utauza kuliko nakala za kitabu mkuu.
Ni wazo tu lakini.
Wewe sasa unataka kumpoteza mwenzio.
Hiyo dawa inahamasisha uzinzi na uzinzi ni dhambi...
Jamaa muache auze tu vitabu kuponya nafsi za watu..hayo ya dawa mbona watu wapo wengi sana wanauza,anayetaka akatafute huko.
 
Wewe sasa unataka kumpoteza mwenzio.
Hiyo dawa inahamasisha uzinzi na uzinzi ni dhambi...
Jamaa muache auze tu vitabu kuponya nafsi za watu..hayo ya dawa mbona watu wapo wengi sana wanauza,anayetaka akatafute huko.
Uzinzi tunafanya Sana. Hiyo dawa inaweza kurudisha heshima nyumbani
 
Uzinzi tunafanya Sana. Hiyo dawa inaweza kurudisha heshima nyumbani
Mbona watu wengi sana wanaziuza hizo dawa
Kwani umekosa huko?
Kwahiyo kama uzinzi watu wanafanya..ndiyo iwe sababu ya yeye kuuza hizo dawa?
Msitake kumrudisha mwenzenu kwenye uovu ili hali alishatoka huko.

Mungu atampa biashara nzuri halali ya kufanya na mambo yake yatakuwa sawa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom