Mikakati ya Serikali kwa maendeleo

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,219
6,650
Kwa miaka mingi, na hata kwa sasa, Serikali imekuwa na mikakati ya kuondoa/kupunguza umaskini km MKUKUTA. LAKINI! Hadi leo kiwango cha umaskini bado hakijabadilika. Tunachoshudia ni juhudi za Setikali kushughulikia Maskini badala ya UMASKINI.

Mifano iko mingi:
︎ Wakulima wa vijijini hadi leo zaidi ya ¾ bado wanatumia jembe la mkono;
︎ Zaidi ya ⅝ ya Wavuvi wanatumia mashua za kasia na tanga;
︎ Zaidi ya ⅘ ya mazao yanasafirishwa nje pasipo kuongezewa thamani;
︎ Wafugaji wengi (⅞) bado wana mifugo mingi inayotegemea maeneo ya malisho kiasi cha kuendelea kuwepo kwa migogoro na Wakulima au Hifadhi za Taifa (km Ngorongoro);
︎ Karibu Waajiriwa wengi wanaishi kwa mshahara usiokidhi mahitaji yao; na
︎ Iko mifano mingi iliyomo kwenye bajeti ya Serikali 2022/23 inayomlenga "Maskini" badala ya "Umaskini"

Kwa tafsiri ya fupi "Umaskini" ni kutokuwa na fedha za kutosha ili kutosheleza mahitaji ya msingi ikiwa ni pamoja na chakula, mavazi na makazi. Hata hivyo, umaskini ni zaidi ya kutokuwa na fedha za kutosha. Shirika la Benki ya Dunia linatafsiri "Umaskini ni njaa".

"Maskini" ni mtu au jamii iliyo na kiwango cha chini cha rasilimali fedha na muhimu kwa maisha. Tafsiri hiyo ina maaana kuwa kiwango cha mapato yake (Maskini) ni kidogo sana kiasi kwamba mahitaji ya msingi ya binadamu hayawezi kutimizwa.

Kwa Tafsiri hizo, Tanzania, kwa mfano, haina Sera muhimu za kilimo ili kutimiza mahitaji ya nchi. Msaada unaotolewa kwa Wakulima mara nyingi hausaidi kulinda usalama wa chakula na kuongeza mapato ya Taifa. Hii wakati mwingine husabibisha Wakulima wengi kuingia katika umaskini zaidi kiasi cha kushindwa kupata mahitaji muhimu ya maisha yao.

Kwa mfano, Bajeti ya Serikali 2022/23 kwenye Sekta ya Kilimo imetenga shilingi bilioni 954 kutoka bilioni 254 (bajeti ya 2021/22) kwa lengo la kuongeza ajira milioni 3 kwa vijana na wanawake.

Fedha hiyo itatumika katika miradi ya umwagiliaji na ruzuku kwa viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo. Lengo hilo halilengi umaskini wa wakulima bali wakulima maskini. Vivyo hivyo kwenye sekta zingine zote za uzalishaji (uvuvi, mifugo, viwanda, nk) lengo ni wahusika.
 
Back
Top Bottom