Mikakati urais CCM 2015 yashika kasi

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
*Makundi yaanza kujipanga mjini Dodoma
*Wapambe waitwa kutathmini hali ya hewa

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIKA hatua inayoonesha kuwa mbio za kuwania urais mwaka 2015 zimeanza, makundi ya wanasiasa yameanza harakati kuunda mitandao huku wengine wakiita wapambe wao na kufanya mikutano kujua namna ya kujipanga.

Uchaguzi mkuu ujao utakuwa na mvuto wa aina yake kwani Tanzania itapata Rais wa Awamu ya Tano kwa mujibu wa katiba kutokana na kwamba Rais wa sasa Jakaya Kikwete kumaliza muda wake kikatiba.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini makundi ya wapambe wakimiminika mjini Dodoma kunakoendelea kufanyika mkutano wa pili wa Bunge la kumi la Jamhuri ya Muungano.

Habari za kuaminika zilizolifikia Majira, zimeeleza kwamba baadhi ya vigogo wenye nia ya kuwania nafasi hiyo juzi na jana walikutana na makundi ya wapambe kwa lengo la kuweka sawa mitandao hiyo kwa ajili ya mwaka 2015.

Mmoja wa watu walioshiriki kwenye mikakati hiyo, alipoombwa na kuzungumzia vikao hivyo juzi kwa njia ya simu, hakukataa wala kuthibitisha jambo hilo bali alisema maandalizi yoyote ya kisiasa yanahitaji mipango na mikakati ya muda mrefu.

"Kweli nipo Dodoma, nimekutana na watu lakini si kwa ajili ya urais tu wa 2015, wengine ni marafiki zangu wa siku nyingi (alitaja majina),tuna mambo mengi ya kuzungumza ya kawaida kwani hata tukizungumzia urais kuna ubaya gani?" alihoji.

Ilielezwa kuwa mkakati huu ni awamu ya tatu baada ya ule wa kwanza na ya pili uliolenga kujiimarisha ndani ya bunge, kuonesha dalili chanya katika kutekeleza lengo hilo.

Awamu ya kwanza ya mkakati huo ililenga kuhakikisha wabunge wasiopungua 85 wanaounga mkono moja ya kambi zinazowania urais, wanapata nafasi ya kurudi au kuingia bungeni jambo ambalo limeelezwa kuwa lilifanikiwa.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, mkakati wa pili ulitajwa kuwa ni kuhakikisha makundi hayo yanashika nafasi nyeti ndani ya kamati mbalimbali za bunge, kazi ambayo nayo imeelezwa kuonesha mafanikio.

Uchunguzi wa Majira umebaini kuwa wapambe hao kutoka mikoa mbalimbali walikutana kwa nyakati tofauti na baadhi ya wanasiasa hao kuweka mikakati hiyo, wengine wakiwa makada wa chama tawala CCM kutoka mikoa na wilaya mbalimbali nchini.

"Haya mambo si madogo inawezekana hawa wanapima upepo ndio maana wameamua kuita watu mbalimbali, waangalie watu mikoani wanasemaje na wanajipanga vipi? kilisema chanzo chetu.

Baadhi ya wanasiasa ambao wamekuwa wakitajwa kuwania urais mwaka 2015 ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Benard Membe, mawaziri wakuu wa zamani Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredereck Sumaye, Waziri wa Maji Profesa Mark Mwandosya.
 
PHP:
rutashubanyuma said...   Ni mama profesa Tibaijuka tu ndiyo kimbilio la CCM 2015...................... 
   February 14, 2011 8:00 AM   [IMG]http://www.blogger.com/img/icon_delete13.gif[/IMG]

My crystal ball leads me to believe this to be CCM gospel truth..............................
 
Wacha wachome mafuta ya usiku wa manane kupanga mikakati lakini ni vema wakajua kwamba uchaguzi ujao watu watapimwa kwa usafi na uzalendo wao kwa nchi kwanza. Hawa wanaokusanya na kuzoa kama vile wanahamia sayari nyingine wataishia hivyo!
 
Wacha wachome mafuta ya usiku wa manane kupanga mikakati lakini ni vema wakajua kwamba uchaguzi ujao watu watapimwa kwa usafi na uzalendo wao kwa nchi kwanza. Hawa wanaokusanya na kuzoa kama vile wanahamia sayari nyingine wataishia hivyo!

Let us be realistic. Mwenye uwezo wa kuhonga zaidi, kufanya siasa za fitna na kuwalaghai wapiga kura ndiye atakayepita. Hii ni hali halisi ya CCM.
 
Kwa kuwa mikakati yenyewe siitofautishi na ile ya 'IVORY COAST' na uhakika kbs lazma watashnda. Lakini ndg zangu, hv nyie inawaingia akilini kwamba kwa uchaguzi wa haki na wa Demokrasia CCM wananafasi tena Tz? Tafakari mwenyewe na jbu utalipata.
 
Rutashubanyuma: Nani alikuambia kuwa huyo mama anakubalika?? Au kwa sababu anatokea huko huko, Tunataka kufumua system yote
 
mi nataka waendelee kuwa na makundi ili wenyewe waleta mageuzi wapite katikati...
 
Nawatakia kila la heri katika maandalizi yao ya kuisindikiza CHADEMA kwenda Ikulu 2015
 
PHP:
rutashubanyuma said...   Ni mama profesa Tibaijuka tu ndiyo kimbilio la CCM 2015...................... 
   February 14, 2011 8:00 AM   [IMG]http://www.blogger.com/img/icon_delete13.gif[/IMG]

My crystal ball leads me to believe this to be CCM gospel truth..............................

Mkuu, nimecheka kidogo baada ya mchangiaji mmoja hapo juu kutilia shaka wazo lako kukaa "kimajimbo" zaidi. Lakini naamini kawaida yako ni kutoa mawazo yenye hoja makini. Isipokuwa huyu mama nina matatizo mawili naye. Kwanza, sidhani kama ni "mtu wa ndani" katika chama hicho kiasi cha kupewa nafasi hiyo. Pili, sijui ni mwanamapinduzi kiasi gani.

Alitoa changamoto sana enzi za BAWATA. Lakini, jinsi alivyohangaika kurejea kwenye siasa kupitia CCM kama ilivyo, sidhani kama anayo nia na uwezo wa kuipindua CCM imfuate yeye zaidi ya yeye kutaka kukubalika na status quo ya CCM ambayo, kusema kweli, haiendi na mtu wa aina yake (same for the Mwakyembes, magufulis, Kilangos, Sendekas, n.k.).

Tumaini pekee kwa mtu wa aina yake ndani ya CCM ni kuingiza mabadiliko makubwa na kuifanya CCM "imfuate" yeye! Anataka hivyo? Na, anao ubavu huo?
 
Na sisi wana JF tumwandee mtu wetu wa kugombea Uraisi, kwa kuanzia nampendekeza Mzee Mwanakijiji
 
CCM hawapati kitu 2015, Rais atatoka CHADEMA .......watu makini, ufisadi umeshaitafuna CCM
 
PHP:
rutashubanyuma said... Ni mama profesa Tibaijuka tu ndiyo kimbilio la CCM 2015...................... 
February 14, 2011 8:00 AM [IMG]http://www.blogger.com/img/icon_delete13.gif[/IMG]

My crystal ball leads me to believe this to be CCM gospel truth..............................

Ruta mkuu ukabila utakumaliza kwa taarifa yako Mama Tiba hana mizizi ndani ya CCM ni mgeni hajui majungu sawa sawa yaliyompata Salimu yatampata Mama akijaribu kukamata Fomu ya Magogoni upo mkuu.

 
lowasa akiingia kwenye kinyanganyiro atasumbua kidogo ila hao paka wengine hawana ujanja
 
bila lowasa na rostam kutiwa risasi tatu tatu kichwani uraisi wa 2015 utatokana na maamuzi yao hao wawili tu, wadanganyika mnalo hili
 
Back
Top Bottom