mikakati hii ya uchaguzi ya vyama vyetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mikakati hii ya uchaguzi ya vyama vyetu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by johnmashilatu, Oct 12, 2010.

 1. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #1
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  Nimekuwa nikifuatilia jinsi vyama vyetu vinavyofanya kampeni zake, hususan jinsi ya kuwafikishia wananchi, wapiga kura, taarifa mbalimbali

  zipo njia nyingi lakini moja ni ile ya kutumia vyombo vya habari, (magazeti, radio na TV) vyama hivi viko mstari wa mbele zaidi kutumia magazeti na Tv zaidi ili kufikisha ujumbe wake

  lakini kwa kiasi fulani nafikiri hawatendi haki kw awapiga kura walioko vijijini, maeneo kama Murusagamba kule Ngara magazeti hayafiki na hata mjini Ngara kwenyewe magazeti yanafika baada ya siku tatu, lakini wenye uwezo wa kuyasoma ni wachache sana. wengi hawaelewi nini maana ya raia mwema, mwananchi n.k

  TV ni vile vile, ni watu wachache wenye umeme na kumiliki Tv!

  bado naamini kuwa radio zina mchango katika kuwafikia watu wengi zaidi

  Naambiwa kuwa wana mikakati wa wagombea wa nafasi za urais wa Tanzania wamekataa kutumia radio kwa vile ni njia ya kizamani

  vinginevyo utaelezaje hatua ya wagombea hawa kukataa kutumia radio kama kwizera yenye usikivu mzuri katika mikoa ya Kigoma, kagera na Rukwa

  Naambiwa kuwa wana mikakati hao ikiwa ni pamoja na wale wa Dr Slaa ambaye baadaye leo atakwenda wamekataa kulipia chini ya shilingi lai tano ili mkutano wao utangazwe moja kwa moja!

  Tujadili
   
Loading...