Mikael P Aweda aanza kuivuruga CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mikael P Aweda aanza kuivuruga CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by NyepesiNyepesi, Jul 26, 2011.

 1. N

  NyepesiNyepesi Member

  #1
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Taarifa za uhakika kabisa toka chanzo cha kuaminika ndani ya uongozi wa chadema jimbo la ukonga zinasema kwamba Bw. Mikael P. Aweda ambaye kwa sasa ni mwenyekiti wa chadema jimbo la ubungo, amechukua fomu za kuwania nafasi ya uenyekiti jimbo la ukonga.

  Kwa mujibu wa katiba ya chadema bw Aweda atashikilia nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chadema jimbo la ubungo hadi mwaka 2014 hapo utakapofanyika tena uchaguzi mkuu ndani ya chama.

  Katika hali ya kushangaza mwenyekiti huyu amechukua fomu za kuwania uenyekiti wa chadema jimbo la ukonga. Jimbo la ukonga linatarajia kufanya uchaguzi wake mnamo tarehe 31/07/2011 kufuatia kugawanywa na NEC(tume ya taifa ya uchaguzi) kwa jimbo hilo kulikofanyika mwaka jana na kuzaliwa kwa jimbo la segerea.

  Bw Aweda alianza kuonekana akipita pita katika matawi mbalimbali ya jimbo la ukonga pasipo hata kumfahamisha aliyekuwa mwenyekiti wa jimbo la ukonga mzee Binagi, na alienda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kushiriki na kusimamia baadhi ya chaguzi za matawi ya chadema ndani ya jimbo la ukonga.

  Kutokana na hali hiyo ya bw Aweda kujitosa kuwania uenyekiti wa jimbo la ukonga, amesababisha mtafaruku miongoni mwa viongozi na wanachama wa ukonga wakihoji kulikoni akimbie kutoka ubungo kuja ukonga?? Na kitu cha kushangaza amechukua fomu kugombea ukonga huku akiwa hajajiuzulu nafasi yake ya uenyekiti jimboni ubungo.

  Hii ni dalili mbaya kwa kiongozi mkubwa kama yeye anayepaswa kuheshimu katiba ya chama pamoja na imani kubwa aliyopewa na wanachadema wa ubungo. Kama ameamua kuwasaliti wanaubungo basi hata wanaukonga hawatomuamini, kwakuwa ameonyesha dalili zote za kutoaminika na usaliti wa demokrasia.

  Ushauri wangu kwa uongozi wa juu wa chadema, kuanzia uongozi wa mkoa wa dsm hadi uongozi wa taifa ni kumuangalia kwa makini mtu huyu asijekuwa ana agenda za siri dhidi ya chadema kwani wakati huu ambapo uongozi wa jimbo la ukonga wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanashinda chaguzi zote zijazo, wamekuwa wakifungua matawi maeneo mbalimbali kuanzia kitunda, kivule, ukonga, pugu na chanika lakini sasa bw Aweda anaonekana kuwakatisha tamaa na kuleta mvurugano hadi kusababisha mzee binagi kutorejesha fomu za kugombea uenyekiti wa jimbo.

  Kwa kuwa bw. Aweda ni mdau hapa JF namuomba ajitokeze hadharani kukanusha habari hii kama sio ya kweli, ama vinginevyo athibitishe kama anagombea nafasi hiyo na atoe ushahidi kwamba amejiuzulu nafasi yake ubungo ili asionekane ni mtu mwenye tamaa na ubinafsi.

  Naomba kuwasilisha.
   
 2. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Kama kapata baraka za Mbowe hakuna tatizo! Hongera Mikael P Aweda! Aikaambee
   
 3. m

  mtotomagwanda Member

  #3
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ntalitolea ufafanuzi hili,mana ni la chama
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa Dr. Kitila Mkumbo ningependa kusikia kauli yako juu ya hizi tuhuma kwa kuwa wewe ni kiongozi wa juu wa chadema lakini pia unaweza kunisaidia kufahamu katiba yenu inaruhusu jambo kama hili?

  Tafadhali mkuu nimekuona uko online, naomba muongozo wako.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ulivyoomba nikadhani wewe ndiye mleta mada NyepesiNyepesi lakini anyway unajuaje hizi habari ni za uhakika.
   
 6. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kuku mgeni hakosi kamba mguuni. Karibu jamvini!!!!

  Tiba
   
 7. p

  politiki JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  cha msingi kama katiba inaruhusu sioni ubaya wake let the democracy takes its roots, kama watu hawamtaki he will be
  voted out so there is nothing to fear. demokrasia ndio jawabu chama ni mali ya watu let the people decide for themselves.
   
 8. F

  FredKavishe Verified User

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,090
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Navyojua mimi amehama jimbo la ubungo sasa anaishi ukonga'kwanini asigombee acha siasa za kizandiki'siku hizi mtu anakaa ukonga mwacheni agombee huko lakini jimbo la ubungo ataacha kuwa mwenyekiti'
   
 9. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ukiona hivyo hamna chama mtu mmoja anakuwa mkt wa majimbo mawili!!!!
   
 10. m

  mtotomagwanda Member

  #10
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uwanja ni mpya ila timu ni ileile thenx TIBA.MI NI COMREDY
   
 11. N

  NyepesiNyepesi Member

  #11
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtu kutaka kujua kutoka kwa insiders, ambaye pia ni kiongozi wa ngazi ya juu ya chama kuna ubaya gani?

  Kama habari hizi ni za kweli ama siyo za kweli siwezi kujua, anayeujua ukweli ni mtoa habari na mtuhumiwa.

  Na maadam mtuhumiwa yuko hapa jamvini, nasubiri majibu yake!!
   
 12. N

  NyepesiNyepesi Member

  #12
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1.Unaweza kuthibitisha kwamba anaishi ukonga? anakaa kata gani ama mtaa gani??
  2.Kwanini asijiuzulu kwanza nafasi yake ubungo ndipo aende kugombea ukonga? kwanini agombee ukonga wakati bado ni mwenyekiti wa ubungo?
  3.Nani anayefanya siasa za kizandiki kama si yeye na wewe?
   
 13. N

  NyepesiNyepesi Member

  #13
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki ndicho kituko anachotaka kuleta huyu mwenyekiti wa ubungo na itakuwa ajabu kwa chadema kukubali upuuzi huu.
   
 14. N

  NyepesiNyepesi Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninasubiri kusikia kutoka kwa viongozi wa chadema kama katiba ina ruhusu mtu mmoja kushikilia nafasi mbili za uongozi katika majimbo mawili tofauti.
   
 15. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Acha kuleta mambo ya kiccm, kwani jmbo ni mali ya mtu binafsi?
   
 16. G

  Gurti JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimesikia, Mikael P Aweda alikuwa m/kiti wa Chadema Ubungo akiwa anaishi Ubungo Kisiwani, manisipaa ya kinondoni. Sasa amehamia manisipaa ya ILALA na nimesikia anajenga kitunda . Sasa kama anaishi ilala aendele kuwa kiongozi kinondoni? Binafsi sioni tatizo kwa kuwa ninamfahamu sana nitampigia simu nijue undani wa suala hili.
   
 17. N

  NyepesiNyepesi Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jimbo si mali ya mtu lakini bw aweda ndo anataka kuleta mambo ya kimagamba ndani ya chadema, kwanini anakuwa na tamaa ya kutaka kujirundikia vyeo??

  Kama ni kweli hebu jibu maswali yangu haya hapa chini,

   
 18. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #18
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  hata hii ya mtotomagwanda paw anaweza akaipotezea, teh teh teh! hiyo ya zamani ulipigwa ban ya maisha nini?
   
 19. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #19
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180

  sasa hapo mtu amevuruga vipi chadema? au kimekuuma kwa kuwa na wewe uko huko ukonga na huna popularity?
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Jul 27, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,998
  Likes Received: 582
  Trophy Points: 280
  sasa hiyo nyepesi uliipata wapi km sio kwa insiders? (sijui insiders unamaanisha watu wa ndani???)))
  na km huna uhakika unaiweka humu ya nini?
   
Loading...