Mijitusi ya Lusinde Vs Sugu - Clouds FM

BMM

Member
Jul 20, 2011
9
3
Nimeona clip ya Lusinde akiporomosha kampeni za mijitusi huko Arumeru kupitia You Tube, lakini pia nilisikiliza nyimbo ya Sugu kupitia You Tube, ki ukweli hawa jamaa waliporomosha Mijitusi lakini wote wakiwa na sababu zao binafsi za kufanya hivyo!!!!
Nikabahatika pia kusikia siku zote mbili Clouds walivyochambua hizo clip na nyimbo;

Kiufupi wailaani sana na kuiponda sana nyimbo ya Sugu (hadi kuhusisha boss wao mkubwa pale kuiongelea na kudiriki kuiplay hiyo nyimbo kidogo),Lakini hii ya Lusinde jamaa kaishia kushangilia tu (japo kwa kejeli fulani) lakini hawakuchambua kama walivofanya kwa Sugu.

Hoja: Binafsi Clouds naipenda na vijana wengi najua huwa tunaisikiliza hasa wakati wa asubuhi tuendapo ktk mihangaiko na jioni tukiwa tunarudi, lakini sijaridhishwa na utendaji kazi wake hasa linapokuja suala la kisiasa, Je wanataka kuniaminisha kuwa Clouds ni mashabiki wa chama fulani?na mm kama kijana nahitaji habari za kisiasa ya kishabiki? au kuchambua ni nani na nani yupo sawa kimalengo na mtizamo?

Ushauri: Usawa na Haki katika Media ni muhimu sana ktk kukuza demokrasia na maendeleo, Clouds pls revisit this angle!
 
Mmoja aliporomosha kabla hajawa mbunge, mwingine aliporomosha akiwa mbunge, tena kwenye kampeni. Kuna tofauti
 
nilijiuzuru kuisikiliza hii radio siku nyingi sana na sijui kama bado ipo hadi sasa
 
Wanamwita sugu........nani.........sugu.....sugu........sugu, ahaaahahaahaaa. Ni vizuri ungetuwekea huo wimbo wa sugu au utupe link yake.........tuone
 
Redio ni nzuri ila inaalibiwa na baadhi ya watangazaji wake wanajifanya kila kitu wanajua wangine tunajua wanajipendekeza kwa baadhi ya viongozi upande wa Magamba.
 
Kuna mtu anaitwa Kibonde, huyu nafikiri anawaangusha sana. Sijui shule yake vizuri ila naidoubt. Jamaa anajifanya anajua kilakitu wkt mi sioni cha maana zaidi ya comedy zake. Hando yuko nondo, actualy ni kwa vile vicheko vyake pale asubuhi vimemualert kila mtu na watu tumeingia u-tb na kuiona ile clip mitusi. Clouds wanatambua vijana wanataka nini sasa, alarm nyingi zimeshawagongea mfano Bushoke alipozomewa pale leaders nk. hata kupatanishwa na Sugu nafikiri ni mision. wajipange wanaweza kukosa suport ya serikali(CDM govt) like how they r enjoying now.
 
Redio ni nzuri ila inaalibiwa na baadhi ya watangazaji wake wanajifanya kila kitu wanajua wangine tunajua wanajipendekeza kwa baadhi ya viongozi upande wa Magamba.

oya hii langi yako sio. utafanya watu wasisome post zako.
 
Redio ni nzuri ila inaalibiwa na baadhi ya watangazaji wake wanajifanya kila kitu wanajua wangine tunajua wanajipendekeza kwa baadhi ya viongozi upande wa Magamba.

watu wengine bwana!ebu toa mirangi yako inatuumiza macho.
 
mmh mimi nawajua fika hawa jamaa wa clouds radio ni watu wa lowasa ndio maana kila kukicha wanapenda sana kumpamba lowasa. nimejaribu kufanya utafiti nimegundua ya kwamba habari yoyote nzuri iliyoandikwa juu ya lowasa wao wanapenda kuipamba sana. lakini itokee habari kama ya dr mwakyembe au sitta huwa wanaruka wala hawajishughulishi kuisoma habari hiyo. kama kuna mtu anabisha aanze kuwafuatilia leo.gelard hando na mwenzake paul james hawa wote ni vibaraka no 1 wa lowasa hakuna asie jua hili. nimeshawahi kuwakuta wakiteta pamoja na fredi lowasa.hawa hawana cha kuniambia ni washenzi tu.
Wamekosa akili za kufikiri sawasawa, wao wanadhani kuwa eti lowasa atakuja kuwa president,huu ni wendawazimu uliopitiliza kabisa.
Ushauri wa bure kwenu ni kwamba, angalieni lowasa wenu alivyoumbuka arusha.amekuwa akijitamba kuwa eti yeye anaheshimika sana arusha.sasa mbona amepigwa chini.kutoa mapesa meeeengi hakukufua dafu.mwizi ni mwizi tu, mchafu ni mchafu tu hawezi kujisafisha na maji taka.nawaambia lowasa wenu hana lolote.kwanza tayari kesha pararise upande mmoja.
 
don't worry about wazushi clouds itakufa kama tbc ni upepo tu waache wajisahau labda wataajiriwa na uhuru radio vijana wa leo wanatka kumuona sumari na sio lusinde waulizeni vizuri,mzalendo iko wapi,uhuru iko wapi rtd iko wapi na sukita imezikwa wapi ni mashoga wa watu hao bana.
 
popote ulipo kijana wa dar na vitongoji vyake jaribu kubadilisha matangazo yako kupitia redio nyingine totote na mjihadhari na clouds fm na tbc hawa ni mawakala wa mafisadi hivyo peleka ujumbe huu kwa mwanamageuzi yeyeote ili ikifika 2015 tutawahoji baada ya kuchukua majimbo yote ya dar.mungu walaani clouds kwani wana damu ya magamba.inshalah
 
oya hii langi yako sio. utafanya watu wasisome post zako.

Mimi nimeona tu huo mstari wa NAPITA nikapita kwa kuwa rangi aliyoitumia si rafiki wa macho. Nadhani hajui rangi rafiki kwa macho.

Heri uliyeamua kumwambia labda atajirekebisha na kuacha kuumiza macho yetu wasomaji.
 
Back
Top Bottom