Miito na mialiko ya kuzimu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,775
699,200
Kuzimu hakushibi wafu... Kila jambo lina nyakati na majira yake... Kuzimu nako kuna majira... Majira ya uhitaji wa wafu... Kwasababu ya mahitaji na matendo ya binadamu... Binadamu wanaoipa haki kisogo, utu wema, tafakuri na upendo.... Matendo yake ya ubinafsi huzaa chuki, udhalimu, kisasi, rohombaya na mauaji ya wasio hatia... Ni miito na mialiko ya kuzimu......

Majira yake ndio haya... Nyakati zake ndio hizi... Nyakati za harakati za kukutana ndugu jamaa na marafiki... Wavizia uhai, wapenda kafara na wale wa mazindiko... Mumiani wa damu za watu wanatega sasa.....! Makinika

Wanatega sasa... Wametega hata kitambo... Njia panda, barabara kuu, mtoni, kwenye kilima, mteremko na kilindoni... Hukuwa na safari ya kutoka, hukuwa na mpango wa kusafiri na wala hujisikii kufanya hivyo lakini ghafla unabadili mawazo... Nguvu kubwa isiyojulikana inakushawishi, inakuvuta inakutaka utoke... Uende! Mwishoni unakubaliana nayo unatoka, unaenda unasafiri... Kumbe wanakusubiri...

Nyakati za majira ya matukio makubwa, matukio ya mwaka, matukio ya kijamii na kifamilia, ya furaha na ya huzuni... Miito na mialiko ya kuzimu huwa si haba
Ni vipindi vya nyakati kama hizi roho yako inaposita kufanya jambo usilazimishe... Isikilize kwakuwa inaona zaidi ya kuona... Lakini pia kama wewe ni mtu wa ibada fanya ibada, fanya sala kabla hujatoa mguu wako nje, kabla hujadanda kipandwa...
Fanya dua, ombea safari.. Ombea kipandwa.. Ombea dereva... Ombea njia.. Ombea na wasafiri wote wasafirio angani nchi kavu na baharini... Kwa rehema za mwenyezi Mungu tuumalize mwaka kwa amani na furaha...

Aaamen... Kukichwa kutambazuka lakini kabla jua halijachomoza kiza huwa totoro... Barikiwa wewe utakayebahatika kusoma ujumbe huu... Nakuombea miito na mialiko ya kuzimu ikupitie mbali wewe na familia yako, jamaa zako marafiki na wote wenye mapenzi mema!

Imendikwa leo
Jumamosi asubuhi
Tarehe 15.12.2018
Saa 08: 45 asubuhi
Kilingeni Msata
Mkoa wa pwani
Jr...!
 
Hahaha haya mkuu ngoja tujongee. Hivi kuzimu kuna walio hai pia au wote ni wafu?!
Ni wakati gani ajali ikitokea unaweza kusema ni mapenzi ya mungu?! Na kama sio kazi yake unajuaje?!
Kuzimu kuna wafu tu... I mean roho za wafu...
Hakuna kifo kinachokosa sababu...
Ni ngumu kufahamu ni kifo cha aina gani, hata hivyo hata tukijua haisaidii.. Muhimu ni kuomba dua na sala za kinga kwakuwa kifo hakina vipuri
 
Kuzimu kuna wafu tu... I mean roho za wafu...
Hakuna kifo kinachokosa sababu...
Ni ngumu kufahamu ni kifo cha aina gani, hata hivyo hata tukijua haisaidii.. Muhimu ni kuomba dua na sala za kinga kwakuwa kifo hakina vipuri
Sasa huko kuzimu nani anakusanya hizo roho na ili iweje?! Binadamu tunajua kila uhai una mwisho yani kifo, sasa kwanini tuogope kufa kama ni kitu kilichopo, hatujui ni kifo gani ni mapenzi yake Mungu na kipi siyo, kama ndivyo kwanini tuombe ili tusife?! Kwanini tusisubiri matokeo, hakuna hajuaye siku wala saa.
Kama kuna watu wanaweza kukutega ufe, wao wanafaidikaje na mauti yako?! Je wao wataishi milele?!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom