Miili minne yaokotwa kichakani Handeni, miwili ikitambulika

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Kuna matukio ya kuokotwa kwa miili ya wanaume watatu na mwanamke mmoja katika maeneo tofauti ya Wilaya ya Handeni, Mkoa wa Tanga.

Kati ya miili hiyo, mwili wa mwanaume mmoja, kutokana na uchunguzi uliofanyika, ulibainika kuwa ni wa Benard Wilson Masaka, Mgogo (43), Mfanyabiashara wa nyama (Bucha) Mkazi wa Manispaa ya Morogoro, ambapo mnamo tarehe 03 Julai 2025, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro alitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu tukio hilo.

Chanzo cha mauaji hayo kilihusishwa kuwa ni wivu wa kibiashara.

Watuhumiwa waliotajwa kuhusika katika mauaji hayo walikamatwa na tayari wamefikishwa mahakamani.
Aidha, miili mingine miwili ya wanaume, ambayo bado haijatambuliwa, ilikutwa imetupwa porini katika maeneo tofauti ndani ya Wilaya ya Handeni, na inaendelea kuhifadhiwa kwa ajili ya utambuzi na uchunguzi zaidi.

Kwa upande mwingine, mwili wa mwanamke mmoja uliokotwa katika Kijiji cha Mkata, Wilaya ya Handeni, mnamo Februari 28 2025, ambapo uchunguzi ulibaini kuwa ni Fatuma Athuman (24), mkazi wa Kidereko, Handeni.

Watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya mwanamke huyo wamekamatwa, na uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kukamilishwa ili hatua nyingine za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linaendelea kushirikiana na Mikoa mingine kuhakikisha wahalifu wote wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria, na linatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kwa wakati kuhusu viashiria vyovyote vya uhalifu katika maeneo yao.

1752497349130.png
 
Vp tena au ndiyo mambo ya Uchaguzi tunatoaga kafala....Poleni wafiwa.
 
Ingekuwa kipindi cha JPM wangesema mengi sana.
 
Mapori ya Handeni yanatumika sana kwa kazi chafu
 
Back
Top Bottom